Zitto amkabidhi Maalim Seif kadi namba 1, Babu Duni namba 10

Mimi Nahisi Maalim alikuwa aanzishe Chama kingine na sio kujiunga vyama vilivopo... yaani kwenye video hio thumbnail hapo ni kama hili wazo limemjia afu sasa ni too late....

Huwa na kawaida ya kusema kuwa CCM ni zaidi ya chama cha siasa, hii ni taasisi kabisa na imejipanga vyema kwenye mipango yake.

Naamini 2020 Zanzibar utafanyika uchaguzi wa haki na uwazi kabisa visiwani. CCM tayari wana confidence ya kuwa CUF haitoweza kuwa tishio tena na ACT haitopata kura za kutishia ushindi wa CCM hii ni kwa sababu ukweli usemwe, kuna watu wamechoka na Maalim na siasa za kupigwa kalenda, wapo watu wengi ambao tayari wamegive up na hili lita affect idadi atakazopata maalim 2020.

Matokeo yakitoka, dunia nzima itashuhudia kuwa CCM imepata ushindi wa kihalali na CUF aliekuwa mpinzani mkuu ameangushwa vibaya, jambo hili litatumika kama uthibitisho wa kuwa CUF hawakuwahi kuibiwa kura na ule ushindi wa kishindo 2016 ulikuwa kweli wa kishindo.

Hii ni movie na director ni CCM!

Mkuu Maalim seif aliliona hilo kabla ya wewe kuandika hapa lakini shida ingekuja icho chama msajili asingekisajili ata kwa bahati mbaya. na uko Act sidhani kama kutakuwa na salama mkakati ni maalim seif asigombee tena urais zanzibar ni mwimba mkali kwa chama tawala kote Tanzania
 
Man, huzijui siasa za Zanzibar! NInachokuambia sio kukalia ushabiki bali nazifahamu siasa za Zanzibar na Wazannzibar kwa ujumla!

Kwanza, kwamba eti angeweza kumtumia mtu kusajiri chama, hicho ni kiroja! CCJ ilifia wapi?! Kwani akina Samuel Sitta et. al walikuwa front?! Tendwa hakuichinjia baharini CCJ?!

Kwamba nchi haitokani na makaratasi sio hoja ya mada yako kwa sababu, kama unaamini hivyo, sasa ulikuwa na sababu gani ya kuona great move kwa Maalimu ni kuanzisha chama ikiwa unafahamu hata iwe vipi CCM hawawezi kutoka nchi kwa kutumia makaratasi?! Hoja hapa ni kwamba, wana-CUF Zanzibar watamfuata Seif kokote kule as long as itakuwa ni upinzani! Zanzibar upinzani peke yake sio hoja bali ni upinzani unaoongozwa na Maalimu Seif! Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana hata mkongwe Hamad Rashid ameshindwa kufurukuta baada ya kuanzisha chama chake! Hiyo ni kuonesha issue sio upinzani bali ni upinzani ulio chini ya nani!

Siasa ya Zanzibar sasa hivi sio ya zamani... Nakushauri uje ukae na watu na uwasikilize maoni yao. They dont take it seriously kama zamani. Wamechoka kudanganywa.... Baada tikitaka ya CCM, Maalim aliishia kuwapa watu hope ya uongo na hapa ndio watu wakajua kuwa huu ni upuuzi. Nakushauri, rudi nyuma usome tena siasa ya Zanzibar na watu wake akisha wafananishe na leo. Siku izi watu wanatizama yao yanawaendea basi, wameshajifunza kuwa hakuna liwalo.

By the way, rudia post yangu nimesema kuwa "NAHISI" kama unajua lugha basi ungeelewa kama huo ulikuwa mtazamo. Kwani kuhamia ACT sio kiroja unafikiri? Tayari kuna watu wanaanza kusema Karma imefanya kazi, kama alivowatimua watu kwa figisu CUF na yeye yamemkuta hayo hayo sasa.

Sasa unasema kuwa Seif atafuatwa popote as long as upinzani, mwanzo uliseme popote atakapoenda wafuasi watamfuata. Sasa ivi iwe ni upinzani.

Ukitaka kujua kwanini nilisema Maalim ni vyema angeanzisha chama chake, kwa sababu hata ACT nayo imeshakuwa ikishutumiwa kutumika na CCM huyo Zitto kabwe.

Unamzungumzia Hamad Rashid? Ni Waziri saivi, anaefurukuta ni Maalim kwa sasa chama kapokonywa kajiunga na chama cha Zitto ambae amekwisha shutumiwa na hao hao wapinzani kuwa anatumika.
 
Unaamini kisichokuwa sahihi!
Hebu Nenda Zanzibar ukaangalie Shangwe Mitaani Wakubwa kwa Wadogo Wake kwa Waume wakipaka Rangi majengo Mapya ya ACT.

Yani Zanzibar imeshageuka Ranging ya Purple/Violet ndani ya Masaa 24 tu.

Hata wakati wachama Kimoja Ndani ya Zanzibar watu waliuliwa, Wengine Walifungwa na Upinzani haukiwahi kukata tamaa wala kuisha.

Subiri tuone 2020 sio mbali.
Nimeona video ya KTV online watu wakisherekea Maalim kujiunga na ACT.... kwa wale watu niliowaona, ni funzo tosha kuwa Wazanzibari wamechoka na upuuzi wa siasa.... na ndio maana nakwambia wafuasi wa Maalim saiv sio wale wa Zamani.

Muulize Mkapa, alipeleka majeshi kuuwa watu pemba na vifaru akavileta zanzibar. Saivi ata wasiwasi hawana mana wanajua kama watu wanafanya yao.
 
Mkuu Maalim seif aliliona hilo kabla ya wewe kuandika hapa lakini shida ingekuja icho chama msajili asingekisajili ata kwa bahati mbaya. na uko Act sidhani kama kutakuwa na salama mkakati ni maalim seif asigombee tena urais zanzibar ni mwimba mkali kwa chama tawala kote Tanzania

Ni vyema ukajifunza siasa za zanzibar, Wazanzibari ni watu wasioyumbishwa neno analolitoa maalim seif ni hilo hilo ata kwa mtoto mchanga anayezaliwa leo, wazanzibari sasa wote wameungana kutaka mabadiliko utakuja kunambia,

Iyo ACT ni ticket tu ya kumuakilisha maalim kwenye uchaguzi mkuu ujao lakini sympathy ya wazanzibari iko pale pale ama kuongezeka zaidi kila uchao. Maalim Seif ndiye aliyebeba matumaini ya Wazanzibari. Jana tu alipotangaza sasa nenda zanzibar emu tembelea majimbo yote yaliyokuwa ya CUF utapata kupanua kichwa chako maalim seif ni mtu wa aina gani Zanzibar.
 
MMtu mzima Seif Sharif Hamad anapokabidhiwa kadi ya chama na mtoto mdogo Zitto Kabwe .Aiseee Lipumba kiboko
New CUF a.k.a Lipumba United Front..wakati mwingine vyama vya siasa vibadili mfumo wao wa mipaka ya mwenyekiti na kanuni za kumtengua mwenyekiti..nikitumia fikra za Amerikani naona Lipumba ni Putin wa CUF
 
Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewakabidhi kadi za uanachama wa chama hicho waliokuwa vigogo wa Chama cha Wananchi (CUF) huku Maalim Seif Sharif Hamad akipewa kadi namba moja na Juma Haji Duni akikabidhiwa kadi namba 10.

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo,

Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.

“Nawashukuru sana kwa kukubali ombi letu kwamba tuje tuchangie nguvu katika chama cha ACT- Wazalendo na ninyi hamkuwa na ajizi mkatuambia njooni na haukuwa uamuzi wa viongozi pekee bali wa wanachama,” amesema Maalim Seif
Weshajkzika wenyewe hawa wazee masikini wa Mungu! Jussa na ujuaji wake kwishilia mbali. Pole zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa ya Zanzibar sasa hivi sio ya zamani... Nakushauri uje ukae na watu na uwasikilize maoni yao. They dont take it seriously kama zamani. Wamechoka kudanganywa.... Baada tikitaka ya CCM, Maalim aliishia kuwapa watu hope ya uongo na hapa ndio watu wakajua kuwa huu ni upuuzi. Nakushauri, rudi nyuma usome tena siasa ya Zanzibar na watu wake akisha wafananishe na leo. Siku izi watu wanatizama yao yanawaendea basi, wameshajifunza kuwa hakuna liwalo.

By the way, rudia post yangu nimesema kuwa "NAHISI" kama unajua lugha basi ungeelewa kama huo ulikuwa mtazamo. Kwani kuhamia ACT sio kiroja unafikiri? Tayari kuna watu wanaanza kusema Karma imefanya kazi, kama alivowatimua watu kwa figisu CUF na yeye yamemkuta hayo hayo sasa.

Sasa unasema kuwa Seif atafuatwa popote as long as upinzani, mwanzo uliseme popote atakapoenda wafuasi watamfuata. Sasa ivi iwe ni upinzani.

Ukitaka kujua kwanini nilisema Maalim ni vyema angeanzisha chama chake, kwa sababu hata ACT nayo imeshakuwa ikishutumiwa kutumika na CCM huyo Zitto kabwe.

Unamzungumzia Hamad Rashid? Ni Waziri saivi, anaefurukuta ni Maalim kwa sasa chama kapokonywa kajiunga na chama cha Zitto ambae amekwisha shutumiwa na hao hao wapinzani kuwa anatumika.
We jamaa una matatizo?! Yaani kwa akili yako unatarajia kuna mtu anaweza kuzungumzia uwezekano wa Seif na CCM? Kuhusu kokote watamfuata, hiki ndicho nilisema:-

Kwamba CUF sio tishio tena Zanzibar, lazima ufahamu kwamba tatizo la CCM Zanzibar sio CUF bali Maalimu Seif na Wapemba walioikataa CCM! Kokote atakaoenda Maalim Seif, wafuasi wa CUF watamfuata na kuendelea kuwa mwiba kwa CCM! !
Sasa hivi hapo unashindwa kabisa kuona kwamba huko kokote nilikosema hakuwezi kuwa CCM?!

Kwamba, eti siasa za Zanzibar zimebadilika, narudia tena! Huzijui siasa za Zanzibar wewe vinginevyo usingeongea hilo jambo! Mpaka kesho, hususani Pemba, ukiweka Gogo vs CCM, Gogo litapigiwa kura!!! Wapemba wako very loyal kwa Maalimu Seif, na ndio maana wala haikushangaza jana ile ile kuona baadhi ya Ofisi za CUF zikipakwa rangi ya ACT huku bendera za CUF zikichomwa moto!!

Sasa kama unaamini Maalimu Seif hana tena ushawishi, wasome hapa The Citizen:
Even though it was still early to draw conclusions, party insiders told The Citizen that consideration was given to join a platform where Mr Hamad will still play as the first among equals in the opposition luminaries heading towards the 2020 elections. Reactions were swift in Mr Hamad’s base in the Isles, with party offices repainted and new flags raised to signify the change. Some party loyalists were seen burning CUF flags and carting away furniture from deserted offices.
Na hao ni The Citizen ambao wapo Bara! Tembelea mzalendo.net ambao ndio hutumiwa sana na Wazanzibar kisha uone reactions zao!

Moja ya articles kwenye Mzalendo, hiki ndicho wanaandika:
Ukweli umeonekana leo baada ya maalim tu alipotangaza kujiunga na ACT Wazalendo, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Mikoa mengine ya Bara. Bendera za CUF na Majengo yaliokuwa na rangi za CUF yalisafishwa within a mites also.. Ni maajabu makubwa yakuona wananchi wanao dai haki zao wamekuwa very sharp to react and adopt another Wings.

Kwa macho yako mwenyewe, hawa hapa:

Na hapo hata amsha amsha, ipo bado!!!
 
Mimi Nahisi Maalim alikuwa aanzishe Chama kingine na sio kujiunga vyama vilivopo... yaani kwenye video hio thumbnail hapo ni kama hili wazo limemjia afu sasa ni too late....

Huwa na kawaida ya kusema kuwa CCM ni zaidi ya chama cha siasa, hii ni taasisi kabisa na imejipanga vyema kwenye mipango yake.

Naamini 2020 Zanzibar utafanyika uchaguzi wa haki na uwazi kabisa visiwani. CCM tayari wana confidence ya kuwa CUF haitoweza kuwa tishio tena na ACT haitopata kura za kutishia ushindi wa CCM hii ni kwa sababu ukweli usemwe, kuna watu wamechoka na Maalim na siasa za kupigwa kalenda, wapo watu wengi ambao tayari wamegive up na hili lita affect idadi atakazopata maalim 2020.

Matokeo yakitoka, dunia nzima itashuhudia kuwa CCM imepata ushindi wa kihalali na CUF aliekuwa mpinzani mkuu ameangushwa vibaya, jambo hili litatumika kama uthibitisho wa kuwa CUF hawakuwahi kuibiwa kura na ule ushindi wa kishindo 2016 ulikuwa kweli wa kishindo.

Hii ni movie na director ni CCM!
Wangemuekea figisu nyingi tu.
 
kadi namba 1 huwa wanapewa waanzilishi wa Chama, ACT wazalendo wanataka kutuambia kadi namba 1 haikuwa na mwenye nayo, hapa wanatupa sababu ya kuamini Seif sharrif Hamad katoa mzigo mzito wa kukinunua hiki chama. Ujinga kama huu huwezi kuukuta katika Chama Cha Mapinduzi

..labda ilikuwa ya Mama Mghwira aliyekuwa mwenyekiti wa ACT na mgombea Uraisi 2015.
 
We jamaa una matatizo?! Yaani kwa akili yako unatarajia kuna mtu anaweza kuzungumzia uwezekano wa Seif na CCM? Kuhusu kokote watamfuata, hiki ndicho nilisema:-

Sasa hivi hapo unashindwa kabisa kuona kwamba huko kokote nilikosema hakuwezi kuwa CCM?!

Kwamba, eti siasa za Zanzibar zimebadilika, narudia tena! Huzijui siasa za Zanzibar wewe vinginevyo usingeongea hilo jambo! Mpaka kesho, hususani Pemba, ukiweka Gogo vs CCM, Gogo litapigiwa kura!!! Wapemba wako very loyal kwa Maalimu Seif, na ndio maana wala haikushangaza jana ile ile kuona baadhi ya Ofisi za CUF zikipakwa rangi ya ACT huku bendera za CUF zikichomwa moto!!

Sasa kama unaamini Maalimu Seif hana tena ushawishi, wasome hapa The Citizen:Na hao ni The Citizen ambao wapo Bara! Tembelea mzalendo.net ambao ndio hutumiwa sana na Wazanzibar kisha uone reactions zao!

Moja ya articles kwenye Mzalendo, hiki ndicho wanaandika:

Kwa macho yako mwenyewe, hawa hapa:

Na hapo hata amsha amsha, ipo bado!!!

We jamaa unanichekesha....

Video ulizoonesha ni wazi kuwa Watu wengi wako bize na mambo yao binafsi badala ya siasa.

Wewe sijui kama waijua zanzibar, wafuasi wa Maalim 2010 unawajua walivokuwa kweli? unanionesha video za watu 15 wakichoma na kushusha bendera halafu unasema kuwa eti Siasa ya Zanzibar ndio ile ile. Nakwambia ivi, CCM wangedeploy FFU Mjini kuwa standby na fujo. Ila leo hii FFU hawanaga habari... hujiulizi tu?
 
Back
Top Bottom