Zitto akutana na wahariri usiku huu Dar

Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi mkuu wa ACT Tanzania usiku huu amefanya mkutano na wahariri wakuu wa vyombo vya habari Tanzania.

Mkutano na wahariri umeenda sambamba na chakula cha jioni katika hoteli moja katikati ya jiji.

Zitto ametumia nafasi hiyo kuwaomba wahariri wamsaidie kuitangaza ACT Tanzania ili kiwe chama kikuu cha upinzani na kilete mapinduzi ya kweli katika siasa za Tanzania

Huu ni ukichaa tena HAUNA KIFANI, sisi tunataka KUWAONDOA MAFISADI/WEZI/WAHUJUMU NCHI, wewe unataka kuwa CHAMA KIKUU PINZANI? Kweli nimeamini sasa Sweet a.k.a CCM B ni WASALITI na hamna mpango wa kuwakomboa Watz.
Pia nilipta mashaka sana kusikia Mzalendo mwenye Mali nyingi sana kiasi kile na mkijifananisha na hayati Mpendwa/Kipenzi chetu Baba wa Taifa wakati yeye alikufa akiwa Maskini, ETI Kiongozi anamiliki Mali Nyingi Kiasi Kile ikiwemo Hammer na nyinginezo.

Adhabu ya Mungu yaja juu yenu nyote WANAFIKI.
 
Ni mtu mjinga pekee awezaye kubeza nguvu ya vyombo vya habari katika kukieneza Chama/Taarifa kwa wananchi.

Chombo cha Habari ni Kiungo Muhimu sana kati ya Taasisi na Wananchi. Msomi Zitto analitambua hilo wala hawezi kulipuuzia.

Vyombo vya Habari vilichangia sana kumpa kura nyingi Dr.Slaa 2010 ila ni wajinga pekee msioweza kulitambua hili.

Acheni watu makini wafanye Siasa, nyie kaeni hapa mkipiga Madomo kama desturi ya wabunge wenu akina Lissu na Lema mkija kustuka kutakuwa kumekucha.

Nyie enezeni chama kwenye magazeti huku CHADEMA mtaani wakipita nyumba kwa nyumba soonly hamtaamini kitakachotokea.
 
Kazi yake kuu ni kuitisha vikao vya chama ambavyo si vya kitaifa, halmashauri kuu wala kamati kuu. Na hata hivyo bado Kiongozi mkuu Taifa bwana Zitto ndie atakayekuwa
-kiongozi wa kusimamia, kufunza na kutoa maelekezo kuhusu shughuli zote za ACT
- mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama

No wonder amewekwa aliyewekwa kwa kivuli cha haki za mwanamke.... sidhani kama kuna mtu mwingine ambaye angekubali kuvikwa cheo hicho cha uenyekiti kivuli!

I just got caught by your signature
nimekupenda zaid ya mwanzo
 
Nadhani wana uhakika na viti viwili mpaka sasa, cha Zitto na Arfi Mbunge wa Mpanda.
viti hivyo havipo na kamwe hawawezi kuvipata, mpanda mjini wananchi walisha sema mapema CHADEMA wanakipenda ila akisimama Arfi hawatakichagua, hapo unapaswa kujiuliza kuna nini
 
Siasa ni ujanja na mbinu,hii mbinu ni nzuri na itazaa matunda I told u this guy is very smart politician

Usijidanganye atapata kura kwa kugawa vijirushwa kwa waandishi.Kazi ya chama cha siasa ni kukesha vijijini kueneza chama kwa wananchi na si vinginevyo.Unaweza kukesha ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo lakini hutaamini matokeo yakitoka
 
EHM amefundwa kazi ya ku-lobby ... Wahariri wamekunja kiasi gani jana Usiku? ZZK anachokifanya ni kuhalalisha matumizi ya ruzuku anazozipata kutoka CCM ...
 
Supreme Leader anawahonga Wahariri ubwabwa, he is using exactly technique of his sponsor (CCM) to common Mwananchi. The question is Editors will play?

Nimezungumza na wahariri mbalimbali na wamenihakikishia hawawezi kusaliti Taaluma yao kwa kupewa vijibahasha..

Sanasana ataendelea kuungwa mkono na magazeti ya CCM kama Uhuru,HabariLeo,JambaLeo na Raia Mwema
 
ZZK ni kila kitu katika ACT.

- Mkuu wa chama
- Mwenezi
- Nuru ya chama
- Kingunge wa chama
- Mganga wa chama
- Mwenyekiti wa chama
- Mlezi wa chama;
- Kichwa cha chama.
 
Kiwe chama kikuu cha upinzani ina maana hakipo kwa ajili kupigana kuwa chama kinachoongoza seriakali bali upinzani milele
 
Back
Top Bottom