Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
Pamoja na kwamba zitto anajengewa zengwe lakini huyu jamaa ana tabia ya ubinafsi fulani hivi na kujiamini sana kwa kujiona yeye ni kichwa sana!!
 
Zito ni KUWADI wa kisiasa na hilo linajulikana na kinachomkimbiza ni aibu zake baada kujua wenzake wameshamjua! kule kwetu kuna msemo usemao kuwa ' UKIWA MWONGO UJANANI BASI UKIWA MZEE UTAKUWA MCHAWI.:frusty:
 
Zito anajisikia na kujiona yeye anajua kila kitu na hili ndio tatizo lake. vipesa vya 'kuzukia' vinampa jeuri sana huyu mtu. hana tofauti hata kidogo na Shibuda!:bored:
 
Chase him out of the party, tumechoka hizo drama zenu cdm,jamaa inaonekana kawapanda kichwani,watanzania wapo zaidi ya milioni arobaini why always him fukuzeni full stop!!!!!
 
zemarcopolo...unapoteza muda mwingi sana kuijadili Chadema badala ya mambo ya msingi kwa Taifa letu fukara. Don't stoop that low brother.
Tuna upungufu mkubwa sana wa madaktari nchini na unajua. Rudi tusaidiane kurudisha japo kidogo kwa Watanzania waliojitolea jasho na damu ili sisi tusome. Tuna deni kwa Watanzania wenzetu.
Ni ushauri tu.
 
CHADEMA siku wakiamua kufanya siasa serious. tayari itakuwa too late. sasa hivi wanafanya mchezo wa kuigiza.
 
Ni kuhusu Zitto kabwe, huyu kijana anakivuruga sana chama kwa mwenendo wake anao ufanya ndani ya chama, unaopelekea kukidumaza chama. Kiukweli zito ni kirusi kinacho kimaliza chama.Hivyo mimi binafsi naomba kamati kuu kuchukua maamuzi magumu dhidi ya zito
 
WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea na kikao chake jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, amekacha kwa sababu za kiusalama.


Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mjadala kwenye vyombo vya habari, hasa alipoingia kwenye malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amekacha kikao hicho na badala yake ametoa taarifa ya kusafiri nje ya nchi.


Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa iliyotolewa kwa wajumbe wa mkutano huo na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, ilisema kuwa Zitto yuko safarini nchini Sudan, lakini anatarajia kuhudhuria mkutano huo wakati wowote.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe wameonyesha dhahiri kukerwa na hatua ya naibu katibu mkuu huyo kutoshiriki.


Waliolalamikia hatua hiyo walisema kuwa limekuwa jambo la kawaida kwa Zitto kutohudhuria vikao muhimu vya chama huku akijua fika kwamba yeye ndiye msaidizi mkuu wa katibu mkuu wa chama taifa.


Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho aliliambia gazeti hili kuwa moja ya ajenda zilizowasilishwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ni kuhusu mapato na matumizi ya chama ambayo alidai ingefaa Zitto awepo kuisikiliza.


Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ajenda hiyo ilikuwa muhimu kwa Zitto kuwepo kwani akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), amekuwa akidai kwamba CHADEMA na vyama vingine hawana hesabu za mapato na matumizi ya fedha za ruzuku wanazopata kila mwezi.
 
Vikao vyote vya kamati kuu viko kikatiba. Na hiki sio kikao cha dharura, mbona Zitto alijua toka januari kuwa tare20 /11 kutakuwa na kikao.kachukue hela nyingine uje upya

yaani zitto aache kuhudhuria vikao vya maana vyenye kubeba mustakabali wa nchi. ili aje kwenye vikao vya kupigana na matofali?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom