dosama
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 912
- 957
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 kupoteza maisha.
Jumapili iliyopita Oktoba 28,2018, Zitto alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.
Leo Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amezungumza na waandishi wa habari na kusema tuhuma alizotoa Zitto hazina ukweli wowote.
Amesema hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.
“Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”amesema Ottieno.
Kamanda huyo amewataka wanasiasa kuchukua tahadhali kwa taarifa wanazopewa na watu mbalimbali kabla ya kuzisambaza ili kuepuka kupotosha jamii.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma
>Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale
>Kigoma: Zaidi ya wananchi 100 wa Jamii ya Wanyantuzu, wadaiwa kupigwa risasi na Polisi
>Kigoma: Siri ya vurugu zilizosababisha mauaji ya askari wawili yavuja
>Zitto Kabwe aumbuka idadi ya vifo 100 Uvinza, RPC asema waliofariki ni wanne