Zitto aitwa Polisi kuthibitisha mauaji ya raia 100 wilayani Uvinza

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuwasilisha vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 kupoteza maisha.

Jumapili iliyopita Oktoba 28,2018, Zitto alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.

Leo Jumanne, Oktoba 30, 2018, Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amezungumza na waandishi wa habari na kusema tuhuma alizotoa Zitto hazina ukweli wowote.

Amesema hakuna watu 100 waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

“Hakuna watu mia moja waliouawa. Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”amesema Ottieno.

Kamanda huyo amewataka wanasiasa kuchukua tahadhali kwa taarifa wanazopewa na watu mbalimbali kabla ya kuzisambaza ili kuepuka kupotosha jamii.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
>Kigoma: Askari Polisi watatu wauawa kwa mishale
>Kigoma: Zaidi ya wananchi 100 wa Jamii ya Wanyantuzu, wadaiwa kupigwa risasi na Polisi
>Kigoma: Siri ya vurugu zilizosababisha mauaji ya askari wawili yavuja
>Zitto Kabwe aumbuka idadi ya vifo 100 Uvinza, RPC asema waliofariki ni wanne
 
mbona yeye hasemi wamekufa wangapi?? au hajafa hata mmoja?? zitto kawachokonoa ili waseme ukweli!!
 
NAULIZA TU HIVI ANGEKUWA MEMBE HAYA YANGETOKEA!? ( Uzi huu umetekwa)
1. Taarifa CAG 1.5 Trillion saga!?
2. Biashara haramu Wabunge na madiwani!?
3. Idadi kubwa mauaji askari na raia Kibiti na maeneo jirani!?
4. Miradi mikubwa kwa kasi ya Roketi Chatto airport, Bandari ....!?
5.Sakata la Makinikia lililopelekea uzalishaji kupunguza na Ajira 90% kupotea,Biashara wadau na taasisi
6. Ben na Anzory hatujui walipo!?
7. Roma na Wengine kutekwa na kutulizwa!?
8. Mh.Tundu Lissu kupigwa risasi kama nduli kwa jaribio kuuwawa!?
9. Musiba kuibuka na kuchafua watu kwa sauti ya maamlaka!?
10. Mahusiano ya kimataifa kudorora!?
11. Kumomonyoka kwa umoja na ustawi wa taifa letu!
12. Watoto wa kike waliopata ujauzito kukosa haki kuendelea na masomo!?
13. Lugha za kejeli kupuuza na kudhofisha uzazi wa mpango.!?
14. Halmal kuu ya CCM ,Kuwa na agenda rasmi kubariki biashara haramu na inayopoteza mabilioni na kutoka Tangazo rasmi ukomo 15 November 2018!?
15. Vitisho na dharau muhimili wa Bunge na PM, mfano Wabunge wa kusini wakitetea wakulima, kwamba mkuu angewafutilia mbali waheshimiwa 17 na kuwatandika shangazi zao!?
16. Vingi Akwilina Akwilini angepoteza maisha kikatili vile!?
17. Pangekuwa na wingi wa Kesi na vifungo Wanasiasa na wanaharakati !?.....

Jamani tuipende na kuifurahia nchi yetu maisha ni leo.
 
Jesh la polisi linajipendekeza tu ili lionekane linafanya kaz bt hutasikia uamzi wowote kufanyika wala feedback kuhusu hilo tukio
 
Mmmmmh ila watu mia ni parefu jamani.
Zito hebu fuatilia vizuri mana hiyo idadi inatia mashaka kwa kweli.
Angalau hata 20 lakini 100 hiyo si vita ya Kali kabisa kama ile ya Iraqi. Naamini Zito atakanusha kama taarifa yake sio sahihi lakini kama hatakanusha aje na orodha ya majina ya hao anaodai wameuawa . Ikiwezekana atafute majina na picha zao na wazazi wao au ndugu wathibitishe.

Hapa ndipo tunapohitaji uwazi na ukweli.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Mmmmmh ila watu mia ni parefu jamani.
Zito hebu fuatilia vizuri mana hiyo idadi inatia mashaka kwa kweli.
Angalau hata 20 lakini 100 hiyo si vita ya Kali kabisa kama ile ya Iraqi. Naamini Zito atakanusha kama taarifa yake sio sahihi lakini kama hatakanusha aje na orodha ya majina ya hao anaodai wameuawa . Ikiwezekana atafute majina na picha zao na wazazi wao au ndugu wathibitishe.

Hapa ndipo tunapohitaji uwazi na ukweli.
Samahani naomba nikuulize hivi unaakili timamu kweli?
Una imani na jeshi la police?
Kwahiyo kama ni watu ishirini ni sawa tu?
 
Samahani naomba nikuulize hivi unaakili timamu kweli?
Una imani na jeshi la police?
Kwahiyo kama ni watu ishirini ni sawa tu?
Sio sawa kuua hata mtu mmoja iwe ni Polisi au RAIA .
Na kama unasoma na kutafakari mie sijahalalisha mauji ya watu 20 .Ila nimeshtushwa na idadi aliyoitoa Zito ya Watu 100.

Ni lazima path ibitishe idadi hiyo kwa majina na ikiwezekana picha ili dunia ujue ukweli.
Vinginevyo akanushe kuwa hakua na taarifa sahihi .

Kwa akili yako timamu unafikiri ni rahisi kuwakusanya watu mia wa jamii ya wafugaji na kuwaua ,tena wa eneo ambalo ni wageni na wala sio wenyeji ? Hicho si kijiji pori kizima!!

Hizo habari zingesemwa hata kabla Zito hajasema.Ninavyojua Polisi wakiua hata mmtu mmoja taarifa zitasambaa kwa kasi nchi nzima sembuse watu 100.
Tena eti wa kabila la Wasukuma tena Wanyantuzu ambao ndio waliojaa kwenye Majeshi hayo hayo ikiwemo Polisi!
Polisi ni watoto wetu ni ndugu zetu toka kwenye makabila yetu . Kufanya kitendo kama hicho sio jambo rahisi kama Zito anavyotuaminisha.
Ujue Polisi nao ni binadamu ; haiwezekani wawaue watu mia wa kabila Moja ambalo miongoni mwa ni wa kabila hilo hilo?

Ndio maana nikasema bora angekisia watu 20 ili hata ikibainika kuwa ni watano au sita ,nane hivi ionekana ni makisio ya wananchi yanayotokana na hofu tu !!
Lakini watu 100 ni lazima liwe jambo la kuthibitishia umma na sio kulisema tu kisiasa , hayo yangekua ni mauaji ya kimbari kama ingekua ni kweli!!

Kwa kumuheshimu sana Zito Bado nasema aje na majina na picha za marehemu kama ikiwezekana authibitishie umma au akanishe.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Hili sio swaladogo uchungunzi sio ati.....kumburuza Zitto mwituni ili akaonyeshe maiti za wanyantuzu zilipo Hawa Polisi wa awamu hii mimi siwaamini kabisa wanaweza kuwazika maelfu ya wanyantuzu waluikuwa tayari wameshakuwa marehemu mwana mbate.
 
Back
Top Bottom