jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 25,020
- 22,559
Naelekea kuanza kukubaliana na bi Josephine kuwa daktari ndo mwenye taarifa sahihi,na pia mwenye wajibu wa kutoa taarifa.Na taarifa hizo hutoa kwa ndugu wa karibu wa mgonjwa.Ukweli ni kwamba hizo msg zilisambazwa kibiashara zaidi, Zitto yupo Muhimbili na anaendelea vizuri, kichwa ndio bado kinamsumbua. Sasa hicho chama chake ndio kilitakiwa kutoa ufafanuzi ili wananchi kwa ujumla wao wapate taarifa za uhakika rather than kila mtu kuzungumza anachokiju. Ila hizi taarifa ninazowapa ni za uhakika.
Pia kama chama kitatoa taarifa,basi taarifa hizo zitakuwa zimetoka kwa ndugu ambaye anawasiliana na daktari moja kwa moja.Ni ssue ya kifamilia na chama hakiwezi kuingilia.
chama kinaweza kutoa taarifa lakini ni baada ya kuwasiliana na wana familia.Chama hakina majukumu ya moja kwa moja ya kuwa update wananchi hadi hapo watakapopata taarifa hizo.
Na kama ndugu wanaongea na vyombo vya habari,basi ni wazi kuwa chama nacho kinapata taarifa kama wengine wanavyopata taarifa.
Chama kinaweza kuwa na taarifa za ugonjwa wake,naamini ni lazima kiwe na taarifa hizo kwasababu Zitto ni kiongozi ndani ya chama hicho.