Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,928
Je, umeshashuhudia maiti ikitolewa kwenye kitanda cha hospital na kupelekwa mochwari?
Je, umeshashuhudia maiti akisafirishwa?
Je, umeshashuhudia maiti akitolewa eneo la ajali ama akipelekwa kuzikwa?
Na je umeshashuhudia ubebaji wa majeruhi ama mgonjwa toka eneo la ajali ama hapo anapogonjeka? Au hospital akihamishwa chumba au kitanda!?
Ubebaji wa maiti ni wa kutanguliza kichwa mbele! Tafsiri yake ni kwamba huyu haamki tena... Yaani hatanyanyuka asimame na miguu yake tena. Huyo hiyo ndio hitimisho la safari yake hapa duniani kuelekea kwenye mwendelezo wa maisha mengine nje ya uhai wa kimwili. Kumbeba kinyume kwa kumtanguliza miguu mbele ni kumzuia mchakato wake kuelekea kuzimu. Hapo ni kuleta ukinzani wa nguvu mbili kiroho la lolote linaweza kutokea!
Ubebaji wa majeruhi ni miguu mbele kichwa nyuma! Tafsiri yake kiroho ni kwamba huyu bado anapumua na ana nafasi ya kusimama tena atakapojaaliwa kupona! Kumtanguliza kichwa mbele majeruhi ni kumchulia kifo na lolote linaweza kutokea hata kama majeraha yake hayakuwa makubwa! Hapa kwa wabebaji hakuna shida ila kama ndugu wakawaona na wanafahamu hili, inaweza kuwaletea shida wabebaji
Kama maisha yasivyo na rivasi kuanzia kuzaliwa mpaka kifo ndio hivyo hivyo kifo kisivyo na rivasi kwenye mwili uliokwisha kutengana na roho. Kwenda tofauti na huo mtiririko wa kiasili ni sawa na kwenda kinyume na roho, ukiilazimisha irudi ambako haparudiki. Na roho huwa haipangiwi hivyo itakachoweza kufanya ni kutoa adhabu
Kuna baadhi ya vifo vya majeruhi ni kutokana na matendo ya kwenda kinyume na asili ya kiroho... Kuna vituko na matukio kwenye misiba pia ni kutokana na, kukiuka ama kwenda kinyume na kanuni za mfu na roho iliyoachana na mwili.
Si kila kitu ni laana
Si kila kitu ni maagano
Si kila kitu ni ushirikina
Vingine ni makosa ya kawaida kwa kujua ama kwa kutojua