ZILIPENDWA: Wanamuziki, nyimbo na mitindo yao

Hivi wakuu samahani,

Hivi wimbo wa harusi original kaimba nani?,ukiacha aliourudia Mr Paul.

Kama kuna mtu anao auweke hapa au ani PM nimpe no anitumie whatsapp.ntashukuru.
 
Hivi wakuu samahani,

Hivi wimbo wa harusi original kaimba nani?,ukiacha aliourudia Mr Paul.

Kama kuna mtu anao auweke hapa au ani PM nimpe no anitumie whatsapp.ntashukuru.
Uliimbwa na Afro 70 Band ya akina Patrick Balisidya...
 
Katika jitihada za kuhifadhi nyimbo na bendi zetu za zamani, nimenzisha mtandao ambao ninakusanya nyimbo hizo na kuzipanga kulingana na albam. Tembelea www.zilipendwa.com ili utoe mawazo yako na kusikiliza baadhi ya nyimbo hizo.
 
wadau natafuta sana wimbo wa kifo cha penzi. wanasema bora ugongwe na train la mizigo.. kifo cha penzi ni kifo kibaya...sikumbuki ameimba nani ila baadhi ya mashairi yake ni hivyo.
 
pia kuna wimbo unasema "wanyaa wabaya mana yake. ni wanadamu wenye choyo...ohhhh huu pia sijajua ameimba nani ila nilikuwa nikiusikia sana ukipigwa live band pale ORION HOTEL au TABORA HOTEL
 
pia kuna wimbo unasema "wanyaa wabaya mana yake. ni wanadamu wenye choyo...ohhhh huu pia sijajua ameimba nani ila nilikuwa nikiusikia sana ukipigwa live band pale ORION HOTEL au TABORA HOTEL

Huo wimbo unaitwa Mganga No 2, umepigwa na Jamhuri Jazz Band toka Tanga.ni kiaa cha ukweli kilichomtokea muimbaji wa Jamhuri baada ya kupanda stejini na sauti kukauka hivyo basi akashindwa kuimba.Ukiskiliza huo wimbo utaskia mganga anamtibu huyo mgonjwa.
 
Wengine tulikuwa hta kuzaliwa bado, ngoja tupite tuu... kimya kimya maana hata sielewi chochot yani
 
Balantanda na wengine nashauri tuweke utaratibu wa kuanzisha club yetu ambayo hiyo tutaweza kushare nimbo mbali mbali zilizopendwa na pia kutembelea kumbi na band ambazo zinapiga zilipendwa kila inapowezekana. Ni namna ya kuunda urafiki na ukaribu pia kwa kuwa na common interest.

Mimi najitolea kushare nyimbo ambazo watu watapenda kupata nyimbo kadhaa ambazo ninazo kwnye library yangu . zilipendwa za kiswahili,lingala na english.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani wengi bado mnaikumbuka MK Group (Wana wa Maghorofani)! Natafuta jina la albam ambazo zilikuwa na nyimbo kama vile Jua la Asubuhi, Kibela, Nishike Mkono n.k., listi ya albam na nyimbo zake itasaidia.
 
Hizi nyimbo enzi hizo mi nadhani raha yake ilikuwa unasikilizia huku unakunywa ulanzi au mbege(pombe za kienyeji)but siyo pombe za sasa hivi.....halafu hivi zile katitu za kenya bado zinaendelea?

Lakini jiulize kwanini bar hawapigi nyimbo za kisasa iula wanapiga za zamani!?
 
Mwenye idea ya break dance leo jumamosi wakiwemo ma-dj mashuhuri wa zamani inafanyika wapi naombeni msaada jamani. Niliona tangazo jumatatu lakini sikumbuki ni wapi
 
Back
Top Bottom