Zile kazi za ifakara health instittute vip jamani

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,985
2,770
IHI walitoa nafasi za ajira 40 kwa Field workers na 30 kwa Interviewers mwezi wa TANO. Vipi wanajamii nafasi hizo zimeshajazwa? mimi na mdogo wangu tuliomba hadi leo tunasubiri kuitwa kwenye usaili hatujapata jibu. pse kama kuna mwenye fununu ya mwisho wake anieleze nitafute kwingine.
 
sina uhakika, ila habari za mitaani ni kuwa Ifakara Research Center wanapendelea dini ya uislamu katika kupata kazi. nasema tena sina uhakika ila habatri hizo mitaani utazisikia!!
 
Salim Abdula ni hatari sana mpaka alishawai kuhojiwa na USA na pia pale Ihi Bagamoyo new site kajenga mpaka msikiti ndani ya ofisi za IHI
 
Na mimi niseme kitu ambacho nina uhakika nacho; mwaka jana miezi ya jioni jioni mwa mwaka 2011 niliskia kwamba kungekua na kazi hapo Ifakara ila masharti yake ni lazima nitoe kiasi kwa ajili ya kuwa short-listed then kama nitapita itabidi salary ya kila mwezi niwe nina imega kidogo ili kuwapa hao waheshimiwa, hata hivyo baaada ya kuona sina uwezo sijui hata iliishia wapi, mwaka 2008 walitoa kazi tena tukaenda kwenye interview niliwahi sana nikasubiri wee, wakaitwa wengine, nakumbuka vyema sana mmoja alikua binti kutoka Moro na akawa anasema alipigiwa simu na "Dr" kwamaba aje kwa ajili ya hio position huku akidai kwamba ingawa yeye hakua anaipenda hio kazi saana ila alikuja kwa ajili ya kumridhisha "Dokta" ili in the future apate kazi nyingine, huwezi amini nilikaa pale nje hadi saa saba na kidogo hivi, hadi watu waliotoka Moro tena (watu wao) wakafika na wakaingia wakafanya interview ndipo ikabidi tuingie sie akina kabwela kuuliza kunani mbona wenzetu wote wameshaitwa na sie bado? tukaambiwa tutoke nje tusubiri baada ya hapo tukaiywa duh niliulizwa maswali ya kijinga sana yaani kabisa unajua hawa wanafanya mchezo wa kuigiza....since then, hawa jamaa naowaona hamnazo kabisa maana kla mtu akianzisha NGO ikiendeshwa kwa misingi ya kujuana kiasi hicho sidhani kama tutafika. Ni ushuhuda wangu na sio hearsays.
 
Dah pole sana mdau wangu kwa yaliyokukuta!ni vema umetuelimisha na sie tusiojua kitu kinachoendelea!
 
Sijui kama kuna ukweli maana nilishawahi kuongea na admin mmoja tulikutana kwa bahati tu tukabadilishana na email kweli akawa ananipa update bila hata ya kumkumbusha. Then akaacha kazi, nikaongea na bwana mmoja yuko HR baada ya kuambiwa kuna ajira. Jamaa akaniambia lete cv leo zaidi ya 6 month kumbe watu walishaanza kazi? Basi noma. Ila hao watu wawili wana dini tofauti. Vigumu ku justify.Anyway bado najipa moyo labda leo jioni watanipigia.
 
ifakara ni taasisi inayoheshimika sana ndani na nje lakini kama wameanza hayo mambo ya NIMR nawapa miaka 2 tu watakuwa kama maduka ya RTC, inasikitisha sana
 
nna rafiki yangu ni mkristo amepata kazi hapo ihi kama miezi3 hivi iliyopita. so kwenye suala la udini sidhani kama lipo kiivyo. ila tanzania ya leo kazi bila kujuana hupati.
 
ifakara ni taasisi inayoheshimika sana ndani na nje lakini kama wameanza hayo mambo ya NIMR nawapa miaka 2 tu watakuwa kama maduka ya RTC, inasikitisha sana
Hapo NIMR Kuna nini?maana nimefanya interview na panel ya watu 10 na nikaambiwa majibu yatanifikia baada ya mwezi ninavyoandika ni miezi miwili sijasikia lolote.Na ktk panel mkurugenzi na mkurugenzi msaidizi wa IHI Walikuwepo pamoja DG wa NIMR.
 
Sijui kama kuna ukweli maana nilishawahi kuongea na admin mmoja tulikutana kwa bahati tu tukabadilishana na email kweli akawa ananipa update bila hata ya kumkumbusha. Then akaacha kazi, nikaongea na bwana mmoja yuko HR baada ya kuambiwa kuna ajira. Jamaa akaniambia lete cv leo zaidi ya 6 month kumbe watu walishaanza kazi? Basi noma. Ila hao watu wawili wana dini tofauti. Vigumu ku justify.Anyway bado najipa moyo labda leo jioni watanipigia.
Mdau ucsahau kutujuza kama jioni ya jana walikupigia simu,tupate kujua kama kunachochote kinaendelea!
 
mdau zile kazi ukiona zinatangazwa ujue wenyewe wako na mabegi yao kuelekea ofisini na wewe ukifanya interview mwenzio anawekewa ac kwenye ofisi hioyo hiyo
 
Guys muwe serious katika yale mnayoyaongelea, Nipo IHI mwaka wa 3 sasa na ni mkatoliki wa kikristu na kazi nilipata via application na before sikumjua mtu yoyote ila nlipiga interview mara 2 before kusain mkataba wa kazi so huyo anayesema kuna Udini ni zaidi ya uchonganishi, ndio msikiti umejengwa bagamoyo but sio eneo la IHI na huo msikiti umejengwa na waislam wafanyao kazi hospital ya bmoyo na IHI, hata zilipo ofisi za IHI kwa sasa zimekodishwa toka hospital ya Bagamoyo, ofisi mpya za IHI zinajengwa Kingani Bagamoyo. Mimi nipo entomology dept hakuna muislam hata mmoja kwa ofis za dar na ifakara-moro hawazidi hata wawili na dept inazaidi ya watu 100..so nashindwa elewa hapo udini umeingiaje? Wadau tusipende kusukumwa na maneno ya mtu mmoja ambaye hajafanya research ya kile anachokiandika ila amesukumwa na ugumu wa upatikanaji wa ajira Tanzania (janga la Taifa kwa sasa)

Hata hao mnaosema wameshaajiriwa bado coz wanaohitajika kwa kazi ni 70 lkn application ni zaidi ya 3500 kuna watu mpk wa Masterz wameaaply hizo post while wanatafutwa ni Form 4 na 6 only kutokana na nature ya kazi yenyewe na policy ya uajiri ndani ya IHI huwezi kumuajiri mtu ambaye ana vigezo vimezidi vile ambavyo vilivyoainishwa coz hata malipo yatakulimit. Most of application nimeziona nyingi ni ngumu kuamini kuwa mtu wa Bachelor anashindwa jielezea atakavyoweza handle responsibilities zilizoaainishwa, let say kila barua ukisoma unakuta mtu kaandika I am enthusiasm with the post because I am hardworker, honest, team player, well organised etc...but hujaelezea utaweza vipi kuhendo responsibilities zilizoelezwa

Another thing, Director haajiri hata siku moja ndani ya IHI pia hata kwenye panel ya kuinterview huwa hayumo kutokana na majukumu yaliyo kwake..anayetangaza kazi ni Principal Investigator via HR na HR anafanya procedure za ajira then anapeleka majina kwa PI ili afanye final decision. If you need more info chek na mie personal humuhumu Jamii Forum ntakupa strategies za kuwin ajira ndani ya IHI
 
Na mimi niseme kitu ambacho nina uhakika nacho; mwaka jana miezi ya jioni jioni mwa mwaka 2011 niliskia kwamba kungekua na kazi hapo Ifakara ila masharti yake ni lazima nitoe kiasi kwa ajili ya kuwa short-listed then kama nitapita itabidi salary ya kila mwezi niwe nina imega kidogo ili kuwapa hao waheshimiwa, hata hivyo baaada ya kuona sina uwezo sijui hata iliishia wapi, mwaka 2008 walitoa kazi tena tukaenda kwenye interview niliwahi sana nikasubiri wee, wakaitwa wengine, nakumbuka vyema sana mmoja alikua binti kutoka Moro na akawa anasema alipigiwa simu na "Dr" kwamaba aje kwa ajili ya hio position huku akidai kwamba ingawa yeye hakua anaipenda hio kazi saana ila alikuja kwa ajili ya kumridhisha "Dokta" ili in the future apate kazi nyingine, huwezi amini nilikaa pale nje hadi saa saba na kidogo hivi, hadi watu waliotoka Moro tena (watu wao) wakafika na wakaingia wakafanya interview ndipo ikabidi tuingie sie akina kabwela kuuliza kunani mbona wenzetu wote wameshaitwa na sie bado? tukaambiwa tutoke nje tusubiri baada ya hapo tukaiywa duh niliulizwa maswali ya kijinga sana yaani kabisa unajua hawa wanafanya mchezo wa kuigiza....since then, hawa jamaa naowaona hamnazo kabisa maana kla mtu akianzisha NGO ikiendeshwa kwa misingi ya kujuana kiasi hicho sidhani kama tutafika. Ni ushuhuda wangu na sio hearsays.

Tafuteni wafadhili wao, halafu waambieni malalamiko yenu muone watakavyowawashia moto ihi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom