Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Mkuu ili kufungiwa umeme kuna vifaa vinahitajika hivyo kukiwa na upungufu wa hata material ya aina moja huwezi kufungiwa mpaka yakamilike hivyo Tanesco nao wanapenda kupata wateja wapya ili shirika lipate mapato na sio kwamba wanachelewesha makusudi
Chalii, wanayoongea au kuyaandika hapa usidhani wanayatunga. Hizi adha na usumbufu upo tena ni mkubwa sana. Mimi mwenyewe kwangu inahitajika nguzo moja tu lakini ni mwezi wa tatu sasa hamna kitu. Hapo hapo ukiwaambia Tanesco wanakujibu kuwa hawana nguzo na walizokuwa nazo wanawafungia wateja wa mwezi 10/2016. Ina maana hao wa mwezi wa kumi hadi sasa wana miezi zaidi ya saba. Material gani yanakosekana kwa miezi saba kama kweli mnafanya kazi yenu na mnawajibika? Kwahiyo mteja wa mwezi huu atapata umeme mwezi wa kwanza mwakani (2018). Sasa kuna haja gani ya kudanganya watu?
 
Bei inategemea na umbali hivyo ndank ya mita 30 ni 321000 mijini na 177000 vijijini.ikizidi hapo inategemea na umbali uliopo
Acheni UPUUZI nyinyi, watu wanakaa hadi miezi sita kisa nguzo. Kwanini mlichukua pesa zao kama hamkuwa na vifaa? Wezi wakubwa nyie.
 
TANESCO TAZARA wanakera sana. Niliomba kubadilishiwa tariff kutoka tariff 1kwenda tariff 4 wakaniambia watakuja kunitembelea wajue vitu nilivyonavyo. Baada ya kuja kwangu wakanitaka nifike ofisini. Na baada ya kufika ofisini jibu nililopewa na mhasibu ni kuwa tatumia umeme mwingi kwa mwezi hadi kufikia unit 139. Lakini nilipomwambia hata hamsini hazifiki kwa mwezi, akanijibu inanibidi niendelee kutumia hadi mwezi wa sita. Cha kushangaza ambacho sijakipenda wamenibambika nanunua tariff 1 kwa sh 350! Inaumiza sana. Mpaka sasa kwa miezi 3 nimetumia jumla ya units 139.99 mpaka muda huu naandika. Sasa sababu ya kunipandishia bei kutoka bei ya sh 292 hadi 350 wakati mita haidaiwi na wamenikatalia kubadilishiwa tariff ni nini?
 
Ukanda wa Temeke maeneo ya TUANGOMA(TOANGOMA) kuna UMEME na baadhi ya nyumba ambazo kimpaka ziko MKURANGA (mkokozi village) zimepewa umeme kupitia Temeke lakini eneo kubwa la kitongoji cha MKOKOZI ambacho kimepakana na Temeke hakuna Umeme
Swali kwann eneo hili la MKOKOZI lisipewe Huduma toka TEMEKE
 
Mm nimelipia nguzo 3 mwezi was September leo mwezi wa June miezi 10 karibia milioni 2 nilizolipa kwa miezi 10 ningezifanyia Biashara zingenisaidia
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO


Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.


5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
Shukran
 
Kama nyumba ipo mbali na nguzo za Umeme, mtu anaambiwa alipie gharama kubwa ili kuongeza nguzo ipi aweze kupata Umeme, ila nguzo bado zinabaki Mali yenu, na mtu mwingine akija kuunganisha katika nguzo niliyolipia Mimi wala sirudishiwi hata nusu ya gharama, je hii ni Sawa,
 
Kwanza niwapongeze kwa kuja humu, nadhani ninsehemu sahihi sana ya kujipima na kujifanyia self evaluation.
Kimsingi Tanesco Mnasumbua sana mwezi sasa nipo gizani hamjafika kufanya savei. Najiandaaa kununua solar tu niachane na nyie.
 
Kama nyumba ipo mbali na nguzo za Umeme, mtu anaambiwa alipie gharama kubwa ili kuongeza nguzo ipi aweze kupata Umeme, ila nguzo bado zinabaki Mali yenu, na mtu mwingine akija kuunganisha katika nguzo niliyolipia Mimi wala sirudishiwi hata nusu ya gharama, je hii ni Sawa,


Hii si sawa aisee
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO


Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

Hivi karibuni kutakuwa na Maombi ya kufuata ILI KUONDOLEWA LINE YA UMEME YA TANESCO!

[HASHTAG]#WatchThisSpace[/HASHTAG]
 
Sasa mimi UMEME nataka sasa wayaringi imefanywa Na MTU ambaye asiye sajiliwa itakuwaje? Naomba msaada wenu.
 
Nina malalamiko yangu kuhusu shirika langu ili la tanesco, iweje nipewe gharama za kuhunganishiwa umeme then naenda kuripa after kulipa naambiwa nisubiri kupigiwa simu ya kuunganishiwa umeme then nakaa baada ya masiku kenda natumiwa sms kuwa niendelee kuwa mvumilivu naendelea kuwa mvumilivu baada ya siku kwnda tena natumiwa sms kuwa niendelee kuwa mvumilivu maana kuna uwaba wa vifaa, hapo ndo nimestaajabu uwaba wa vifaa wakati mimk nimeshalipa pesa yenu mkanunulie ivyo vifaa, daaah naendelea kuishi giza tu mnakera sana kwakweli,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tatizo la nyaya za umeme,eneo la Mbagala Nzasa kwa Mwarabu.
Karibu na bar iitwayo KAHOMBA au karibu na Nursery School iitwayo MONTESSORI nyaya hizi ziko chinichini saana kiasi cha kuhatarisha usalama.
 
Back
Top Bottom