Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO

Hawa jamaa ni wahuni kichizi hata mimi sasa ni zaidi ya miezi miwili tangu nilipie mahala pa Nguzo moja hadi sasa kimya..... Kila nikiwafuata wanasema nguzo hakuna.....
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz

Mimi nimeomba kufungiwa umeme Tangu last month June. Nimekamilisha taratibu zote. Tanesco WAMEFIKA nyumbani/site kufanya survey. Wameniambia natakiwa kulipa certain amount (kwa sababu nataka three phase). Nimewambiwa hela ipo wanipe utaratibu wa kulipia. Hapo ndo shida imeanza. Naambiwa hela nilipe TANESCO (najenga mkoani). Nikauliza mbona naambiwa hela tunalipia benki? hawana majibu. Kibaya zaidi naambiwa nilipe Lakini risiti hakuna (eti watanipa reference number). Nikastuka (maana sijawahi ona pesa ya serikali inalipwa bila risiti). Tangia hapo napewa visingizio, mara vifaa vimefuatwa mkoani, mara tunafanya stock taking na sababu lukuki. Kiukweli nimekuwa disappointed. Nasubiri nipate opportunity niende makao makuu labda nitasaidiwa.

Lakini kutokana na hii experience niliyoipata, Nimepata jibu kwanini Mashirika ya umma yanakufa kila mara/au yanatengeneza hasara. Yaani kuna umangi meza mkubwa sana TANESCO.

I hope wahusika wanapita humu wanaziona hizi kero.
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
SAfi sana, ubarikiwe!
 
Tanesco mi nawashauri hili

Tengezeni uwezekano wa mtu kuangalia salio la units za umeme kwenye akaunti yake kupitia simu ya kiganjani, yaani iwe kama tunavyoangali salio la king'amuzi kupitia simu baada ya kuweka namba za king'amuzi.

Sasa nanyie tengenezeni huo mpango yaani iwepo system mtu akibofya anaingiza namba za mita kisha angaalia salio la units.

Itakua bonge la huduma maana usiwepo home ili mradi unaijua namba yako ya meter unacheki tu, hakuna haja ya kumpigia sim beki tatu akachungulie kwenye meter, hakuna haja ya kuangalia kadi iko wapi, itakua hakuna haja ya kutumia ile user interface kuangalia salio la units.

Hayo ni mawazo yangu kama mtaona inafaa ni vema mkafanya huo mchakato.
 
TANESCO hii system mliyoanzisha baadhi ya sehemu ya kukata umeme kwa baadhi ya nyumba tu kwenye eneo hilo hilo huku nyumba za jirani zina umeme si nzuri. Na juu ya hapo watu wenu wakipigiwa simu ni kama vile wanalizimishwa kutoa msaada.
Swala hili limetokea jana Tabata Segerea umeme umekatwa kwa baadhi ya nyumba tu cha ajabu nyumba zilizotenganishwa na uzio tu zina umeme. Inaeleweka kuwa inaweza kuwa ni tatizo la kiufundi lakini cha ajabu leo tena siku nzima umeme hakuna na umerudishwa jioni hii kuja kukatwa tena kwa baadhi ya nyumba tu.
Kupiga namba yenu ya dharula mpokeaji simu ni kama vile analazimishwa kutoa huduma maana anapiga stori kwenye background huku anasema subiri. Huu si uungwana. Haileti maana kuweka namba ya dharula lakini mtu akiwa na dharula haishughulikiwa.
Namba ya dharula ya Tabata ni ‭0715 768 589‬. Na baada ya kulazimisha huyo aliyepokea simu katoa reference namba ya 2366.
Kuweni na weledi katika huduma ya wateja maana nina yakini bila ya sisi sidhani kama kuna Tanesco.

Disgruntled Client
Tabata Segerea.
 
Tanesco mi nawashauri hili

Tengezeni uwezekano wa mtu kuangalia salio la units za umeme kwenye akaunti yake kupitia simu ya kiganjani, yaani iwe kama tunavyoangali salio la king'amuzi kupitia simu baada ya kuweka namba za king'amuzi.

Sasa nanyie tengenezeni huo mpango yaani iwepo system mtu akibofya anaingiza namba za mita kisha angaalia salio la units.

Itakua bonge la huduma maana usiwepo home ili mradi unaijua namba yako ya meter unacheki tu, hakuna haja ya kumpigia sim beki tatu akachungulie kwenye meter, hakuna haja ya kuangalia kadi iko wapi, itakua hakuna haja ya kutumia ile user interface kuangalia salio la units.

Hayo ni mawazo yangu kama mtaona inafaa ni vema mkafanya huo mchakato.
Mkuu hili wazo lako ni UTAJIRI kwakuwa umewapa wazo hili bure naamin kama wana vichwa watachangamkia fursa.
 
Naomba nitoe shukrani binafsi kwa TANESCO kwa jinsi mlivyonisaidia kuweka umeme kwenye makazi yangu Bunju. Nimefata utaratibu bila kuhonga au kupita njia za panya na kufungiwa umeme haraka kuliko nilivyotegemea. Kiukweli kuna mabadiliko makubwa mno kiutendaji.

Nilikuwa nishajipanga kishari nikijua mtazingua tu. This is my personal experience.
 
Baada ya kupoteza matumaini ya kupata umeme wa REA japo tulisha haidiwa muda mrefu sasa vijana tunataka kuunganisha nguvu ili tuvute kwa gharama zetu, samahani naomba kusaidiwa ndani ya kilometa moja na nusu tutahitaji nguzo ngapi, na kila nguzo itatugharimu shilingi ngapi maeneo ya vijijini.?
 
achaneni na tanesco fungeni umeme wa solar ambao uko intergrated na wind turbine, mchana unapokea umeme jua na umeme upepo usiku unapokea umeme upepo. hamna sijui luku imeisha sijui umeme umekatika? unafunga umeme siku hiyo hiyo unatumia siku hiyo hiyo.
 
Jana nimemtuma kijana wangu kwenda kupata namba ya kumbukumbu TANESCO Mkuranga akaelezwa kuwa network inasumbua aache no za simu mambo yakiwa tayari atajulishwa.

Naye akachukua za TANESCO Mkuranga, kila akiwapigia jibu, bado network haijarudi, sisi tupo kwenye mradi mpya, huku tunatangaziwa kuwa mwisho ijumaa.

Kila kitu kifanywe kwa ueledi, anayefata Huduma TANESCO kaacha kutoa Huduma sehemu nyingine ili tuumuunge mkono Mh Rais tupunguze njoo kesho ili tusonge Mbele.
 
Gharama za meter separation ( kuwekewa mita ya peke yangu kwenye fremu ili nisichangie umeme na mwenye nyumba ? Na vitu gani vingine vinavyohitajika
 
HATUA YA KWANZA

MAOMBI YA MWANZO

Je mteja anaweza kuchukua fomu ofisi yeyote ya tanesco?

Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

JE KUNA GHARAMA ZOZOTE KATIKA UCHUKUAJI WA FOMU?

Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

1. Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

2. Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa.

3. Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, kitambulisho cha kazi (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

4. Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa ruhusa ya mwenyenyumba kama atakuwa ni mpangaji. Lazima mteja aje na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni.

5. Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya serikali husika.

6. Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika.

7. Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo

1. Kuisoma fomu kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja mpaka kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

2. Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za tanesco. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

3. Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

4. Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:

MAELEZO

Muda wa makadirio

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 7 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100)

Ndani ya siku 10 za kazi

Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)

Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya tanesco ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (reference number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms) (kwa sasa ni bank ya nmb tu), wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika na tanesco. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena tanesco bali tanesco watakuwa na taarifa zake zote na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

MAELEZO

Muda wa kufungiwa

Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu)

Ndani ya siku 30 za kazi

Ujenzi wa njia ya nyongeza itahitajika

(mita 30- 100)

Ndani ya siku 60 za kazi

KAMA MFUMO MPYA WA USAMBAZAJI UNAHITAJIKA KUJEGWA AU MFUMO WA UMEME MKUBWA UNAHITAJIKA KUONGEZWA KWA AJILI YA KIWANDA AU BIASHARA KUBWA (KAMA HAKUNA MFUMO WA KUMUUNGANISHIA MWOMBAJI) (ZAIDI YA MITA 100)

Ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA NASI

Kituo cha huduma kwa wateja: - 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
Wengine tulichukua fomu nakuzirudisha, ishu kuja kupima savei, nimefuatilia mpaka basis. Naambiwa nilipie usafili Niko Tarime nyamongo
 
TANESCO naomba mjibu maswali ya wadau ili kuthibitisha kuwa inawathamini wateta.
Me swali langu ni kwamba kama gharama za kufungiwa umeme zinategemeana/tofautiana kutokana na umbali wa nguzo au Transforma kwa nimi huku Kigoma bei ni sawa yaani haijalishi nguzo ipo jirani na nyumba yako au mbali.
 
tanesco office ya kisarawe inayo hudumia ukanda wa baadhi ya maeneo ya ilala kama chanika ndiyo office bogus kuliko tanesco offices zote Tanzania. Pale hata kupaita genge la wahuni unakuwa umewapendelea. Ujinga mtupu, wanachukua hela za watu bure kabisa, wakisha kusahinisha makaratasi ndiyo basi. Unafuatilia mpaka unakata tamaa. Yule maneja wa pale nazani ndiye meneja dhaifu kuliko ma-meneja wote ulimwenguni.
 
Back
Top Bottom