Zijue sababu za Wanawake wengi kupenda wanaume wakubwa kiumri kuliko wao

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,488
21,960
Kwa kawaida, wanaume wengi wanapenda kuoa mabinti wenye umri mdogo. Ndio maana wanawake wengi wenye umri mkubwa wanapigania ndoa zao kuliko wanaume. Na wanawake wengi wasio na waume ambao hawakuzaliwa jana hupata wasiwasi sana wanapozeeka bila kupata mwanaume wa kumuoa.

Ukweli, wanawake wengi wanapendelea wanaume wakubwa kiumri kuliko wao. Kibiolojia, wanawake hukomaa mapema. Na inaaminika sana kwamba wanawake kwa ujumla wana busara zaidi kuliko wanaume wa umri wao. Mawazo haya ni hali halisi ya watu wengi.

Binafsi naamini, umri sio suala halisi katika mahusiano. Wanawake hutafuta wanaume ambao wanaweza kuwaongoza vyema bila kujali umri wao. Naamini hivyo kwa sababu nimeshuhudia wanawake wengi ambao wameolewa kwa furaha na wanaume wenye umri mdogo kuliko wao na wanaishi vyema sana.

Sasa Wanaume wengi wenye umri mkubwa wana sifa fulani hivi ambazo huwafanya wapendwe sana, sifa hizo ni...

1. Wanajua wanawake wanataka nini, ndani na nje ya chumba cha kulala.

2. Hawaogopi ndoa.

3. Hawakwepi majukumu yao katika ndoa.

Nk nk..

Kwa hiyo wanawake wengi hutamani sana kuolewa na 'vibabu'.

Vibabu tujuane hapa.
 
IMG-20230521-WA0010.jpg
 
Back
Top Bottom