Ziara ya Wang Yi barani Afrika italeta uhakika katika dunia inayojaa sintofahamu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG41N1418258266.jpg


Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Misri, Tunisia, Togo na Cote d'Ivoire kuanzia tarehe 13 hadi 18 mwezi huu. Huu ni mwaka wa 34 mfululizo kwa waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara barani Afrika kila mwanzoni mwa mwaka mpya.

Mwaka 2023. Afrika ilishuhudia fursa pamoja na changamoto, na kwamba licha ya hadhi ya kimataifa kuinuka sana, pia imekumbana na taabu kama migogoro, mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa mzigo wa madeni.

Kutokana na hali hiyo, ziara hiyo ya Waziri Wang Yi barani Afrika itathibitisha kwamba wakati dunia inaingia katika kipindi cha misukosuko na mabadiliko, China inathamini urafiki wa jadi kati yake na Afrika na azma yake ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika haibadiliki. "Uhakika" huu ni muhimu sana kwa uhusiano kati ya China na Afrika na jamii nzima ya kimataifa.

Mwaka huu ni mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa "Mpango wa utekelezaji wa Dakar wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika", ikiwa ni pamoja na "Miradi Tisa" inayotekelezwa kwa pamoja na pande zote mbili.

Kwa mujibu wa mpango, Mkutano mwengine wa FOCAC utafanyika nchini China mwaka huu. Kwa sasa, dunia tunayoishi inakabiliwa na hali mbaya ambapo changamoto kuu tatu zinaweza kuja kwa wakati mmoja, na athari zao kwa Afrika zinaweza kuwa kubwa.

Kwa hiyo, pamoja na kuangazia uhusiano wa pande mbili, ziara hiyo ya Wang Yi pia itaangalia jinsi ya kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hizo na kupanga malengo ya maendeleo ya China na Afrika siku zijazo.

Kwanza, athari za mabadiliko ya hali ya hewa zinaongezeka kwa kasi. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikikabiliwa na hali mbaya ya hewa, na mabadiliko ya hali ya hewa yanazidi kuwa msukosuko halisi, unaotishia moja kwa moja maendeleo ya kiuchumi, usalama na utulivu wa Afrika.

Mara kwa mara nchi za Afrika zimetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia zaidi matakwa na matatizo ya Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuiunga mkono Afrika katika kutafuta njia ya maendeleo endelevu ya kijani.

Hivi sasa, China inashika nafasi ya kwanza duniani katika sekta ya nishati mbadala. Ushirikiano kati ya China na Afrika itasaidia kuinua uwezo wa nchi za Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo ya uchumi wa kijani.

Pili, athari kubwa ya maendeleo ya haraka ya teknolojia ya akili bandia. Hivi sasa, teknolojia ya akili bandia inaunda upya mitindo ya maisha ya binadamu na mbinu za uzalishaji, na hata itaunda upya muundo wa nguvu wa kimataifa na sura ya mahusiano ya kimataifa.

Hata hivyo, bado kuna pengo kubwa la kidijitali kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Mwaka 2022, kiwango cha matumizi ya mitandao ya internet barani Afrika kilikuwa 50% tu, chini ya wastani wa dunia wa 66%.

Wakati teknolojia ya kidijitali na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapohusiana kwa karibu, pengo la kidijitali litazidisha pengo kati ya matajiri na maskini katika Afrika na mabara mengine.

Kwa hiyo, China na Afrika zinahitaji kuimarisha zaidi ushirikiano katika mambo ya kidijitali, badala ya kuchukulia maendeleo ya kidijitali kama fursa nzuri kama zinavyofanya baadhi ya nchi zilizoendelea, kuzuia nchi nyingine kunufaika na teknolojia ya kisasa.

Tatu, sintofahamu katika mikakati ya kimataifa zinaongezeka. Kutokana na kuongezeka kwa pamoja kwa ushawishi wa nchi zinazoendelea, nia ya Marekani na nchi nyingine kudumisha utawala wa Magharibi imekuwa ikiongezeka, ambayo imesababisha kuvunjika kwa mitindo ya uhusiano wa kimataifa.

Wakati huohuo, 2024 pia inajulikana kama "mwaka wa uchaguzi mkuu." Sio tu nchi zenye nguvu duniani kama Marekani na Russia, lakini pia nchi muhimu zinazoendelea kutoka Afrika kama Misri na Afrika Kusini zitafanya uchaguzi, hii itakuwa na athari kubwa kwa hali ya kimataifa kwa siku zijazo.

Kwa hivyo, China na Afrika zinapaswa kusimama kwenye kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na kuchangia nguvu chanya zaidi katika amani, maendeleo na utulivu wa dunia.

Kama alivyosema Wang Yi wiki hii alipohudhuria ufunguzi wa Kongamano la Hali ya Kimataifa na Diplomasia ya China mwaka 2023, China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja na kusukuma dunia kuelekea katika mustakabali mwema.
 

Attachments

  • VCG111164721339.jpg
    VCG111164721339.jpg
    28.9 KB · Views: 1
Hivi sisi waziri wetu wa masuala ya kigeni yupo na mipango kama hii ya kuipa Tz ushawishi na kukamata fursa?
 
Back
Top Bottom