Ziara ya Dk. Bashiru Nzega

VINCENT KASAMBO

New Member
Oct 27, 2018
3
1
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dk Bashiru Ally ambayo ni Maelekezo ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiendelea na ziara Wilayani Nzega katika Mkoa Tabora Tanzania.

Dk. Bashiru amekagua miradi mbalimbali ya serikali kama Barabara na Madaraja, majengo ya Shule na maendeleo ya wanafunzi kielimu na kuielekeza TARURA ambayo ndiyo mjenzi wa Barabara za Mijini na Vijijini kuhakikisha zile barabara muhimu zinaingizwa kwenye mpango wa kuzijenga na kukamilika ifikapo mwaka 2020 ili kupunguza adha inayojitokeza kwa sasa.

Kwa Wilaya yetu ya Nzega TARURA inaendelea na ujenzi wa barabara za Lami mjini na ujenzi wa barabara vijijini hilo liko wazi serikali ipo kazini na utekelezaji wa Ilani ya CCM unajionyesha dhahiri.

Akiongea na wananchi Shuleni hapo, Katibu Bashiru ameupongeza uongozi mzima wa Wilaya ya Nzega chini ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula na Kabinet yake pamoja na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kusema kwamba, "Nawapongeza sana wananzega kwa kazi hii kubwa, kwa kuwa katika safari ya kujenga taifa, ujenzi wa taifa unahitaji taasisi madhubuti, moja ya taasisi hizo ni shule, bila kuwa na shule hakuna heshima, na bila heshima hakuna taifa, shule ni kitovu cha utaifa wetu na utu wetu."

Ziara ya Katibu Bashiru inaendelea Wilayani Nzega na leo atakuwa katika mradi wa maji ya kutoka Ziwa Victoria Mwanza, ziara hiyo umehudhuriwa pia na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora ukiongozwa na Mwenyekiti CCM Hassan Wakasuvi na Katibu CCM Solomon Kasaba wakiambatana na baadhi ya wabunge mkoani Tabora.

Niungane na mitazamo ya Katibu wetu wa CCM Taifa Dk. Bashiru Ally pamoja na mitazamo ya Rais wetu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Magufuli kwa yote aliyoyasema leo katika hafla iliyofanyika leo Mkoani Mwanza ya uwekezaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Meli mpya na Chelezo ktk Bandari ya Igogo Jijini Mwanza.

Nawapongeza sana kwa mitazamo yao kwa ujenzi wa taifa ili kuendeleza heshima iliyojengwa na viongozi mbalimbali waliopita akiwemo Baba wa taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na vilevile kusahihisha makosa yao kwa maana kila uongozi unayo makosa na mazuri vile vile.

Mimi nitaongezea Nyama au Chumvi na ikiwezekana Sukari ilimradi naongezea kitu ktk hoja, kauli na mitazamo ikiwemo hali ya mazingira tuliyonayo sasa tukizingatia kwamba kesho ni siku ya Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yetu.

Kwa kuanza na aliyoyasema Dk Bashiru kuhusu ujenzi wa Taifa letu pale aliposema ".. ujenzi wa taifa unahitaji taasisi madhubuti", na moja ya taasisi hizo ni shule, nakubaliana kabisa na hilo kwa sababu elimu ndio ufunguo wa maisha ya binadamu, taasisi hii huenda ni muhimu kuliko taasisi nyingine zote kati ya hizo, katika kuhakikisha taifa linakuwa na binadamu wanaojiweza kifikra, kiuchumi, kisiasa, kiutawala na kiutamaduni wao, kitu cha kwanza kabisa ni kuhakikisha mfumo wa elimu unakuwa madhubuti ili kukamilisha dhana nzima ya taasisi madhubuti.

Na ni waalimu pekee kati ya makundi/matabaka ya kijamii wenye kuwakilisha mtazamo wa jamii au taifa husika, hakuna taasisi imara na madhubuti penye mfumo wa elimu wa hovyo hovyo na wenye kubagua wananchi/binadamu kimatabaka, na hakuna elimu bora penye walimu wa hovyo hovyo yaani waliofeli au kununua mitihani kisha kupelekwa kituo cha chuo kama njia ya kujipatia shahada ya ualimu.

Taifa litakalozalishwa hapo ni taifa la wasomi makundi, na wasaliti wa taifa na lenye viongozi mawakala walio tayari kuliweka rehani taifa na watu wake kwa mataifa ya kibepari, na hicho ndicho alichokidhihirisha leo Rais Dk Magufuli pale Mwanza aliposema enzi za uwaziri wa Profesa Mwandosya akimaanisha utawala enzi zile kuwa, watumishi wa Bandari na usafirishaji wa mizigo kwenye Meli walitoa tiketi hewa na kujinufaisha wao wenyewe fedha hizo walizokuwa wakikusanya bandarini hapo, huo ni mfumo mdogo tu.

Ukweli ni kwamba, baada ya nchi za kiafrika kupata uhuru wake, viongozi wa kiafrika na wasomi waliofuatia wengi ni wasaliti, makundi na mawakala wa Mataifa nyonyaji wa kimataifa; wamesaliti watu wao, wamesaliti uhuru wa nchi zao, wamesaliti tamaduni zao, wamekuwa sehemu ya ufundi, ukoloni mamboleo unaodhihirishwa na dhana ya Utandawazi, huu ni ukandamizaji pia wa wananchi waitwao wanyonge na kizazi cha utandawazi ni cha mamluki na cha kishetani.*
*Kizazi cha kwanza cha viongozi wazalendo wa kiafrika hakikuwa cha wajinga kama baadhi ya viongozi wasomi wa kizazi hiki.

Licha ya kuleta uhuru wa nchi zao, viongozi hao walibaini mapema kwamba, kama Afrika itaachwa ijiendee hovyo kwa kila nchi kivyake; nchi zote zingekuwa mateka wapya wa ukoloni mamboleo kabla ya uhuru wake haujapata mizizi.*
Kwa kutambua hilo, waliunda Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) ili kutetea haki, heshima na nafasi ya mwafrika katika jamii ya kimataifa.

Lakini ulikuja kufeli kwani viongozi waliopatikana baada ya hapo wengi walitokana na wakoloni hao hao kwa kuwekeza fedha nyingi zilizotumika kuwashawishi wananchi wa nchi zao.

Na katika kutekeleza jukumu hilo, baadhi ya viongozi, kama Rais wa Ghana, Kwame Nkurumah wakawa waathirika wa mbinu chafu za mabeberu hayo, hata Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ni miongoni mwa walionusurika kwa kutekeleza nadharia ya kwa vitendo huku wakihubiri Umoja wa Afrika kama ambavyo Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru na Rais Dk Magufuli.

Walikuwa viongozi wenye maono makubwa na kama walivyo wenye maono wote, urithi waliotuachia umo kwenye maono zaidi kuliko ktk vitendo, ni wakati na kazi na wajibu wa viongozi wasomi wa sasa kuyaenzi na kuyatafsiri katika vitendo maono hayo, badala ya kuendeleza maono tu bila vitendo.

Hapa kwetu Tanzania tuliunda na kujenga misingi imara na madhubuti kupitia Azimio la Arusha, lakini akina Alihaji na genge lake ndani ya Chama wakalipindua Azimio bora kutokea kwa kutuletea Azimio la Zenji ambalo kimsingi ulikuwa mpango wa wakoloni hao wa kimataifa.

Haya matamko yasiyo na utekelezaji wa kuibadili mifumo mbalimbali kama ya elimu kuwa bora na itakayowafanya kila mtoto wa kitanzania kusoma pamoja kuliko ilivyo sasa watoto wa viongozi na watumishi wa serikali na matajiri kusomesha watoto wao tofauti na shule za serikali tangu shule za msingi, kutengeneza katiba ya nchi kwa kuweka miiko na maadili na kuondosha sheria zinazowawezesha wengine kufanya ufisadi bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria, na bila kuzitafsiri sheria za nchi kutoka kiingereza kwenda ktk lugha yetu ya Kiswahili; Basi hatutakuwa tukimaanisha kujenga taifa la watu huru na wenye usawa, tutakuwa sawa na tunaowakosoa kila siku kwamba wametufikisha hapa tulipo ("PABAYA") na kusifu uongozi wa awamu ya tano ambao nao hautaki kuyabadili yaliyotufikisha hapa "PABAYA".

Kwa maana, ukweli yaliyotufikisha hapa ni hayo niliyoyasema, Mfumo mbovu wa elimu na ubaguzi wa kupata elimu, Sheria kubaki katika lugha isiyo ya wananchi au ya taifa kwa lengo la kuwafanya mitaji wananchi, Katiba inayolinda wevi, mafisadi waliokwenda kuficha fedha Uswi zi kwa kutokuwa na miiko na maadili, sheria zinazoruhusu kuingia hatiani.

Kutofanya hivyo, basi, si rahisi kubeza tawala zilizotangulia, wala mafisadi ya sasa yanayoonekana katika ziara mbalimbali za Rais Dk Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, nasema si rahisi kubeza pasipo ujasiri wa kifisadi na usaliti uliokubuhu, dhana na nyenzo za kisukuma mbele maono hayo katika kulinda na kutetea heshima ya Mtanzania ambayo ilijengwa ktk Nafsi ya Mwafrika na Ujamaa wa Mwalimu Nyerere.

Ni kichekesho, kama alivyosema Mrisho Gambo ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kupeleka wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi waliopata alama 70 chini ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 28 ambayo ni alama D, hata pale imeonekana kuongezeka alama 100 chini ya 250 ambayo sawa na asilimia 40 ambayo ni sawa tu na D kwa sababu C ya kipindi cha mfumo wa elimu bora ilianzia asilimia 41, na kipindi hicho watoto wa viongozi na watumishi wa serikali na matajiri walikutana na watoto wa masikini ktk shule za serikali.

Hivi leo tunazungumzia elimu bure bila usawa uliokuwepo zamani ni kuhadaa wananchi na kwa kuwa wajinga ni wengi hawawezi kuliona hilo wala kupambana na ubaguzi huo, ujinga unatengeneza hofu, na hofu huzika ndoto za watu wengi sana.

Kwenye hili bado nitaendelea kusema, na kusema kuna maana nyingi sana, hatuwezi kuruhusu upotoshaji kuwa sehemu ya uongozi kisha tuuite ni bora, kwa bila kuboresha haya.

JK. NYERERE: "TUPUNGUZE TOFAUTI KATI YA MANENO NA VITENDO"

Itaendelea kesho sehemu ya nne na kuendelea na mwisho tarehe 10 baada ya maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwiyeya Singu Ntabanwa. 0784977072
 
Back
Top Bottom