Zembwela: Elimu ya Sheria si makalio eti kila mtu awe nayo

Asante CCM

JF-Expert Member
Jun 22, 2023
346
1,301
Akionyesha kuguswa na kukerwa na kuvunjiwa heshima na wachangiaji wake kwenye picha aliyoiweka (instagram) akiwa Dubai Zembwela amemjibu mmoja wa wale kuwa;

"Sisi tulienda kushuhudia kama kweli wale jamaa ni wataalamu wa bandari na tulionyesha.

"Sasa ulitaka mimi mtu niliyesoma Sayansi Kimu nijiingize kwenye masuala ya vipengele vya Sheria, naweza wapi? Wapo wataalamu wa Sheria kama kina Kibatala, Lissu na wengine, hao ndio wajibu wao sasa wa kututetea tuwe na vipengele sahihi kwa manufaa ya nchi.

"Sheria siyo makalio eti kila mtu awe na elimu kwayo!"

Zembwela.
 
Umejitoa kwenye hii Sakata good msiwe mnaitumia hovyo watu wanakerwa sana na tabia ya kutetea hata usichokijua

Waandishi wa Habari tumieni taaluma yenu kuandika kweli siyo kutumika na kujipendekeza mchaguliwe

Tangu wameteuliwa wachache wenu mmeacha kazi yenu ya kufichua uovu Bali mnasifia tuuuuuuu usk na mchana

Naona Zembwela amepigwa kitu kizito kichwani
 
oky if so, alienda kutazama nn , au alienda kushangaa ma mitambo yanavyozunguka.

Maana hata yeye sio mtaalam wa mambo ya bandari Wala hana taaruma ya marine engineering .
 
Itakuwa alipima kwa macho ya kawaida.
Kwa macho ya kawaida alijuaje ufanisi? Hii leo ukimchukua mtu huko kijijini ukimleta hapa bandarini Dar, akiona mitambo ya TICTS ikifanya kazi, atasema inafanya kazi kwa ufanisi maana huko bush hata crane ya kubeba mizigo ni nadra kuonekana. Huenda ugeni wa mazingira ulimfanya afikie hitimisho alilolifikia.
 
Back
Top Bottom