Zelensky: Kufeli kwa mazungumzo kutamaanisha 'Vita vya Tatu vya Dunia'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa anaamini kushindwa kufanikisha mazungumzo ya kumaliza uvamizi wa Urusi kutamaanisha "vita vya tatu vya dunia".

Akizungumza na CNN Jumapili, Zelensky alisema yuko tayari kuzungumza moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin, akiongeza kuwa anaamini kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee ya kumaliza mapigano.

"Nadhani tunapaswa kutumia muundo wowote, nafasi yoyote ili kuwa na uwezekano wa kufanya mazungumzo," alisema.

Hata hivyo, Zelensky alisema kuwa anakataa makubaliano yoyote ambayo yangehitaji Ukraine kutambua maeneo yanayojitenga yanayofadhiliwa na Urusi kuwa huru.

Rais wa Ukraine alisema anaamini kwamba kama nchi yake ingekuwa mwanachama wa Nato, "vita havingeanza".

"Ikiwa wanachama wa Nato wako tayari kutuona katika muungano, basi fanya hivyo mara moja," alisema. "Kwa sababu watu wanakufa kila siku".

Hakuna kusalimu amri

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeutaka mji unaokabiliwa na mgogoro wa Mariupol ujisalimishe ifikapo 05:00 saa za huko Jumatatu asubuhi - pendekezo ambalo Ukraine imekataa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Urusi la Ria Novosti, wizara hiyo imesema kuwa itafungua korido za kibinadamu ili kuruhusu wakaazi kuondoka ifikapo saa 10:00 kwa saa za huko (08:00 GMT) ikiwa itapata jibu la maandishi kwa pendekezo hilo.

Kanali Jenerali Mikhail Mizintsev, mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Usimamizi wa Ulinzi cha Urusi, alinukuliwa na Ria Novosti akisema kuwa maafisa wa eneo hilo watakabiliwa na "mahakama ya kijeshi" ikiwa hawatakubali masharti ya kujisalimisha.

Mapema Jumatatu, Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alisema kuwa kunaweza kuwa "hakuna swali" la kujisalimisha.

"Tayari tumefahamisha upande wa Urusi kuhusu hili," alinukuliwa akisema na Ukrainska Pravda.

Chanzo: BBC Swahili
 
Volodymyr Zelensky aseme kwenye vita ya tatu ya dunia Tanzania itakuwa inakiwasha ⁷ na nani? Tunagombea nini?

Ratiba imepangwa na nani? Na Tanzania tuko kundi gani?
Mimi naomba tupangiwe na Malawi au Burundi ili tushinde asubuh tu. Tukiwekwa na Kenya mziki utakuwa mgumu na mshindi hatabiriki. Tanzania vs Afghanistan lazima tuchakae
 
Wewe na ndiye unayekunya, watu wanajuwa wanachokifanya tulia tuone huyo muliyekuwa munampamba na kumsifu kwamba ndio baba wa dunia hii Putini, taarifa tulizonazo Moscow wanapanga foleni kununua kilo ya sukari muda huu
wew acha kudanganya watu, uko moscow ipi? Sisi tunawasubili muingize timu zenu za magumashi. Sio mnapiga kelele tu mpo nje ya uwanja.... Nyie kama wanaume ingieni uwanjani tukinukishe...
 
Wewe na ndiye unayekunya, watu wanajuwa wanachokifanya tulia tuone huyo muliyekuwa munampamba na kumsifu kwamba ndio baba wa dunia hii Putini, taarifa tulizonazo Moscow wanapanga foleni kununua kilo ya sukari muda huu
Huyu hapa comedian hajui NATO wana mpango gani kaamua kukubali yaishe soma hapa:
t’s a compromise for everyone: for the West, which doesn’t know what to do with us with regard to NATO, for Ukraine, which wants security guarantees, and for Russia, which doesn’t want further NATO expansion,” Zelenskyy said late on Monday in an interview with Ukrainian television channels
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom