Ze komedi...

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
-Vijana wabunifu sana, wasanii wa kweli! Walianzia EATV-walifanya vizuri, wakawa maarufu wakaitwa Bungeni mpaka Ikulu wakajisahau wakadhani ni maarufu kuliko EATV yenyewe, wakatemwa!
-Wakaja TBC wakaanza vizuri, wakapata tenda nono, wakajiona wako juu ya DUNIA, matanuzi kwa sana, wakaanza kutukana watu (kwamba wamefulia)!
-Sasa, hawana mvuto, hawaeleweki wanafanya nini, wanaburudisha au wanaganga njaa tu! mashabiki hakuna tena, Wapo TBC tu kwa sababu ya Contract ya Vodacom, Ikiisha-KAZI BASI! Warudi kijiweni...

Tuwaite nao wamefulia kama walivyowaita wenzao??
Message;
Ukiwa Juu usijishau na usione wengine ni wapumbavu badala yake ongeza juhudi zaidi na heshimu watu wote!
 
siku hizi masanja anatumia muda mrefu kujiboost wakati hamna kitu wale wa chanel 5 wanakuja vizuri not bad
 
Futuhi nao sijui kimetokea nini huko. Ila wamejipanga tena. Nawamis wale wakongwe
 
Mafundisho yapo mengi mazuri but ili wakubalike zaidi waache kuvaa nguo za kike kila mara maana yake nini!
 
ubunifu kwisha kazi hakuna jipya ni yale wanarudia waingie kwenye tamthilia au maigizo barabarani,
 
Lugha za matusi na kutukana watu ndo walidhani ndiyo uchekeshaji, ilifikia wakati inakuwa ngumu kuangalia na watoto au wakwe, Inabidi wabadilike sana kwani wao si wakubwa kama uchekeshaji wenyewe, nazikumbuka enzi za kina mzee Jangala, Kiatu, pia kina Pembe na maigizo yao
 
Hii nayo pia ni indicator ya kwamba "watanganyika si mabwege tena". The biggest problem ni kwamba walivyohamia huko TBC wakaanza kuplay against the people. Tunaowaita mafisadi wao wakawa wanawasifia, wakakejeli watu wanaoaminiwa na watanzania mfano Dr. Slaa, wakawa hawapo tena update with the issues. Hebu imagine the following opportunities kwa comedian:

1. JK alivyoanguka jukwaani

2. Kuvua magamba

3. Mafisadi kuendelea kupeta ilhali wabunge wa upinzani wakikamatwa kwa masuala ya kisiasa.

4. Kujiuzulu kwa Makamba

5. Nape etc.

Sasa wako upande ule hawawezi tena kuikejeli CCM wala serikali yake maana ndiyo upande wao. Hii inanikumbusha marehemu Kolimba, kwa wanaomfahamu the guy wa one of the samartest and a no non-sense person. Wakampa licheo CCM akaanza kutetea yale asiyoamini baadae akawa anaonekana kituko na asiye na mvuto.

Vipaji bado wanavyo, wakihama tu upande you will see!!!!! Umaarufu utarudi pale pale au hata zaidi.
 
Atabaki mzee majuto tu, na ataendelea kubaki King Majuto!, Ataendelea kusumbua MBAYA KABISA

Kamasanja kana lugha flani ya Kebehi sana, kweli maskini akipata......
 
kuna kipindi walimkejeli mzee mengi wa itv,tangu pale siangalii tena kipindi

Kuna laana hata kama mtu sio mzazi wako, malipo ni hapa hapa.

Wale watoto (Joti na Mpoki) Walikuwa pale na walikuwa wanalazimishwa enzi hizo mpaka director wao Seki, wanacheza cheza tu, hovyo kabisa wakaingia EATV wakapata umaarufu, wakapata umaarufu, wakajifanya wajanja, Hakuna mwanzo usiokuwa na Mwisho!.

Kauli za masanja ni mbovu sana bora watu wengine wowote lakini sio masanja!
 
Back
Top Bottom