Zawadi ya pesa kwenye sherehe....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Kila ninapoenda kwenye harusi au sherehe za birthday
au nyinginezo kuna kitu huwa kinanishangaza sana....

Nacho ni utamaduni wa watu kutoa zawadi ya pesa.....

Tena wakati mwingine unakuta mc anasisitiza kabisa kuwa zawadi ni zawadi
chochote ulichonacho wape maharusi au mwenye sherehe mfano birthday hivi....

Swali hapa ni hili,zawadi si inatakiwa kuwa kitu kitakochobaki kwenye kumbukumbu..?

Je zawadi ya noti ya elfu kumi au hata laki utaikumbuka kwa miaka mingapi?

Jee huu utamaduni ni sahihi???????

Hatuwezi kuanza kubadilika na kutoa zawadi zenye maana zaidi
zinazo last forever?????????

Nyinyi humu mnasemaje???????????
 
hakuna kinacho dumu maisha vile vile......

badala ya kumpa mtu kanga ambayo inaweza kuchakaa baada ya muda ambayo pengine mhusika anazo mivao mingi mno na asingehitajia, bora hata umpe pesa akachange pamoja akanunue kile anachokihitajia kwa wakati ule.
 
Kila ninapoenda kwenye harusi au sherehe za birthday
au nyinginezo kuna kitu huwa kinanishangaza sana....

Nacho ni utamaduni wa watu kutoa zawadi ya pesa.....

Tena wakati mwingine unakuta mc anasisitiza kabisa kuwa zawadi ni zawadi
chochote ulichonacho wape maharusi au mwenye sherehe mfano birthday hivi....

Swali hapa ni hili,zawadi si inatakiwa kuwa kitu kitakochobaki kwenye kumbukumbu..?

Je zawadi ya noti ya elfu kumi au hata laki utaikumbuka kwa miaka mingapi?

Jee huu utamaduni ni sahihi???????

Hatuwezi kuanza kubadilika na kutoa zawadi zenye maana zaidi
zinazo last forever?????????

Nyinyi humu mnasemaje???????????

the boss naomba unipe mfano wa zawadi zinazolast forever unayoweza kupewa ktk sherehe,
sioni ubaya wa kupewa pesa kama zawadi,pia kuna wale wanafunga ndoa tz lkn hawaishi tz hivyo zawadi ya pesa ni nzuri kuwapa,pia ukipewa zawadi ya pesa utanunua ukipendacho na ambacho huna,coz mara nyingi watu wanaweza kukununulia masufuria au vitenge ambavyo tayari unavyo.hata hivyo zawadi ni zawadi haijalishi ni pesa au chochote mradi kiwe kimetolewa kwa upendo.
 
Back
Top Bottom