Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,502
- 9,282
Wafanyabiashara wa Nafaka na Matunda waoshusha mizigo yao katika Bandari ya Malindi wakitokea Tanzania Bara, wamekwama kushusha Bidhaa kutokana na kupanda kwa ushuru wa utoaji wa Mizigo
Mfanyabiashara Hassan Hamad anasema Mzigo wake umekwamba kwasababu Ushuru ulioletwa hakuwa na taarifa nao ambapo anasema Mzigo aliokuwa analipia Tsh. 56,000 sasa hivi ametakiwa kulipia zaidi ya Tsh. 240,000
Mgomo huo umekuja baada ya siku moja serikali ya Zanzibar, kubinafsisha shughuli za utendaji wa bandari ya Malindi kwa Kampuni ya African Global Logistics (AGL) ya Ufaransa.
Wakizungumza na waandishi wa habari wafabiashara hao wamesema kimsingi wafanyabiashara hawakatai, Bandari kubinafsishwa lakini serikali inapaswa kuwawekea mazingira wezeshi ili kumudu biashara zao bila ya vikwazo vya ushuru
Akizungumzia mgogoro huo Afisa Uhusiano wa Shirika la Bandari Zanzibar, Hassan Amour amesema viwango hivyo vya ushuru vipo tokea zamani lakini vilikuwa havitumiki ili kuwapa unafuu wafanyabiashara hao.
Hata hivyo amesema baada ya kuingia uongozi mpya wa kampuni ya AGL ya Ufarasa, walihitaji kukabidhiwa kumbukumbu zote za nyaraka za uendeshaji ikiwemo na tozo bandarini hapo na kuanza kuzitumia.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar, Joseph Meza, akizungumza na waandishi wa habari, amesema kubinafsishwa kwa shughuli za bandari ya Malindi kutaongeza ufanisi ikiwemo makontena ya mizigo kutolewa kwa muda muwafaka.
Nipashe/IPP Media