Zanzibar: Pemba hali ni tete, vurugu kati ya Polisi na raia

Status
Not open for further replies.
Waungwana mliopo zenji tunaomba updates za huko,au mitandao haifanyi kazi..
Mkuu huku watu wanajiandaa na uchaguzi wa marudio. Hata hivyo cuf imesimamia msimamo wa kutoshiriki isipokuwa wagombea ubunge na udiwani wengi kutoka cuf wanapita nyumc kwa nyumba ili kuwaeleza watu wawapigie kura na ikitokea wamepita waseme 'ilitokea kwa bahati mbaya lakini sikupenda' Tatizo njaa ndo zinasababisha kukosa msimamo.
 
Twende kwenye Mada,
Zanzibar hali si shwari, mabomu yameripotiwa kulipuka sehemu kadhaa visiwani humo, nyumba zimechomwa moto huko
pemba nk.
Swali nalouliza, maalim seif yuko daresalaam katika hotel ya serena.

Kama kiongozi ambaye amekuwa akitahadharisha serikali kuwa hali ya machafuko inaweza tokea kama mchakato wa kumtangaza kama mshindi rasmi wa urais wa zanzibar, na kweli kuelekea tarehe ya Uchaguzi visiwani humo, mambo hayo yameanza kujitokeza.na yeye maalim katika hali isiyoeleweka ameendelea kuishi serena hotel,
Je ndio kukimbia kwenyewe au?
Kama ni mapumziko baada ya matibabu, kwani nyumbani kwake zanzibar hawezi kupumzika?.
Je itakuwaje akae hotelini kwa gharama za serikali ambayo haitambui?
View attachment 329946
Unajua sababu za kuwepo hapo Serena? Alifika hapo akitokea wapi?
Kabla ya kuja kuhara humu Jf muwe mnatumia hata akili ya kiroboto kufikiria. Magu na Shein walienda kumwona Seif hapo Serena kwa kipi?
 
Viongozi wa dini wameshaonya kuhusu kutumia nguvu kubwa za kijeshi kufanya uchaguzi hewa Zanzibar lakini viongozi wa Tanzania kimya wameziba masikio.. Mungu tunaomba utupatie viongozi wataotawala kwa haki na amani
 
Kama kulinda nchi yetu dhidi ya watu wabaya na walafi kama fisadi Lowasa &Co. unaita ni ukandamizaji basi na iwe hivyo!
Najua bila ya kumtaja Lowassa hauli ukashiba, lakini hebu tujadili kimantiki, kwani ni halali kwa askari kutumia zana za kivita kwa raia wa nchi yao? Hujui kwamba JWTZ inatamkwa kwamba ni jeshi la kulinda mipaka ya nchi yetu, unaelewa maana yake?
 
Ndiyo kwanza tumeanza kuwachana watanyooka tu ngoja tujiweke sawa bunduki zipo nyingi na risasi za kutosha sisi kazi yetu kuwatwanga tu.


This is so much irresponsible of you blood sucker! Lets not get to this mess, please. Nashangaa sana watu wanaoshabikia vurugu za Zanzibar, hata sisi wa Bara hatutakuwa salama, sipendi kabisa watu wafe eti kwa sababu za kisiasa. Nachukia sana watu ambao hawaoni mbali kuhusu hili jambo. Sooo sad!

-
 
Mkuu huku watu wanajiandaa na uchaguzi wa marudio. Hata hivyo cuf imesimamia msimamo wa kutoshiriki isipokuwa wagombea ubunge na udiwani wengi kutoka cuf wanapita nyumc kwa nyumba ili kuwaeleza watu wawapigie kura na ikitokea wamepita waseme 'ilitokea kwa bahati mbaya lakini sikupenda' Tatizo njaa ndo zinasababisha kukosa msimamo.
Ushabiki
 
Walishasema hawataachia kwa nchi kwa karatasi sasa acha mtutu ufanye kazi.

Hizo bunduki na mabomu yapo kila mahali au hawa viongozi wa kibongo wanafikiri wanazo wao tu.

Hapa ndiyo pale mzungu anapofurahiaga kwa kuuza silaha na kubeba rasilimali za nchi kiulainii kisha anatuachia urithi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe
Kinachotokea zanzibar kinasikitisha sana,
wakati mwingine unaweza kujizuia kuongea chochote kuhusu zanzibar lakini utalazimika kulingana na hoja zinazojengwa humu,

wazungu ni werevu sana wanajua africa na nchi za kiarabu kuna lasilimali kubwa sana kwa ustawi wa nchi zao, naamini hadi leo wanajuta kwa nini walikubli kuyaachia makoloni yao.

Na lazima watengeneze kila mbinu waendelee kuvuna mali hata kwa gharama ya uhai wetu.

nchi ya siria ni mfano hai sasa imebaki magofu tupu raia wengi wamekufa,

eti baada ya watu kupoteza maisha yao na nchi kuharibika sasa ndio wanakaa kwenye meza ya mazungumzo kwa nini wasikae kabla?

Nani kafaidika? wapinzani waliokuja kwa gia ya kuleta maisha mazuli? au serikali iliyoamini ndiyo yenye haki ya kutawala?

ifike wakati wananchi tusiwe watumwa wa wanasiasa, wanaotugombanisha ili kupata nafasi ya madaraka.

lakini pia kwa kuwa tumekubali kuwa nchi ya kidemokrasia tukubali kuruhusu demokrasia itawale na maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.

ikishindikana majadiliano yafanyike kabla ya madhara kutokea,

tusikubali kuwakaribisha wazungu kuja kuvuna rasilimali zetu kwa gharama ya uhai wetu.

TANZANIA NI MUHIMU KULIKO KITU CHOCHOTE TUDUMISHE AMANI.
 
Atakuambia usalama na amani yetu sio jukumu lake yeye kachaguliwa kutumbua majipu tu sasa na seleka likikomaa tukaanza kukimbizana hapa nyumbani sijui atamtumbua nani,kaka ake anajua sana kucheza hide and seek alimuachia huu msala makusudi kama kipimo hakika udhaifu wake utajianika karibuni kwa hilo linalokuja.
 
Pemba hali ni tete, vurugu kati ya maafsaa wa polisi na raia zimeripotiwa hii Leo huku mamia ya wapemba wakikimbilia Mombasa katika nchi jirani ya Kenya.

Ikumbukwe vurugu hizi zinakuja ikiwa ni Siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi visiwani humo ndugu Jecha kutoa waraka wake kwa vyombo vya habari kuwa hali ya usalama visiwani humo ni salama na Amani.

Mungu iepushe Tanzania na haya majanga
10376863_244269689243989_3740904164997124683_n.jpg

10363330_244269699243988_2952147378466933171_n.jpg

1915685_244269742577317_6720535532716214146_n.jpg

12821400_244269919243966_2618324487934497365_n.jpg
Mods huyu apigwe ban, hakuna kitu hicho na picha za vurugu hizo ni za miaka ya nyuma sana.
 
Hiyo sio Pemba jamani wacheni kutudanganya, hiyo ni Unguja na inaonekana hizo Picha sio za Jana wala leo. Ukiangalia kuna Daladala ya KIJICHI-SPICE (511). Mleta mada tuambie ukweli, hali ya Pemba haiko ivo.
 
Hiyo sio Pemba jamani wacheni kutudanganya, hiyo ni Unguja na inaonekana hizo Picha sio za Jana wala leo. Ukiangalia kuna Daladala ya KIJICHI-SPICE (511). Mleta mada tuambie ukweli, hali ya Pemba haiko ivo.
Apigwe ban haraka kabla hajachafua hali ya hewa! Mjinga sana huyu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom