Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MHE. JUMA USONGE - ZANZIBAR NYAMA NI ELFU 13 KWA KILO, TANZANIA BARA NI ELFU 6-7 KWA KILO
"Ipo tozo ya halmashauri, ipo tozo ya kijiji ambayo inachajiwa kwa ng'ombe yuleyule mmoja anayeenda Zanzibar, ipo tozo ya TRA, TPA, tozo ambayo inaitwa export leave ambayo hata Mkenya akija kununua ngombe anampeleka Kenya hii anachajiwa, ambayo na Mzanzibar anachajiwa," - Mhe. Juma Usonge
"Tozo ambazo zimekuwa kichefuchefu kwa Zanzibar na zinazopelekea bei ya nyama kuwa nzito, kuna tozo inaitwa Wizara ya Mifugo inayotoza ng'ombe anayepelekwa Zanzibar, ikiwezekana hii ifutwe kabisa na isamehewe, sote ni nchi moja na tunafanya kazi kwa pamoja,"- Mhe. Juma Usonge
"Bei ya nyama ukilinganisha Bara na Zanzibar ni tofauti sana, Bara nyama inanunuliwa kwa kilo moja ni elfu 6 hadi elfu 7, lakini Zanzibar kilo moja ya nyama unanunua kwa shilingi elfu 13 na kuendelea, yote hii inasababishwa na Wizara haijaamua kusamehe baadhi ya tozo,"- Mhe. Juma Usonge.