Zanzibar itapojitenga na Tanganyika: Itaendelea kuliko Singapore au Dubai

nakuunga mkono kama anajua hilo basi wazanzibar wangeipinga ccm kwa nguvu zao zoote but udini kama usemavyo mkuu unawasumbua sana! Ccm ndo imedumaza maendeleo ya bara hata visiwani! Tatizo wazanzibar hawamjui adui yao.

hivi kuichagua ccm ni kuendekeza udini? Ni dini gani hiyo naomba ufafanue hapa!
 
hakuna kitu kinachoniudhi ktk maisha kuliko mtu kuishi leo kwa kujisifia ya jana

jana ishapita na walioishi jana waliishi jana na mazuri au mabaya yao

sisi tunaishi leo na tuna mambo yetu tuache kuota tuwe na mawazo mazuri ya kuidhibiti vyema leo yetu
 
Kwanza uelewe kuwa Dubai haina Rasilmali yeyote ya kuizidi Zanzibar.

Haina hata mafuta ambayo nchi nyingi za kiarabu ndio yaliyowasaidia/yanayowasaidia kiuchumi.

Dubai iliendelzwa kibiashara na kufanywa kitovu cha biashara kati Yuropa, Asia, Afrika. Hakuna zaidi ya hilo.

Zanzibar, historically ndio iliokuwa kitovu cha biashara baina ya Yuropa, Asia, Amerika na Afrika.

Zanzibar ndio ilikuwa makao makuu ya biashara/uchumi ya Oman, Abudhabi, Baluchistan na nchi za karibu ya huko na karibu ya Zanzibar, zama hizo nyingi kati ya hizo nchi zilikuwa si nchi kamili na zilikuwa zikitaliwa na Sultan wa Oman ambae makao yake Makuu yalikuwa Zanzibar. Mpka alipoingia mkoloni, Mjerumani na Muingereza na kabla yao Mreno, ndio wakaziparaganyisha na kuanza kuzitawala kimabavu himaya za Zanzibar.

Sipo hapa kutowa somo la historia, lakini nimeona ni kubrief, kukubaisnishia kuwa Zanzibar inaweza kujitengenezea rasilmali biashara ki ulaini kabisa na kuipiku kimaendeleo Tanganyika kwa haraka zaidi, kwani Zanzibar kwa sasa ni nchi ndogo na inaweza kujiwekea na kujiletea maendeleo ya haraka zaidi ya Tanganyika. Seuse, kwa sasa inajulikana kuwa ukanda wa bahari inyoizunguka Zanzibar una rasilmali kubwa ya mafuta na gesi asilia.

Zanzibar ina wasomi wengi waliozagaa karibu dunia nzima wanaoweza kuwatosheleza, iwapo tu watawawekea mikakati ya kuwalipa na kuwaenzi vizuri. Wana wafanya biashra waliozagaa dunia nzima na iwapo watawawekea mazingira mazuri, wapo tayari kurudi na kuiendeleza Zanzibar.

Kwa kifupi, Zanzibar inaweza ikawa Singapore ya Afrika within a very short period. Let's say between 10 and 20 years. Provided, hakuna siasa za majungu na hakuna kuingiliwa kiuchumi na Tanganyika.
Nakubaliana kabisa historia inaonesha zenji kilikuwa kitovu cha biashara hapo kale, ila bidhaa muhimu kabisa iliyokuwa ikipatikana kwenye soko hilo enzi hizo ni slaves , bahati mbaya baada ya bidhaa hiyo kuharamishwa wadau wa soko hilo hawakuwa wabunifu wa bidhaa mbadala ya kuliendeleza soko hivyo kubaki historia. Hata hivyo penye nia pana njia na saa ya kukombozi ni sasa Zenji yaweza kabisa kuipiku Dubai,
 
Zakumi,
Enzi za ukoloni mbona hali ilikuwa hivyo? Makuli wa meli pale Bukoba walikuwa Warwanda na Warundi. Wapishi na walinzi kwenye meli za Ziwa Victoria walikuwa Wajaluo kutoka Kisumu. Sijui nini kilichotokea na kusimamisha uendelezwaji wa shughuli hizo. Kagame anajua kabisa na kukubali kuwa Tanzania ndiyo backbone yake.

Kwetu kwenye mashamba ya Mkonge wafanyakazi walikuwa wanatoka Rwanda, Burundi, Malawi na Mozambique. Hata Chiluba aliwahi kfanya ukarani Tanganyika.

Irony iliyokuwepo sasa ni kuweka matatizo ya kiuchumi kwenye muungano wakati matatizo hayo yanatokana na uzembe wa viongozi. Hivyo hata kutengana haitafanya kiongozi mzembe aliyetoka Zanzibar au Tanganyika kubadilika.
 
Nikuulize. Hivi Zanzibar inaweza kuuza bidhaa zake Rwanda na Burundi bila kupitia Tanzania bara? Au watapitishia Mombasa? Ninachosema ni kwamba Zanzibar haiwezi kuendelea bila kuitegemea Tanzania bara

Yaonekana hata map ya Bara la Afrika hujawahi kuitizama.Ukikaa Pemba North Kabisa ya kisiwa hicho, Mombasa ipo karibu kuliko Dareselaam.

Hivyo huna hoja ya msingi hapo kusema lazima Bandari za Tanganyika zitumike.Anyways, wengi ya watu hufikiria kama Zanzibar kujitenga ni ugomvi kati ya jamii hivyo Tanganyika kufunga boarder zake au Zanzibar kususa kufanya biashara na Tanganyika.Hili ni wazo potofu ambalo haliingii akilini kwa mtu mwenye kujadili uchumi.
 
Watu kwa kupenda kurahisisha mambo mhhhh!!!

Kutoka Pemba Kaskazini hadi Kenya Mombasa ni mwendo wa dakika kama 30 kwa boti.Na watu huenda kila leo kuuza karafuu zao kukimbia mazishi ya SMZ ya kuwabana wapemba kiuchumi.
 
MUDA UMEFIKA KWA WAZANZIBARI KUSIMAMA MUDA WENYEWE NDIO HUU! WASIMAME KWA PAMOJA NA KWA KiZALENDO WAUTUPE MBALI UMWINYI WA BARA NA UBINAFSI WASONGE MBELE,HUKU TUBAKI NA MCHWA WETU WASIOCHOKA KUTAFANA NCHI!
 
Back
Top Bottom