Zanzibar itapojitenga na Tanganyika: Itaendelea kuliko Singapore au Dubai

Kwanza uelewe kuwa Dubai haina Rasilmali yeyote ya kuizidi Zanzibar.

Haina hata mafuta ambayo nchi nyingi za kiarabu ndio yaliyowasaidia/yanayowasaidia kiuchumi.

Dubai iliendelzwa kibiashara na kufanywa kitovu cha biashara kati Yuropa, Asia, Afrika. Hakuna zaidi ya hilo.

Zanzibar, historically ndio iliokuwa kitovu cha biashara baina ya Yuropa, Asia, Amerika na Afrika.

Zanzibar ndio ilikuwa makao makuu ya biashara/uchumi ya Oman, Abudhabi, Baluchistan na nchi za karibu ya huko na karibu ya Zanzibar, zama hizo nyingi kati ya hizo nchi zilikuwa si nchi kamili na zilikuwa zikitaliwa na Sultan wa Oman ambae makao yake Makuu yalikuwa Zanzibar. Mpka alipoingia mkoloni, Mjerumani na Muingereza na kabla yao Mreno, ndio wakaziparaganyisha na kuanza kuzitawala kimabavu himaya za Zanzibar.

Sipo hapa kutowa somo la historia, lakini nimeona ni kubrief, kukubaisnishia kuwa Zanzibar inaweza kujitengenezea rasilmali biashara ki ulaini kabisa na kuipiku kimaendeleo Tanganyika kwa haraka zaidi, kwani Zanzibar kwa sasa ni nchi ndogo na inaweza kujiwekea na kujiletea maendeleo ya haraka zaidi ya Tanganyika. Seuse, kwa sasa inajulikana kuwa ukanda wa bahari inyoizunguka Zanzibar una rasilmali kubwa ya mafuta na gesi asilia.

Zanzibar ina wasomi wengi waliozagaa karibu dunia nzima wanaoweza kuwatosheleza, iwapo tu watawawekea mikakati ya kuwalipa na kuwaenzi vizuri. Wana wafanya biashra waliozagaa dunia nzima na iwapo watawawekea mazingira mazuri, wapo tayari kurudi na kuiendeleza Zanzibar.

Kwa kifupi, Zanzibar inaweza ikawa Singapore ya Afrika within a very short period. Let's say between 10 and 20 years. Provided, hakuna siasa za majungu na hakuna kuingiliwa kiuchumi na Tanganyika.
Usifikirie kuwa sihifahamu Historia ya Zanzibar, naifahamu sana...! Na kama kujivunia maendeleo ya karne zilizo pita basi Kilwa ndio ilikuwa inaongoza maana utawala wake ulikuwa kuanzia Pwani ya Somalia mpaka Msumbiji sofara, utawala ulioanzia mwaka 957 CE. Na visiwa vilivyokuwemo kati yake, Mombassa, Pemba, Zanzibar, Mafia, Comoro na Mozambique. Biashara zilishamili na ilifikia mpaka kujitengenezea sarafu yake...! Mambo yalikuja kuharibika walipovamiwa na Wareno mwishoni mwa karne ya 14...!

Haya ni mambo ambayo yeshapita, hizi ni zama tofauti na za zamani...! Unguja ilikuwa muuzaji mzuri wa Karafuu na mbata, soko ambaro hivi sasa limekamatwa na Singapore na kuna nchi zingine kama Guiana, Brazil na West Indies, hawa pia ni walimaji wazuri wa karafuu tena zenye ubora mkubwa.

Haya yote Zanzibar yamepotea na mchawi si Tanganyika ila Wazanzibar wenyewe. Kila kukicha tunasikia jinsi askari wa KMKM wakikamata wasafirishaji wa karafuu, wanao peleka nchi jirani... Kumbuka kuwa KMKM ni mali ya serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Tuzungumzie rasilimali zilizokuwepo Zanzibar kwa sasa, je kuna mkakati gani ambao serikali ya mapinduzi ZNZ inayo ili kujikwamua na lindi la umaskini uliokithiri hivi sasa. kumbuka kuwa wale waliokuwa kwenye serikali iliyo pinduliwa January 1964, wengine bado wapo hai. mauwaji ambayo wengi wenye asili ya Arabs na Indians waliuwawa katika mtindo wa genocide... Wapo na wana machungu na kile wanacho kiamini kuwa ni nchi yao halal kabisa, nchi ambayo wamenyang'anywa na machinja chija wa mauwaji ya halaiki (Kimbali). Rejea kitabu cha UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO kilicho andikwa na Aman Thani Fairooz, vile vile maelezo ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ambaye naye aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila ya kushitakiwa...!

Kwa maoni yangu mimi, ile dhambi ya mauwaji yaliotokea Mwaka 1964, ndio inaila Zanzibar hivi sasa, na itaendelea kwa karne nyingi sana.

ps364879_l.jpg

Kilwa Coin, c. 1315, Fitzwilliam Museum
 
Tatizo kubwa ni elimu ya chini kama Zanzibar haitatilia mkazo elimu haiwezi kuendelea.Zanzibar sijui hata kama wana university??
hujui kama wana university!!na utabaki hivyohivyo hujui,kwakua wajua lakini hutakikujua,una macho huoni unamasikio husikii.
 
province(zanzibar) yenyewe inategemea kila kitu kutoka bara, watakimbilia wapi? Huo ni upofu tu usiozingatia ukweli na uhalisia, waulize bajeti yao ni kiasi gani? Na inatoka wapi? Halafu bila hata aibu wanajifanya kutaka kujitenga,wakiulizwa wanatoka wapi wanasema zanzibar wakikana kwa makusudi utanzania hali halisi ndio unaowaweka hapo walipo...

ulİza kabla ya muungano zanzibar ilikua wapi na tanganyika ilikua wapi kiuchumi...jifunze historia kwanza ,sio una toa porojo...
 
X-PASTER nchi nilizotaja hapo juu zimeendelea kutokana na rasilimali watu. Watu hao waliweka mipango mizuri ya keuneleza nchi zao ikiwa ni pamoja na kuexploit resources chache walizo nazo kama land.

For that matter nchi yeyote ile inaweza kuendelea (ikitaka tu)as long as ina rasimali watu.

sasa hii rasilimali mdebwedo inaweza kuendelea kweli?
 
Kilicho waponza Zanzibar ni uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa awali. Walitishwa kuwa kama hamkuingia kwenye Muungano kuna njama za kuja kuwaondoa madarakani. Naam, hilo ndio kosa lao. Wakasaini Mkataba wa muungano mbi mbio bila hata kufikiri mara mbili, kwa sababu tu, ya uchu wa madaraka.

Zanzibar kiuchumi ilikuwa mbali sana, masomo yalikuwa bure, wazee walikuwa wakilipwa posho kila mwezi kupitia branchi. Mayatima wakilelewa na Serikali bure. Wazee wasiojiweza walikuwa na nyumba ya wazee wakiishi, kula kunywa bure. Hospitali zilikuwa bure. Economy ilikuwa one of the strongest katika Afrika kama si dunia ukilinganisha na idadi ya watu.

Zanzibar ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na umeme, TV ya rangi, bandari yeneye kufanya biashara za kimataifa. Na mengi mengineyo. Yote hayo yanaweza kabisa kujirudia na zaidi, iwapo tu, viongozi wataacha uchu wa madaraka na siasa za majungu na fitna zitakwisha. Na zaidi ni Tanganyika kutoingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.
 
............Zanzibar kiuchumi ilikuwa mbali sana, masomo yalikuwa bure, wazee walikuwa wakilipwa posho kila mwezi kupitia branchi. Mayatima wakilelewa na Serikali bure. Wazee wasiojiweza walikuwa na nyumba ya wazee wakiishi, kula kunywa bure. Hospitali zilikuwa bure. Economy ilikuwa one of the strongest katika Afrika kama si dunia ukilinganisha na idadi ya watu.

Zanzibar ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na umeme, TV ya rangi, bandari yeneye kufanya biashara za kimataifa. Na mengi mengineyo. Yote hayo yanaweza kabisa kujirudia na zaidi, iwapo tu, viongozi wataacha uchu wa madaraka na siasa za majungu na fitna zitakwisha. Na zaidi ni Tanganyika kutoingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.

Iwapo yote uliyosema hapo juu nikweli, unadhani nani amesababisha hali ya ZNZ imeporomoka?
Jibu mnalo lakini kila mkiambiwa mnakuwa wakali... CCM na serikali zake ndio wamewarudisha Wa ZNZ nyuma kimaendeleo, ndio haohao wamedumaza maendeleo ya Watanganyika. Lakini mkiambiwa hayo mnaanza kuingiza udini.
 
nakuunga mkono kama anajua hilo basi wazanzibar wangeipinga ccm kwa nguvu zao zoote but UDINI kama usemavyo mkuu unawasumbua sana! CCM ndo imedumaza maendeleo ya bara hata visiwani! TATIZO WAZANZIBAR HAWAMJUI ADUI YAO.
 
Kilicho waponza Zanzibar ni uchu wa madaraka wa viongozi wachache wa awali. Walitishwa kuwa kama hamkuingia kwenye Muungano kuna njama za kuja kuwaondoa madarakani. Naam, hilo ndio kosa lao. Wakasaini Mkataba wa muungano mbi mbio bila hata kufikiri mara mbili, kwa sababu tu, ya uchu wa madaraka.

Zanzibar kiuchumi ilikuwa mbali sana, masomo yalikuwa bure, wazee walikuwa wakilipwa posho kila mwezi kupitia branchi. Mayatima wakilelewa na Serikali bure. Wazee wasiojiweza walikuwa na nyumba ya wazee wakiishi, kula kunywa bure. Hospitali zilikuwa bure. Economy ilikuwa one of the strongest katika Afrika kama si dunia ukilinganisha na idadi ya watu.

Zanzibar ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na umeme, TV ya rangi, bandari yeneye kufanya biashara za kimataifa. Na mengi mengineyo. Yote hayo yanaweza kabisa kujirudia na zaidi, iwapo tu, viongozi wataacha uchu wa madaraka na siasa za majungu na fitna zitakwisha. Na zaidi ni Tanganyika kutoingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.
Dar Es Salaam, note maneno yangu "... ile dhambi ya mauwaji yaliotokea Mwaka 1964, ndio inaila Zanzibar hivi sasa, na itaendelea kwa karne nyingi sana."
 
Siku muungano huu ukivunjika nitafanya sherehe kubwa mno, hatuwahitaji hawa na wao hawatuhitaji huu ndiyo ukweli kwani siku zote kuna manung'uniko yasiyokwisha. Ndoa ikifika mahali ugomvi haushi na hakuna maelewano basi ni kupeana talaka tu.TUMEWACHOKA WAZANZIBARI NA WAO WAMETUCHOKA MUUNGANO UFEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
 
Tuwaache Zenji waende,wakiendelea si watatusaidia washirika wao wazamani na tutawaiga?Nendeni.Ila shida zikiwazidi MUSIRUDI!
Nendeni,Maelezo yamenukuliwa toka kwa prof wa Uchumi,sie twabwabwaja tu!
 
nanai anayewanga'nga'nia? hao ni wansiasa wenzao walio na masilahi kisiasa zaidi lakini kwa wananchi hawaoni wala faida yeyote inayolalia upande mmoja.
Sasa mbona tunawang'ang'ania na kuwachagulia viongozi kila kukicha??
 
Ile Zanzibar kabla ya uchaguzi ni tofauti na Zanzibar baada ya Uchaguzi ,kila siku maendeleo yanaongeza hatua ,kwa maana hata jana haifanani na juzi ,hapo Tanganyika tusubirini tu ,mkizubaa mtaona vumbi na hata njia tuliyopita hamutoweza kuitrace ili kutufikia.
 
Maendeleo ya maneno tu wazenji nawaamini. Kelele tuuuuuuuuuuuuuuuu hamna kitu. Mnatutegemea watanganyika kwa kila kitu! Tukiwaacha mmekwisha. Hivi Zanzibar tangau mwezi jana hadi leo nini kimeongezeka vile we mwiba! Yaani Seif kuwa makamu wa rais hapo tayari maendeleo siyo enhh!!!!???? Mi nilijua mmepigwa bao. Mmeolewa na mnafurahia ndoa ya bwana mpya. Sawa ngoja tuone!
 
Siku muungano huu ukivunjika nitafanya sherehe kubwa mno, hatuwahitaji hawa na wao hawatuhitaji huu ndiyo ukweli kwani siku zote kuna manung'uniko yasiyokwisha. Ndoa ikifika mahali ugomvi haushi na hakuna maelewano basi ni kupeana talaka tu.TUMEWACHOKA WAZANZIBARI NA WAO WAMETUCHOKA MUUNGANO UFEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.
Kuna rafiki yangu Mmoja Mganda. Alifanya sherehe kubwa sana Idi Amin alipompindua Obote. Haikupita muda nikakutana naye akilalamika huyu Idi Amin mtu baya sana. Anakinja watu. Tafakari
 
Kuna rafiki yangu Mmoja Mganda. Alifanya sherehe kubwa sana Idi Amin alipompindua Obote. Haikupita muda nikakutana naye akilalamika huyu Idi Amin mtu baya sana. Anakinja watu. Tafakari

Jasusi:

Kwa maoni yangu binafsi, idadi ya watu na eneo la Tanzania bara, ulitakiwa kuwepo uchumi wa nguvu wa kufanya watu kutoka katika nchi ndogondogo za maeneo ya Afrika mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Comoro, Zanzibar na Mafia kuja kufanya kazi za vibarua bila uchumi kuteteleka.
 
Zakumi,
Enzi za ukoloni mbona hali ilikuwa hivyo? Makuli wa meli pale Bukoba walikuwa Warwanda na Warundi. Wapishi na walinzi kwenye meli za Ziwa Victoria walikuwa Wajaluo kutoka Kisumu. Sijui nini kilichotokea na kusimamisha uendelezwaji wa shughuli hizo. Kagame anajua kabisa na kukubali kuwa Tanzania ndiyo backbone yake.
 
Kuna rafiki yangu Mmoja Mganda. Alifanya sherehe kubwa sana Idi Amin alipompindua Obote. Haikupita muda nikakutana naye akilalamika huyu Idi Amin mtu baya sana. Anakinja watu. Tafakari

Tatizo zanzibar hawatutaki wanaona tunawadhulumu, sasa katika mazingira kama haya ya kutoaminiana dawa ni kutengana, na kama kuna wa kujuta ni wao kwani ndiyo hawahitaji muungano kwa vile wana mafuta, lini umesikia watanganyika wanawatukana wazanzibar? Kila leo wazenji wanatukana watanganyika,WAONDOKE TUUUUUUUUUU
 
iwapo yote uliyosema hapo juu nikweli, unadhani nani amesababisha hali ya znz imeporomoka?
Jibu mnalo lakini kila mkiambiwa mnakuwa wakali... Ccm na serikali zake ndio wamewarudisha wa znz nyuma kimaendeleo, ndio haohao wamedumaza maendeleo ya watanganyika. Lakini mkiambiwa hayo mnaanza kuingiza udini.

kwa hiyo unashauri wazanzibari waunge mkono chama gani mbadala ili kuwarudishia maendeleo yao? Jee, unadhani chadema wapewe nafasi visiwani labda, huenda wakailetea zanzibar maendele? Yaani wafanye tena jaribio la tatu baada ya kuijaribu tanu na ccm sasa waijaribu chadema labda watafanya zanzibar kuwa pepo ya dunia?

Unashauri hivyo au una mbadala mwingine?
 
Back
Top Bottom