Zamani kupenda haikuwa Haki ya Mwanamke, Mwanamke anahaki ya kupenda pia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Anaandika, Robert Heriel.
Baba.

Zamani Mwanamke hakuwa na Haki ya kupenda, hakuwa na Haki ya kuchagua mwanaume WA moyo wake, Mwanaume anayempenda. Mwanamke alikuwa kama kikaragosi tuu kisicho na haki ya kuamua hatma ya Maisha yake katika mahusiano yake.

Mwanamke alichaguliwa Mume na akaolewa, ni wazazi wachache waliozingatia mioyo ya mabinti zao. Hiyo iliwafanya Wanawake wawe watumwa WA wanaume Kwa Milienia nyingi.

Lakini je, ni kweli Mwanamke Hana moyo WA kupenda? Hana Haki ya kupenda? Labda Hilo swali la pili ambalo linahusu Haki, Kwa maana Upendo ni moja ya Haki za Mwanadamu bila kujali ni Mwanamke au Mwanaume. Kuhusu moyo WA kupenda Hilo litajibiwa na watu wenyewe Kwa sababu Siri ya moyo niyamtu mwenyewe.

Wanawake nao wanayohaki ya kupenda. Kumpenda mwanaume wamtakaye bila kujali. Muhimu wazazi wanachoweza kufanya ni kumzuia Binti asiolewe mpaka apate Akili ya utambuzi(utu uzima) Kwa sababu Haki pia inaendana na utambuzi.

Mimi kama Baba, ndiye Taikon Mtibeli. Sitawachagulia Binti zangu Waume zao, nafasi yangu ni kuwapa miongozo na namna ya kufanya uchaguzi wao sahihi. Kwa Sababu mimi ndimi Baba yenu, nitaheshimu uamuzi wenu, nitaheshimu furaha yenu ikiwa tuu haivunji Kanuni za Asili, sheria za nchi na Imani ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Utaratibu huu mpya wa mwanamke kuchagua wa kumpenda na kuolewa nae ndo umezalisha masingle mothers wasio na idadi, ndo umezua talaka zisizoisha, ndo umefanya bikra zimekua adimu kama mataji pale Spurs.

Binti wa sasa hv katika kutafuta huyo wa kumpenda amejikuta anadeti na wanaume wasio na idadi, akishaachwa na huyu anatafuta mwingine mpaka siku anakutana na huyo husband wake tayari ameshatumika vya kutosha na pengine ameshazalishwa na wahuni huko mitaani. Anasubiriwa an innocent soul aje abebe majukumu ya kulea watoto wasio wake.

Mwanaume wa kutafutiwa anakua haina kudeti, yaani wazazi wakisharidhika inapangwa tarehe ya ndoa watu wanaoana. Waarabu na Wahindi huu utaratibu wanao mpaka sasa hivi na unawasidia sana.
 
Utaratibu huu mpya wa mwanamke kuchagua wa kumpenda na kuolewa nae ndo umezalisha masingle mothers wasio na idadi, ndo umezua talaka zisizoisha, ndo umefanya bikra zimekua adimu kama mataji pale Spurs.
Hapa kuna ukweli mwingi!
 
Tatizo wanawake Wenyewe ckuiz wamekuwa too much selective,na ndio maana wengi wao wapo single.Yaana unakuta dada wa watu mzuri tu Ana miaka 28 na bado anaishi na wazazi wake.
 
Back
Top Bottom