Zain promotion: Ni kweli ama batili??

MissKitim

Member
Apr 27, 2009
44
2
Wadau,
Naombeni msaada..
Ni kipindi sasa Zain wanaendesha promotion ambapo washindi wanatakiwa kupata sh. 500,000 cash kila siku, toyota corrola na ticket ya kwenda Africa kusini kila wiki, na mwisho wa promotion mshindi atapata RAV4.
Hii promotion ni kutuma neno JIVUNIE kwenda 15656, na unauliza maswali ambapo kila swali lina point na unakatwa sh 300 na ushee per SMS..Eventually unakusanya pointi ambazo zinaingia kwenye droo ya kupata hizo rewards juu.

NINACHOULIZA DRAW YA KUPATA WASHINDI INACHEZESHWA WAPI NA SAA NGAPI? MEANING KWENYE CHOMBO KIPI CHA HABARI???...WENGI WANASHIRIKI NA HELA ZAO ZINALIWA LAKINI HAWAJUI HII PROMOTION INACHEZESHWA SAA NGAPI NA WAPI..Hawaoni si TBC, ITV, STAR TV...nk
MBAYA HATA UKICHEKI MTANDAO WA ZAIN..UNAONA MAELEZO YA HII PROMOTION NA ZAWADI. KUNA TAB YA WASHINDI/WINNERS UKICLICK TOKA TAREHE WALIYOANZA HII PROMOTION HUONI HATA JINA MOJA LA MSHINDI..

TUELEWE VIPI? HELA ZA WATU ZINALIWA KINYEMELA AMA NI VIPI?
NAOMBENI MSAADA wa kujua hii kitu inachezeshwa wapi???
 
Utapeli wa hali ya juu...

ni deci mpya kwa jina jipya. mi mwenyewe nimevuna zaidi ya pointi 59000 sijaona chochote na maswali yao yamekaa kiubongo fleva fleva. kwa ujumla ni wizi mtupu na usijekuta tunachangia kijani na njano kwa ushindi wao wa kishindo.bora tigo nimeambulia 10m air time. ni matatizo yetu ya kutaka majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Matapeli wezi wakubwa hawa.Wanawaibia wateja wao mchana mchana jua linawaka.Kuna jamaa kafikisha point 700,000 hajapata hata fulana.Kila point ni shs 300 sasa huu kama si wizi ni nini?
 
Afadhali yenu , mimi nina pointi 1,500,000 kwenye promosheni ya Jikoki ya TIGO,sikushinda hata fursa ya kuambiwa umepata message za bure, wanakupoza kwa dakika tatu tigo kwa tigo na ndio imetoka,wote hao ni wezi na matapeli wakubwa
 
Hata mie nimeshtuka ndo maana imebidi niulize. Hapa ofisini wengi wanajibu hayo maswali, unakuta mmoja ana pointi laki 500 na mwingine ana point 50,000. Halafu wote wanaletewe message eti upo kati ya 30% au 10% ya wachezaji wa juu. No one ameshinda hata airtime.
Kama ulivyosema mdau wa juu,usikute tunachangia kijani na njano..mbona hizi promotion zimezidi hivi uchaguzi unavyokaribia?

Naona na vodacom wameanza the same promotion..ya kwao kali. One message sh. 500/=

kama kuna watu wa zain wanasoma humu, please clarify. Hizi laki 500,000 za kila siku, corolla na ticket za kila wiki na RAV4 ya mwisho zinachezeshwa WAPI (i.e in what media? na saa ngapi?

Inanishangaza
 
Honestly, i am still looking for an answer..was this a kiini macho kama wadau wanavyosema hapo juu ama? Hii promotion imechezeshwa wapi na mshindi wa RAV4 ni nani? Sijaona on any media? Sasa wamedai wameextend na kuna RAV4 nyingine.....Please mwenye jibu kamili
 
Leo wananiambia niko katika 5% wlio juu khaa...nina point 3500 tu.....halafu walisema mchezo mwisho 8/8/2010 na kuna mtu taondoka na RAV4 ya milioni 50....leo wanasema bado haijapata mtu na mchezo unaendelea...hivi hakuna watu wanaopaswa kukontroo hivi vitu?....wapi ile BAHATI NASIBU YA TAIFA?
 
Wizi mtupu! Hakuna njia ya mkato kupata pesa. Just work hard. Vinginevyo mko mikononi mwa deci
 
Wadau,
Naombeni msaada..
Ni kipindi sasa Zain wanaendesha promotion ambapo washindi wanatakiwa kupata sh. 500,000 cash kila siku, toyota corrola na ticket ya kwenda Africa kusini kila wiki, na mwisho wa promotion mshindi atapata RAV4.
Hii promotion ni kutuma neno JIVUNIE kwenda 15656, na unauliza maswali ambapo kila swali lina point na unakatwa sh 300 na ushee per SMS..Eventually unakusanya pointi ambazo zinaingia kwenye droo ya kupata hizo rewards juu.

NINACHOULIZA DRAW YA KUPATA WASHINDI INACHEZESHWA WAPI NA SAA NGAPI? MEANING KWENYE CHOMBO KIPI CHA HABARI???...WENGI WANASHIRIKI NA HELA ZAO ZINALIWA LAKINI HAWAJUI HII PROMOTION INACHEZESHWA SAA NGAPI NA WAPI..Hawaoni si TBC, ITV, STAR TV...nk
MBAYA HATA UKICHEKI MTANDAO WA ZAIN..UNAONA MAELEZO YA HII PROMOTION NA ZAWADI. KUNA TAB YA WASHINDI/WINNERS UKICLICK TOKA TAREHE WALIYOANZA HII PROMOTION HUONI HATA JINA MOJA LA MSHINDI..

TUELEWE VIPI? HELA ZA WATU ZINALIWA KINYEMELA AMA NI VIPI?
NAOMBENI MSAADA wa kujua hii kitu inachezeshwa wapi???

Hata Tigo wanaendesha kitu kama hicho kinaitwa eti JIKOKI, maswali wanayouliza na ahadi zinazotolewa ni pamoja na kwenda Afrika Kusini kuangalia fainali za kombe la dunia, Nahisi kuna utapeli pia. Wahusika kama wapo kwenye forum hii wajitokeze ili kusafisha hali ya hewa.
 
Na mtaliwa sana kwa kupenda vitu vya dezo. Halafu mi najiuliza, kama ma-griiti thinkas wa hapa JF wanaweza kuchotwa na utapeli kama huu hali ikoje kwa wananchi wa kawaida wasio na elimu.
 
Matapeli wezi wakubwa hawa.Wanawaibia wateja wao mchana mchana jua linawaka.Kuna jamaa kafikisha point 700,000 hajapata hata fulana.Kila point ni shs 300 sasa huu kama si wizi ni nini?

WAIT, anapoints 700,000*300=210,000,000!!!!! ( MILIONI MIA MBILI NA KUMI!!!), Ama kweli kuna watu wana fweza hapa bongo, hayo ni mavuno ya mwaka mzima!!!!!!!! mwe! hakyamungu ndiyo maana kuna watu bado wanacheza KARATA TATU! Sasa huyu anategemea zawadi gani itayorudisha hiyo fweza? gari yenyewe ni RAV4!!!! my my...............Au mimi mgumu wa kuelewa?
 
Jamani **** mtu anajua jisnsi ya kujitoa kwenye promotion ya ZAIN...they keep sending me those messenges and I m not interested in answering them.
 
WAIT, anapoints 700,000*300=210,000,000!!!!! ( MILIONI MIA MBILI NA KUMI!!!), Ama kweli kuna watu wana fweza hapa bongo, hayo ni mavuno ya mwaka mzima!!!!!!!! mwe! hakyamungu ndiyo maana kuna watu bado wanacheza KARATA TATU! Sasa huyu anategemea zawadi gani itayorudisha hiyo fweza? gari yenyewe ni RAV4!!!! my my...............Au mimi mgumu wa kuelewa?

Hiyo hesabu uliyopiga umenowa Amoeba, kwa sababu sms moja inakuwa na pointi kathaa
 
Na kweli hamna cha dezo, bure Ghali

...Ila unaesema great thinkers, hata great thinkers hucheza LOTTO kwa kutoa kidogo ili upate kikubwa..Ni part of life watu kujaribu bahati zao.
Ila iwe legal na kweli...sio kuiba hela halafu zawadi hazionekani. Honestly we could be contributing to a green and yellow party bila kujua.

Cha kushangaza, Mbona hizi promotion zimeshika kasi kipindi hiki cha uchaguzi, halafu zote Voda, Zai etc...wanadai mwisho October....mmhhhh?????
 
Yalinikuta nakijiondoa mapema maana nilihisi hali ya kuibiwa bila ya kujijua!!!
 
Kitu kingine kinachotia shaka kuhusu bahatinasibu hii ni aina ya wanayoyaita wao maswali; hebu soma hili kuona kama lina sifa ya kuitwa swali: "Jibu swali ujipatie pointi 2000; vipindi vya michezo katika TV, unapendelea mchezo gani? 1 = Kandanda, 2 = Basketi, 3 = Riadha, 4 = Mwingine". Linaweza kuwa swali, lakini sioni jibu ambalo litamfanya mtu awe amekosea kwani kila mtu ataeleza anachokipendelea.
 
Back
Top Bottom