Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 78
- Thread starter
- #61
Sasa mzee inatupasa kuchangia mawazo yetu katika academia ya Tanzania, Labda Prof Luhanga ameamua kwenda kufundisha UDOMNafurahi kama nimekuchekesha maana kucheka katika fikra hizi ni kitu adimu sana. Luhanga alikwenda sabatical leave uk baada tu ya kuondoka madarakani.
Ukiacha hayo, engineering consultancy bado tunaweza kupewa na watu hawa tunaowadharau kama ni wazee. Wanafanya hivyo sehemu nyingi tu. Namna tulivyowatumia hawa wataalamu ni ngumu kwao baada ya muda mrefu kazini kuanzisha kampuni halafu wakaziendesha kama wafanyabiashara. Impact yake ni kuwa tunawafanya hata wanaochipukia kuogopa kukaa ndani kwa kuhofia haya wanaoyaona kwa wale waliowatangulia.
Kama Kingunge analipwa kwa kulala ndani ya siasa za tanzania, je hawa wasomi ambao wanaweza kuwa na michango mikubwa ya maendeleo kwa nchi yetu wanalipwa wafanye nini? Ndio yale ya Prof Machunda na safari yake ya ukerewe