Yule ni "damu yangu" kabisa . . .

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Ivi kwanini mwanao ni "damu" yako na sio DNA yako? Damu inahusikaje apo wakati sperms ndo zilihusika? Kama ni damu, kwann mara nyingi group hazilingani?
 
Basi wewe uanze kusema "yule ni DNA yangu". Jee, kuna tatizo hapo?

Utoto mwingine haufichiki.
 
unataka kuiba mtoto? maana hilo jina, hahaha

anyway huu ni msemo tu, mfano kuna mwingine anaweza kukuambia nimekupenda au kukuchukia toka moyoni, hii haimaanishi kuwa moyo unahisia lkn ni njia moja wapo nzuri ya kufikisha ujembe.
 
Yaani jina lako wewe kujiita jambazi lazima unahusika na hayo ya ujambazi.

Usiwe na wasi weye mwite wako unavyosuggest.
 
mkuu production ni genetics inayotokana na genes .... damu huwa na chembe chembe za genes ambazo ndizo zinazotoa kiumbe ... DNA-Deoxyribo Nucleic Acid is a nucleic acid containing the genetic instructions used in the development and functioning of all known living organisms

ndiyo maana DNA test hufanywa kwa kutumia hata mate au fluids za binadamu .... hivyo basi worry not .... damu ndiyo chanzo cha reproduction of living things
 
Kwa maoni yangu hilo ni suala la lugha tu mkuu (Waziri (?) Nundu alisema 'figurative'!). Ni kama vile mtu akisema 'roho ngumu' au 'inavunja moyo' au 'unajipa moyo' nk zote hizi ukitaka kwenda kwenye maana ya neno kwa neno unaweza ona kuwa havi make sense kabisa!
 
unanikumbusha jamaa mmoja akiudhiwa anasema;

'na huyu ni bao kama mabao mengine'
kwa kifupi ni 5-0
 
Hahahaaa, kuna baba mmoja alimkataa mwanae kwa sababu alikuwa na Group tofauti la damu. Yaani baba na watoto wake 5 wlikuwa na group "O" na yule mmoja akawa na Group "A". Baba akasema huyo wa group "A" sio mwanae, na hivi sasa ana ugomvi mkubwa na mkewe akiamini alizaa nje ya ndoa.
 
Ivi kwanini mwanao ni "damu" yako na sio DNA yako? Damu inahusikaje apo wakati sperms ndo zilihusika? Kama ni damu, kwann mara nyingi group hazilingani?

Mtoto wako lazima awe na sehemu (%) ya DNA yako ingawa inawezekana akawa na blood group tofauti na wewe. Kinachoangaliwa ni pairing of chromosomes. Hv ulisoma arts eeeh ?!
 
Hapo zamani hakukuwa na kipimo cha DNA, kulikuwa na kipimo cha damu. Ikiwa mumefanana groups basi ndiyo mwanao, ikiwa tofauti basi siye. Lakini siku hizi mambo yamekwenda mbele zaidi na vipimo vya DNA ndiyo vimeshika kasi na ni vya uhakika zaidi.

Ndiyo maana ukaja msemo 'huyu ni damu yangu'
 
Basi ukitaka kujua kama mtoto ni wako au la toa sperm zako na zake ukapime.
 
unataka kuiba mtoto? maana hilo jina, hahaha

anyway huu ni msemo tu, mfano kuna mwingine anaweza kukuambia nimekupenda au kukuchukia toka moyoni, hii haimaanishi kuwa moyo unahisia lkn ni njia moja wapo nzuri ya kufikisha ujembe.

sa kwann tunaongea vitu ambavyo kiuhalisia sivyo?
 
Jamani mtu kama umesoma social science ni vema ukawa mpole tu ukasubiri wataalam wakadadavua vitu kuliko kuparamia. Sasa kuna ubaya gani kusema damu yangu? Ulitaka watu tuseme huyu ni sh.h.wa zangu? Nyamb..f!!
 
Back
Top Bottom