Yule Mzee aliyekatiza Uwanjani...

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
Nadhani kwa mliowahi uwanjani siku ya mechi ya Yanga na Zamalek mlijionea miongoni mwa vituko ni yule babu aliyevalia American Suti (kwa muonekano alikua mithili ya mjumbe wa KAMATI YA UFUNDI) ambaye aliamua kwanza kwenda kwenye lango la upande ambao Zamaleki walikuwa wanapasha alizozana kidogo na kocha wa makipa wa Zamaleki na kisha kuamua kukatiza uwanjani bila wasiwasi au bughudha yoyote..

.........Nilidhani mambo haya yalkiishia wakati ule wa shamba la Bibi.............
 
Kama hayo yametokea, ujue wamewachokoza waMisri, Yanga wakienda kufanyiwa vituko huko Misri wasije wakasema ndio sababu ya kufungwa. Tumeyaanza wenyewe.
 
hivi kwani wataenda kucheza egypt? nawashauri Yanga wasiende labda kama wanaenda kukipiga nchi nyingine
Mkuu Misri Lazima waende, Zamalek walikuja Dar kutoa POSA TU, kule ndio NDOA yenyewe...............najua unazungumzia kuhusu yae machafuko...........imegundulika yaligubikwa kisiasa zaidi na ile mechi ilishachezwa na Ligi ya Huko Karibu Inaanza.........Labda Yanga waweke hoja ya pingamizi kwa minajili ya kujinusuru tu!!!!!!.........
 
Ndiyo maana sipendi mpira wa Tanzania. Huwezi kuwa na akili timamu ukapenda mpira wa Tanzania. We mpira gani usio na akili, jiulizeni toka Simba na Yanga wameeanza kutumia uchawi badala ya vipaji wamechuma nini Africa Kama si kuambulia mayai viza kila kukicha. Wachezaji wa Simba na Yanga wanaroga mpaka kocha ili wapangwe? Mpira si uchawi kamwe bali ni kipaji. Watanzania hamkeni jamani.
 
kafe huko!
Tangu ndumba zianze Simba imefika fainali ya kombe la shirikisho na imefika robo fainali ya Champions League.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom