Yuko Chuo Kikuu ila anataka kurudia mtihani wa CSEE kama PC

Usifikirie ulipo tu,fikiria miaka ijayo atakapomaliza hizo ajira zitakuepo?

Mwaka jana wanafunzi kadhaa waliomaliza masomo ya udaktari wameshindwa kufanya internship kutokana na serikali kutokua na fedha za kuwalipa, na wanaofanya wanasign mkataba wa kukubali ucheleweshwaji wa malipo sasa huyo anayeanza kusafisha cheti cha form four akija kufika huko itakuaje, aendelee tu na degree yake aliyokua anasoma.[/QUOTE

ukifanya unachokipenda hata pesa itakua nyuma ya, sio wote wanaosoma MD zilikua ndoto zao HAPANA bali mazingira ya nchi, utakuta waliopenda kua pilot,geologst,eng,tichas etc etc
 
Kaka yangu Alipata div 2 pt 11 ya pcb..., Mwaka 2009 alienda kusoma advanced diploma ya Acc ifm baada ya kukosa mkopo bodi..kpnd hicho anasema div I I boys walikosa mkopo wasichana ndo walikuwa wana pata ila kwa boys ni div I tu... Bahati Alikuwa analipiwa kila kitu na Ministry of Finance na haikuwa mkopo bali grants..Ministry of Finance ndo ilimvutia na hakuna kingine chochote ukizangatia familia ilikuwa choka mbaya..... Wakat anasoma ifm mara kwa mara alikuwa akitueleza kwamba hafurahii kabisa anachokisoma... Bahati nzur mwaka 2009 alifanikiwa kumaliza masomo yake.... alikaa karibu miaka miwili home bila ajira hii ili mfanya kuwa mtu wa mawazo mda wote mpaka nikawa namuonea huruma aisee.... Mwaka wa tatu alifanikiwa kupata kazi kwenye Ngo moja... Alifanya hiyo kazi mwaka mzima ila mara nying alikuwa akitueleza kwamba hafurahii kuwa muhasibu anataman sana angekuwa Dr ila alikuwa anahofu umri ni tatzo kwa sababu alikuwa na 29 by that time... Siku moja tulikuwa wote kanisani kuna Padre mgeni miaka 45-"49 hiv mtu mzima sana tu akawa anajitambulisha baada ya misa... Akasema yy anatokea jimbo la Mwanza na amekuja kusalimia tu na anasoma diploma ya Clinical Officer pale Sengerema na yuko sec yr.... Yule Father alikuwa kama Ameya boost mawazo ya bro.... Tukiwa home aliniita na kuniambia dogo sikiliza nataka nirudi shule, mm nikahisi labda anataka soma cpa akaniambia hapana nataka nikasome MD.. Nikamuuliza kazi vp akaniambia anaacha.. Na kwel baadae aliacha Kaz na ninavyoandika sasa chuo kikifunguliwa atakuwa mwaka wa pili MD pale Muhimbili.... Never Give Up Follow Ur Dream... Mungu amsaidie katika masomo yake AMINA.

Nimemaliza Diploma ya Mechanical engineering DIT ila now nimeamua nibadilishe fani nimeapply Laboratory technology ngazi ya diploma ni jambo la kawaida sana kupigania elimu inayofaa ktk mazingira unamoishi
 
Back
Top Bottom