Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Alikuwa noma km Lisu bungeni, wakambana sana.
Alitimuliwa kufundisha UDSM, kisha wakamzuia ku practice uwakili.
Njaa ikazidi, akarejea gambani na kupewa ubunge wa viti maalumu na Rais Mkapa.
Kuna kipindi nilisikia ni mwanasheria wa CCM.

Walimfanyia kitu mbaya so alikuwa hana ujanja, kwa kipindi kile ccm walikuwa wanakubania kila kitu ukiwa kinyume nao thats what they did to the dude, labda kama anaweza kwa sasa arudi upinzani ni mtu mwenye uwezo wa kujenga na kutetea hoja. Walimmaliza ila anaweza kuwa lulu kama atahamia the dream team! Hata mahakamani pia ni jembe sana sema ndo hivyo tena kila mtu ana maisha yake.
 
acheni kuchonga mzee wa watu katulia zake ni Lecture wa kutegemewa vyuo vitatu nenda Mzumbe,Tumaini na Secuco
 
Wakuu kama mlivyopata taarifa, Mh. Roman Shao, Diwani Kata ya Makiidi - Rombo (CCM) amefariki hivi leo huko KCMC - Moshi. Huyu ni Baba Mzazi wa Mh. Joseph Selasini, Mbunge wa Rombo (CHADEMA) na pia ni Baba Mzazi wa Dr. Masumbuko Lamwai.

Hebu kipindi hiki cha majonzi kwa familia yao tuungane nao kuwafariji, hayo mengine mtajadili baada ya msiba kama kutakuwa na umuhimu au haja wa kufanya hivyo.
 
Rip babu, ndo maana mtoto wa masumbuko anaitwa Roman naye ni mwanasheria. Mungu awatie nguvu wafiwa wote.
 
Ukimtaka huyu mtu nenda pale Mwananyamala Kisiwani ukamvizie siku nzima, haiwezi kupita wiki hajapita
 
Alikuwa noma km Lisu bungeni, wakambana sana.
Alitimuliwa kufundisha UDSM, kisha wakamzuia ku practice uwakili.
Njaa ikazidi, akarejea gambani na kupewa ubunge wa viti maalumu na Rais Mkapa.
Kuna kipindi nilisikia ni mwanasheria wa CCM.
ni moja ya kumbukumbu ya utawala wa kiimla wa BWM ambao umelifikisha taifa letu hapa kama tulivyo! kama kuna jambo ambalo siku zote nitamheshimu JK ni kuacha demokrasia ikue licha ya upinzani mkali toka kwa wahafadhina ndani ya chama chake wanaotaka chama chao kisiruhusu uhuru wowote wa maoni na demokrasia ya vyama vingi kusitawi!
 
Kwa wale wasiojua mchango wa Lamwai kweney Upinzani ni yeye aliesimama kidete kumtoa Gerezani Seif Sheriff Hamad aliekuwa katika kesi ya Nyaraka za siri .Lamwai musimhukumu wka yaliomkuta ni sawa sawa na Kasanga Tumbo. Muacheni Lamwai afunze vijana wengine watakaofuata Nyayo zake hapo Bongo.
I have alot of respect for him hata Dala dala yake ilifika wakati kukamatwa kila siku ili kumkomoa tu asipate kula yake , Lamwai alibakiwa na Leseni ya Uwakili Zanzibar tu Baada ya kufutiwa Leseni yake ya uwakili na pia kufutiwa nafasi yake ya uhadhiri pale Mlimani haya ndio majeraha ya Mkapa kwa wasiowajua . Tuwaulize Watanzania Jee Munamjua Balozi Nyaki na kwa nini alirudishwa Nyumbani Bongo kutoka Washington kwa AMri ya Mkapa kwa vile tu alimpokea Mrema Enzi hizo wakati Mrema alipokua NCCCR MAGEUZI. Maadui wote waliojijengea CCM ndio hao hao watakaoimaliza CCM .
 
naona pamoja na kuwa chama cha mafisadi wanambana kweli, wamemgaia eskudo wakati wao wakiendesha ma-vogue...!


huyu jamaaalikuwa madhubuti sana ila baada ya kupata kichapo cha ukweli toka kwa mafisi wa ccm alishindwa kuvumilia na kuamua kurudi misri lakini hadi leo hii jamaa ccm haiko moyoni muwalize wanafunzi wake wa sheria kule tumaini watawambia na kiukweli enzi zake game ilikuwa tight sana kwa wapinzani si mnaona kina cheyo wamebakia wapinzani jina tu saivi na mwenzake mrema
 
Masumbuko ni lecturer tumain university kanifundisha criminal law,he is a gud guy,
 
Mwaka 1994 akiwa NCCR Mageuzi tulimchagua kuwa Diwani kata ya Manzese, na hapo ndipo alianza kujulikana zaidi mitaani. Mwaka 1995 akiwa aligombea ubunge jimbo la Ubungo na alikuwa ameshinda pamoja na wenzake wa NCCR katika majimbo yote ya DSM lakini uchaguzi huo ulifutwa saa nane ya usiku baada ya tume kuona kuwa dsm yote imechukuliwa na upinzani.
Kwa kuwa NCCR haikuridhika na uchaguzi tanzania nzima, iliamua kujitoa, ila kisheria haikuwezekana. Wagombea wengine wote wa NCCR walitangaza kususia uchaguzi wa marudio dsm, lakini Lamwai alikataa na kushiriki; na tulimchagua kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Matokeo hayo yalipingwa mahakamani na Lamwai akashindwa kesi; na huo ukawa mwanzo wa mporomoko wake.
Baada ya hapo alifutiwa ualimu wa udsm na pia serikali ilimfutia leseni yake ya uwakili wa kujitegemea. Lamwai akadhoofu na akawa hana budi kujisalimisha kwa CCM. Ndipo Mkapa alimteua kuwa mbunge.
Kitendo cha Lamwai kurudi CCM na kuteuliwa na mkapa, kilimshushia heshima katika jamii - kama mchangiaji mmoja alivyosema 'siamini kama mtu aliyekuwa anaikandia sana ccm angeweza kurudi huko'. Wengi tulimwona kama mtu aliyekosa uvumilivu na ujasiri wa kundelea kuwa upinzani - alitusaliti. Kwa kuwa JK hakumteua tena kuwa mbunge; ikawa ndio mwisho wake katika siasa. Hana tofauti na Kabourou wa Kigoma

Kumbukumbu mzuri sana hiiii....... bado una data kichwani ziko sawa kabisa
 
Huyo mkapa pamoja na kuza viwanda vyetu, ebu tuweke mabaya yake hasa ya judhoofisha upinzani
 
Poa sasa nimefahamu, lakini hawa jamaa sometimes wanatuchezea akili, siamini jinsi alivyokuwa anaikandia CCM, ati leo hii naye kesha kuwa mwanasheria wao. Kweli siasa ni MCHEZO MCHAFU!

Ulikuwa huji? na wala usije kushangaa siku moja Slaa au Zitto wapo CCM wanakula Vinono! hiyo ndio siasa! unatakiwa uende kwa mwendo pole na kamwe si mwendo kasi unaweza kujikwaa na usipate wa kukunyanyua ....
 
Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?mbona hasikiki ...
MWENYE HABARI ZAIDI JUU YAKE AZIMWAGE HAPAJAMVINI...
 
Lamwai ni nasikia ni mwanasheria wa CCM. Pia kwa sasa anafundisha somo la sheria katika vyuo mbambali. Mwaka 2010 nilimuona Tumaini University kituo cha Kurasini.

Hana jipya zaidi ya kuishiwa kila alichokuwa nacho alipokuwa NCCR. Hilo ndo kosa la watu wengi katika siasa kurudi CCM.
 
aliingizwa mjini na akajitosa katika bahari ya mawe! kaumia sana , sasa hivi hana lake tena!
 
pima mwenyewe na uone hapo kuwa huyu ni Dr. (PhD) na kapotea hivi then uniambie miaka mitatu ijayo hawa wafuatao itakuwaje:
  • Shonza
  • Mwampamba
  • Tambwe Hiza
  • Kabouru
  • Shitambala
...
...
\ongeza wa kwenu pia
 
Back
Top Bottom