Yondani Mchezaji bora 2012/2013

Baraka F.K

Member
Aug 28, 2012
79
26
Mlinzi wa kati timu ya Yanga Kelvin Yondani ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mpira wa miguu nchini kwa msimu wa 2012/13 na kiasi cha pesa mil 5 katika sherehe iliyofanyika jana usiku katika hotel ya Double Tree.

Kipre Tchetche ameibuka na tuzo ya mfungaji bora kwa msimu na kiasi cha mil 5, huku mlinda mlando wa Priso David Burhan akishinda tuzo ya golikipa bora na kiasi cha mil 5.

Abdallah Kibadeni ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka na kitita cha mil 7.5:

Yanga imekabidhiwa kitita cha mil 70 kama bingwa wa Ligi Kuu, huku Azam ikipewa mil 35 kwa kuwa mshindi wa pili na Simba mil 25 kwa kuwa mshindi wa tatu.

Wengine ni
1.Full Maganga - Mgambo JKT mchezaji mwenye nidhamu
2.Simon Mberwa - Refarii bora mil 7.5
3. Abdulman Musa U-20 Ruvu shooting - Chipukizi mil 1.
4. Hassan Dilunga U-20 Ruvu - Chipukizi mil 1.
5. Chande Magoja - Mgambo jkt U-20 -Chipukizi mil 1.
6. Tony Kavishe Mgambo U-20 Chipukizi mil 1.
7. Hamis Saleh JKT Oljoro U-20 Chipukizi mil 1.
8. Rajab Zahir Mtibwa Sugar U-20 mil 1.
9. Timu yenye nidhamu - Yanga mil 15

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Safi sana zawadi ziangaliwe upya na pia wawasaidie gharama za usafiri,malazi,vifaa vya mazoezi,matibabu kwa kila timu kupunguza utegemezi wa milangoni!hongera sana Vodacom!!
 
Timu yenye nidhamu yanga,. Hahahaaaa izrael mkongo umeona aibu yako, mwaka jana ulutuaribia vijana wetu wenye nizam wakakupa mkong'oto
 
Safi sana zawadi ziangaliwe upya na pia wawasaidie gharama za usafiri,malazi,vifaa vya mazoezi,matibabu kwa kila timu kupunguza utegemezi wa milangoni!hongera sana Vodacom!!

kweli aisee, hizo zawadi ni kiduchu mno!
 
Goalkeeper wa Prison inawezekana kabisa , Prison ilikuwa na ukuta imara sana, ila foward ilikuwa butu, atakuwa alifungwa goli chache, Simba na Yanga hazitengenezi chipukizi wote wametoka timu zisizodhaniwa
 
Soka limekua....ila usikimbilie kusema Simba na Yanga hawatengenezi Chipukizi, we unafikili Seleman Matola na Amri Saidi wanafanya nini na kikosi cha Simba B alikadhalika na upande wa Yanga.....pia angalia usajiri wa Simba msimu huu jinsi ulivyo; acha blah blah bwana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom