Yathibitika: Wenye mihemko ya kupenda sana ngono wataalamu wabaini si hiyari yao…!

amygdala.jpg

Eneo hili linahusika sana....
86534785-660x450.jpg

Wataalamu nchini Ufaransa wamesema kwamba, hatimaye wamebaini, sehemu ya ubongo inayowapeleka watu puta wanapompenda mtu kimapenzi na kuwa kama vichaa. Wamesema eneo la ubongo linalofahamika kama amydala, ndilo linalohusika.

Wamebainisha kwamba, kwa kadiri eneo hilo linavyokuwa kubwa ndivyo ambavyo mtu anavutwa kimapenzi haraka na kwa mshawasha mkubwa zaidi. Hii ina maana kwamba, wale wanaosukumwa kupenda haraka na kuwehushwa na kupenda, siyo hiyari yao, bali ni namna tu ubongo wao ulivyotengenezwa.

Eneo hili la ubongo huchokozeka haraka zaidi kuliko eneo lingine, pale mtu anapoingia katika kumpenda mtu. Kabla ya ugunduzi huu, eneo hilo la ubongo lilikuwa likifahamika kwa kazi yake ya kuwafanya wanyama kuvutana kwa lengo la kupandana.

Kwa hiyo hamu au kiwango cha kusukumwa mtu kufanya mapenzi , au kuvutika kimapenzi, kinategemea pia pamoja na mambo mengine, ‘saizi’ ya eneo hilo la ubongo.

Kwa hiyo kwa wale waliokuwa wakishangazwa na baadhi ya wanaume au wanawake wenye tabia ya kupenda sana ngono na kuwa kama vichaa kutokana na kupenda huko naamini sasa wamepata jibu kwamba si kulogwa bali ni tatizo la kwenye ubongo.

kumbe ndio maana suzy wa sinza huwa ananisumbua mbaya..
 
Last edited by a moderator:
nakubaliana na wee Neylu, kumbuka wapo watu ambao hawana matamanio kabisa ya kufanya ngono na hata wakifanya hawahisi chochote, hayo ni matokeo ya kuwa na Amygdala ndogo sana ambayo haimudu kuchochea hisia za kungonoka....

Acheni mbwembwe nyie. Mambo ya ubongo mapana na sana. Huwezi ku-conclude mambo kirahisi hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi baba mie kidogo sijaelewa. Huyo amydala yeye anawafanya watu kupenda na kuwehuka kimapenzi right? Sasa hii inahusianaje na kupenda sana ngono? Kwa sababu naelewa kuwa kupenda na ngono havina mahusiano yaliyo nyoofu meaning mtu anawezafanya ngono pasipompenda muhusika. Hii kupenda sana na kuwehuka kimapenzi si inamaanisha kuwa deep in love na kudata kimapenzi au? Yaani mfano MwanajamiiOne amempenda naniliu, na kwa kuwa MwanajamiiOne anayo amydala kubwa basi MwanajamiiOne amekufa, ameoza, amedata kwa naniliu. Sioni nafasi ya kupenda ngono na mahusiano na amydala au ndo tuchukulie inavyofanya kazi kwa wanyama. (Nahisi nitahitaji uniandikie kilugha baba)
 
Last edited by a moderator:
hivii, hiyo amagydalena huwa inaongezeka na kupungua kutokana na mzunguko wa mwezi wa wanawake au?????
maana kwetu au kwangu mimi hamu inakuwa kubwa kipindi fulani tu cha mzunguko.

Swali zuri sana.
Hicho kipindi kipo.
Kwa wanyama tuna sema yupo kwenye "heat".
Ndio maana nikasema watu waache mbwembwe.
 
This field is too broad to conclude a thing. Hao wanasema "yathibitika" wajipange.
.....yah mkuu ndo mana kwenye matibabu kuna kitu kinaitawa differential diagnosis and definitive diagnosis.....yaani dalili moja ya ugonjwa (au hali yoyote mwilini) inaweza kusababishwa na ugonjwa mmoja au zaidi....mfano homa(fever) inaweza kuletwa na typhoid au malaria kwa hiyo ukifanya kipimo ndo unapata ...definitive diagnosis yaani diagnosis ya mwisho.....the same to hypersexuality pia.....mtu anaweza kuawa na MANIA lakini kwaida usijue sisi tunasema ni pepo la ngono/au anapenda ngono....
 
Mtambuzi baba mie kidogo sijaelewa. Huyo amydala yeye anawafanya watu kupenda na kuwehuka kimapenzi right? Sasa hii inahusianaje na kupenda sana ngono? Kwa sababu naelewa kuwa kupenda na ngono havina mahusiano yaliyo nyoofu meaning mtu anawezafanya ngono pasipompenda muhusika. Hii kupenda sana na kuwehuka kimapenzi si inamaanisha kuwa deep in love na kudata kimapenzi au? Yaani mfano MwanajamiiOne amempenda naniliu, na kwa kuwa MwanajamiiOne anayo amydala kubwa basi MwanajamiiOne amekufa, ameoza, amedata kwa naniliu. Sioni nafasi ya kupenda ngono na mahusiano na amydala au ndo tuchukulie inavyofanya kazi kwa wanyama. (Nahisi nitahitaji uniandikie kilugha baba)
Mwanangu MwanajamiiOne mbona swali lako limejibiwa katika kile nilichoeleza, hebu soma vizuri hapa chini:

amygdala.jpg

Eneo hili linahusika sana....

Kwa hiyo hamu au kiwango cha kusukumwa mtu kufanya mapenzi , au kuvutika kimapenzi, kinategemea pia pamoja na mambo mengine, ‘saizi' ya eneo hilo la ubongo.

Kwa hiyo kwa wale waliokuwa wakishangazwa na baadhi ya wanaume au wanawake wenye tabia ya kupenda sana ngono na kuwa kama vichaa kutokana na kupenda huko naamini sasa wamepata jibu kwamba si kulogwa bali ni tatizo la kwenye ubongo.
 
Last edited by a moderator:
.....yah mkuu ndo mana kwenye matibabu kuna kitu kinaitawa differential diagnosis and definitive diagnosis.....yaani dalili moja ya ugonjwa (au hali yoyote mwilini) inaweza kusababishwa na ugonjwa mmoja au zaidi....mfano homa(fever) inaweza kuletwa na typhoid au malaria kwa hiyo ukifanya kipimo ndo unapata ...definitive diagnosis yaani diagnosis ya mwisho.....the same to hypersexuality pia.....mtu anaweza kuawa na MANIA lakini kwaida usijue sisi tunasema ni pepo la ngono/au anapenda ngono....
Dr. Mo, nimeshasema pamoja na mambo mengine lakini hilo la size ya Amygdala linachangia, au hukusoma nilichoandika?

Back
Top Bottom