Yanga yageuza changamoto ya marefa wa Tanzania kama fursa.

Baba Kiki

JF-Expert Member
May 31, 2012
1,544
940
Katika somo la ujasiriamali, kuna dhana maarufu ya kugeuza changamoto kuwa fursa ya kujiletea maendeleo. Inashauriwa kuwa wakati wengine wakiendelea kulalamika na mazingira magumu au yanayowakwaza katika kutimiza malengo yao, mjasiriamali halisi hutumia mazingira hayo hayo na changamoto zake na kuzigeuza kuwa fursa.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa Yanga, ambayo timu nyingi za kibongo zikiendelea kulalamikia waamuzi wenyewe washaacha huo mchezo na badala yake wametumia uzembe au ubovu wa waamuzi kujipatia pointi hasa pale inapoonekana mechi ni ngumu na matokeo yanahitajika kwa namna yoyote. Mara ya mwisho Yanga kuwa na mabifu makubwa na kuonja na kuumizwa na chungu ya marefa ilitokea Machi 10, 2012 pale kati ya mechi yao na Azam walipolala 3-1 ambapo walipomgeuza mwamuzi Israel Nkongo kuwa punching box, na tangu madhila yale, wamejua vizuri kutumia fursa.

Hakuna shaka kuwa klabu ya soka ya Yanga imekuwa kinara wa kutumia vizuri maamuzi mabovu kwa kile kinachoitwa uwezo mdogo wa waamuzi wa soka Tanzania ambapo 'uwezo' huu mdogo wa waamuzi hawa umekuwa ukitumiwa na Yanga kama fursa muhimu ya kujipatia matokeo, ambapo zimekuwa zikiisha kwa malalamiko kutoka timu ambazo zimekuwa pinzani kwa Yanga.

Katika mechi za mwaka jana, Yanga inakumbukwa zaidi kwa matukio ya kadi nyekundu na penati katika mechi kama tano hivi zilizokuwa ngumu, na mara baada ya kadi hizo, Yanga iliweza kutumia vizuri nafasi na kujipatia matokeo mazuri. Mifano kwa ufupi ni kama malalamiko ya Mwadui, Coastal Union, Mbeya City, Simba na Azam hasa baada ya goli halali la Kapombe kukataliwa na kuinyima ushindi Azam badala yake kuwa sare ya 2-2, utagundua kuwa Yanga huwa hawapigi kelele na marefa, yenyewe refa "akijichanganya kidogo", inaadhibu tu.

 
Back
Top Bottom