Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,235
103,869
KUNA wakati huwa hatupendi ukweli. Tunapenda kudanganyana kwa sababu tu ya ushabiki. Ni kama hili la Simba na Yanga kimataifa.

Nimeona tambo za Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Wanatamba kuwa watafanya vizuri na kufika mbali.

Wanatamba kuwa wao ni bora kuliko timu yoyote nchini kwa sasa. Ni kweli. Matokeo ya Ligi ya ndani yanaonyesha hilo. Ni wazi kuwa Yanga iko katika kilele cha ubora wao.
Tangu msimu uliopita mpaka sasa wamepoteza mechi moja tu ya ligi. Ni rekodi bora sana. Hakuna timu nchini imewahi kufanya hivyo.

Yanga imekuwa vyema sana ndani na nje ya uwanja. Haipotezi mechi kizembe. Ni ngumu kutabiri inapoteza mchezo lini. Inapendeza sana.

Lakini ukweli ni kwamba pamoja na uimara ilionao Yanga sasa bado ina mengi ya kujifunza katika michuano ya kimataifa.

Huku kwenye mechi za CAF, Simba ina dunia yake. Imejenga ufalme ambao hautikisiki kirahisi.

Ilianza ikiwa hovyo lakini imekwenda ikiimarika siku hadi siku. Sasa wamekuwa wababe hasa wakiwa nyumbani.

Baada ya miaka 15 bila kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, miaka hii mitano iliyopita imebadilisha kila kitu.

Ilionekana kama imebahatisha ilipofuzu robo fainali mwaka 2019. Ni kweli haikuwa na timu imara sana kama sasa. Lakini ilikuwa na hesabu kali.

Pamoja na kufungwa 5-0 na AS Vita pale Kinshasa. Ikapigwa tena kipigo kama hicho na Al Ahly pale Cairo. Bado Simba iliweza kupenya. Iliweka hesabu kali na mipango ya kushinda nyumbani.

Leo hii Simba ni kati ya Timu 10 bora Afrika. Unajua Simba Sc inaelekea wapi. Kituo kinachofuata ni kunyakua kombe la kulitua juu ya mlima Kilimanjaro-Visit Tanzania. Kuna baadhi huleta dhihaka kwamba Simba imechukua kombe gani Afrika?!! Ni kweli hajachukua lakini ni nani anayeweza kutoka 1 ghafla akafika 10 bila kupita 2 na 3? Kwa hiyo Yanga wanayo ya kujifunza zaidi ya mengi ambayo mpaka sasa wamejifunza.

Kwanza kabisa wameingia kwenye kuendesha timu kiuwekezaji kama ilivyofanya Simba Sc na Mo Dewji. Hatimaye GSM amewekeza Yanga na matunda yameanza kuonekana. Pili wamekuwa na msukumo wa kuhakikisha wanatumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata matokeo. Hii ndiyo ile Simba wanaita Kwa Mkapa hatoki mtu.

Leo hii katika point 46.5 za Tanzania CAF Simba ina point 39 na Yanga ina 10 pekee. Nasema izidishe bidii kujifunza ili kuvuna point nyingi zaidi na kufika viwango vya Simba Sc. Ikazane kwa sababu wote walikuwa ligi ya mabigwa Afrika lakini Simba anakuwa mkiwa bila mdogo wake Yanga ambaye hatimaye amedondokea Kombe la Shirikisho.

My Take
Wivu wa maendeleo ni jambo jema, ila wivu wa chuki ni dhambi itakufa kifo kibaya
 
Mpira una njia zake ikiwemo, kuwa na uongozi imara na bora, kuwa na pesa ya kutosha kufanya uwekezaji wa benchi la ufundi bora na wachezaji bora na kuwa na mipango na mikakati bora kufikia mafanikio.

Yanga ipo kwenye mfumo wa kujijenga kuwa sehemu ya timu zenye history kubwa Africa. Sio kwa kuongeleka kuwa timu inayofunga vigogo halafu kombe haubebi, sio timu inayoongeleka kufika robo fainali, sio timu ya kuongeleka kuwa inatoa wachezaji wa magoli makali ya wiiki au wachezaji bora wa wiki. Hapana bali kuwa timu iliyobeba ubingwa wa CAFCC au CAFCL.

Nyie mliona hadi sasa mna mafanikio basi endelea kushangilia aina ya mafanikio mnayoyaona mnastahili.

focus ya Yanga ni makombe sio kuishia njiani na kujisifu. Na kama swala la kujifunza basi Yanga inajifunza kwa waliofika mwisho wa safari kuwa wamewezaje kufika pamoja na vikwazo vyote vya njiani, sasa aliyeishia njiani atakufundisha nini ilihali na yeye safari imemshinda japo kasogea tu hatua kadhaa. Tutajifunza kwa waliobeba makombe.
 
KUNA wakati huwa hatupendi ukweli. Tunapenda kudanganyana kwa sababu tu ya ushabiki. Ni kama hili la Simba na Yanga kimataifa.

Nimeona tambo za Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Wanatamba kuwa watafanya vizuri na kufika mbali.

Wanatamba kuwa wao ni bora kuliko timu yoyote nchini kwa sasa. Ni kweli. Matokeo ya Ligi ya ndani yanaonyesha hilo. Ni wazi kuwa Yanga iko katika kilele cha ubora wao.
Tangu msimu uliopita mpaka sasa wamepoteza mechi moja tu ya ligi. Ni rekodi bora sana. Hakuna timu nchini imewahi kufanya hivyo.

Yanga imekuwa vyema sana ndani na nje ya uwanja. Haipotezi mechi kizembe. Ni ngumu kutabiri inapoteza mchezo lini. Inapendeza sana.

Lakini ukweli ni kwamba pamoja na uimara ilionao Yanga sasa bado ina mengi ya kujifunza katika michuano ya kimataifa.

Huku kwenye mechi za CAF, Simba ina dunia yake. Imejenga ufalme ambao hautikisiki kirahisi.

Ilianza ikiwa hovyo lakini imekwenda ikiimarika siku hadi siku. Sasa wamekuwa wababe hasa wakiwa nyumbani.

Baada ya miaka 15 bila kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, miaka hii mitano iliyopita imebadilisha kila kitu.

Ilionekana kama imebahatisha ilipofuzu robo fainali mwaka 2019. Ni kweli haikuwa na timu imara sana kama sasa. Lakini ilikuwa na hesabu kali.

Pamoja na kufungwa 5-0 na AS Vita pale Kinshasa. Ikapigwa tena kipigo kama hicho na Al Ahly pale Cairo. Bado Simba iliweza kupenya. Iliweka hesabu kali na mipango ya kushinda nyumbani.

Leo hii Simba ni kati ya Timu 10 bora Afrika. Unajua Simba Sc inaelekea wapi. Kituo kinachofuata ni kunyakua kombe la kulitua juu ya mlima Kilimanjaro-Visit Tanzania. Kuna baadhi huleta dhihaka kwamba Simba imechukua kombe gani Afrika?!! Ni kweli hajachukua lakini ni nani anayeweza kutoka 1 ghafla akafika 10 bila kupita 2 na 3? Kwa hiyo Yanga wanayo ya kujifunza zaidi ya mengi ambayo mpaka sasa wamejifunza.

Kwanza kabisa wameingia kwenye kuendesha timu kiuwekezaji kama ilivyofanya Simba Sc na Mo Dewji. Hatimaye GSM amewekeza Yanga na matunda yameanza kuonekana. Pili wamekuwa na msukumo wa kuhakikisha wanatumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata matokeo. Hii ndiyo ile Simba wanaita Kwa Mkapa hatoki mtu.

Leo hii katika point 46.5 za Tanzania CAF Simba ina point 39 na Yanga ina 10 pekee. Nasema izidishe bidii kujifunza ili kuvuna point nyingi zaidi na kufika viwango vya Simba Sc. Ikazane kwa sababu wote walikuwa ligi ya mabigwa Afrika lakini Simba anakuwa mkiwa bila mdogo wake Yanga ambaye hatimaye amedondokea Kombe la Shirikisho.

My Take
Wivu wa maendeleo ni jambo jema, ila wivu wa chuki ni dhambi itakufa kifo kibaya
1. Makolokolo wameingia kiuwekezaji wa kampuni na Mo tangu 2015.

MAFANIKIO YA SIMBA:

Kutinga robo fainali za CAFCL mara 3 na robo fainali ya CAFCC mara 1 ndani ya miaka 7.

2. Yanga FC wameingia kiuwekezaji wa kampuni ya GSM 2021.

MAFANIKIO YA YANGA:

Kutinga robo fainali ya CAFCC baada ya mwaka mmoja na nusu tu.

Je kati ya Simba FC na Yanga FC ni klabu ipi inapaswa iige mfano kwa klabu nyingine kiuwekezaji na kimaendeleo?
 
Yanga ni club iliyoanzishwa na waswahili yani wale macheki bob wa miaka hiyo, so hata inavyo operate kila kitu kinafanywa kijadi zaidi.

Simba ni timu iliyoanzishwa na wazungu na wote tunafahamu mzungu hajawahi kuwa na ambitions za kishamba.

Na ndio maana unaona hata baada ya kutanguliwa na Yanga kama klabu ya kwanza kuanzishwa lakini bado Simba ndio iliyokuwa timu ya kwanza kuwa updated kufanya mambo kisasa ikiwemo kucheza mpira wakiwa wamevaa viatu nk.

Simba ndio Club ya kwanza kufanya biggest achievement katika kila carrier

Kwahiyo mi nashangazwa na watu wanaoshangazwa na happiness level waliyofikia Yanga baada ya kufika robo.

Mnashangaa furaha yao yao katika hili? Hawa waliwahi kufanya biggest party the first day walipoanza kuvaa viatu...sasa sembuse robo ya CAF CC tena ya 30 anniversary??

NB: Nasikitika kuwa sijaeleweka
 
Tunajifunza kwa wanaojua na wanao tumia sayansi ya mpira kupata ushindi kama Mamelodi,Aly Ahly,Esperence nk ni si kama hawa .
images (38).jpeg

Mara waote moto ,mara Kinyume nyume.
 
Acha porojo, Mpira ni uwekezaji na kupata wataalamu sahihi. Kilichokua kinawakwamisha Yanga ni fedha ambayo itakuwezesha kupata watu sahihi wenye uwezo wa kutafsiti mipango ya Taasisi.

Kwasasa Yanga Wana fedha kiasi na imepata watu sahihi ndiomaama wapo vizuri.
Usifikiri Yanga inapata matokeo Kwa kubahatisha, Iliwagharimu kuwekeza fedha Kwa kuwatafuta Laliga na Sevilla katika plani zao na mpaka Sasa wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ughaibuni.

Yanga hawaitaji kujifunza chochote Kwa Simba kwakua njia zote walizokua wakitumia Simba kupata matokeo hazifai Kwa mpira wa kisasa.
Simba wamekua wakitumia njia chafu za mkato Ili wajifurahishe na vilabu vingi vilikua vikilalamika namna mambo yanavyo fanyika wakiwa hapa Kwa Mkapa.

Mwishowake Simba wali umbuliwa na CAF Kwa kupigwa faini kutokana na vitendo vya kishirikina na tabia chafu katika mpira wa miguu.
Yanga imechagua kuwekeza katika wataalamu wa soka na mbinu za kisasa kupata matokeo.
Yanga walisha vuka izo hatua za kulazimisha matokeo Kwa njia chafu za kupuliza madawa na Ulozi wa kiwango Cha CAF.
Yanga itafanikiwa mapema kwakua inapitia njia sahihi ila gharama zake ni fedha katika wataalamu.
 
Unasema hamtaki njia za mkato wakati mmebeba kikosi kizima cha AS Vita na kukihamishia hapa?
 
Yanga ni club iliyoanzishwa na waswahili yani wale macheki bob wa miaka hiyo, so hata inavyo operate kila kitu kinafanywa kijadi zaidi.

Simba ni timu iliyoanzishwa na wazungu na wote tunafahamu mzungu hajawahi kuwa na ambitions za kishamba.

Na ndio maana unaona hata baada ya kutanguliwa na Yanga kama klabu ya kwanza kuanzishwa lakini bado Simba ndio iliyokuwa timu ya kwanza kuwa updated kufanya mambo kisasa ikiwemo kucheza mpira wakiwa wamevaa viatu nk.

Simba ndio Club ya kwanza kufanya biggest achievement katika kila carrier

Kwahiyo mi nashangazwa na watu wanaoshangazwa na happiness level waliyofikia Yanga baada ya kufika robo.

Mnashangaa furaha yao yao katika hili? Hawa waliwahi kufanya biggest party the first day walipoanza kuvaa viatu...sasa sembuse robo ya CAF CC tena ya 30 anniversary??

NB: Nasikitika kuwa sijaeleweka
Una mental slavery kuamini kila kitu cha wazungu ni bora labda niku ulize pale Simba mzungu ni nani? Try again?
 
Watu ujifunza Kwa walio fanikiwa hajalishi mzungu au mwafrika, Yanga imejifunza kwa Laliga na Sevilla utaalamu wa kisayansi jinsi soka linavyo endeshwa. Kwasasa wanatafuta mtaji wa wanachama na Mashabiki zote izo ni njia za kitaalamu kupelekea kujitegemea.
Sasa Yanga wajifunze Nini Kwa Simba, Kuwasha moto uwanjani, kupuliza madawa vyumbani au kutoa makafara na kufukia uwanjani!!
 
Ujinga ni mzigo unaweza kuiga kwa timu isiyo na miundo mbinu ya michezo?, Kipi Cha maana ukichoonesha kinapaswa kuigwa kutoka kwa Simba?. Matokeo ya mpira ni ya muda ambao hata ihefu au Namungo anaweza kuyapata.
Ungeolodhesha yanga aige nini kutoka kwa Simba kwanza kabla ya kuota ndoto ya kuchukua CAF cup wakati timu haina uwezo hata wa kuvunja mkataba wa mchezaji mwenye thamani ya 400m, uchukue ubingwa wa CAF na akina Baleke au Kanoute?

Platinum member hovyooo kabisa 😅
 
KUNA wakati huwa hatupendi ukweli. Tunapenda kudanganyana kwa sababu tu ya ushabiki. Ni kama hili la Simba na Yanga kimataifa.

Nimeona tambo za Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Wanatamba kuwa watafanya vizuri na kufika mbali.

Wanatamba kuwa wao ni bora kuliko timu yoyote nchini kwa sasa. Ni kweli. Matokeo ya Ligi ya ndani yanaonyesha hilo. Ni wazi kuwa Yanga iko katika kilele cha ubora wao.
Tangu msimu uliopita mpaka sasa wamepoteza mechi moja tu ya ligi. Ni rekodi bora sana. Hakuna timu nchini imewahi kufanya hivyo.

Yanga imekuwa vyema sana ndani na nje ya uwanja. Haipotezi mechi kizembe. Ni ngumu kutabiri inapoteza mchezo lini. Inapendeza sana.

Lakini ukweli ni kwamba pamoja na uimara ilionao Yanga sasa bado ina mengi ya kujifunza katika michuano ya kimataifa.

Huku kwenye mechi za CAF, Simba ina dunia yake. Imejenga ufalme ambao hautikisiki kirahisi.

Ilianza ikiwa hovyo lakini imekwenda ikiimarika siku hadi siku. Sasa wamekuwa wababe hasa wakiwa nyumbani.

Baada ya miaka 15 bila kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, miaka hii mitano iliyopita imebadilisha kila kitu.

Ilionekana kama imebahatisha ilipofuzu robo fainali mwaka 2019. Ni kweli haikuwa na timu imara sana kama sasa. Lakini ilikuwa na hesabu kali.

Pamoja na kufungwa 5-0 na AS Vita pale Kinshasa. Ikapigwa tena kipigo kama hicho na Al Ahly pale Cairo. Bado Simba iliweza kupenya. Iliweka hesabu kali na mipango ya kushinda nyumbani.

Leo hii Simba ni kati ya Timu 10 bora Afrika. Unajua Simba Sc inaelekea wapi. Kituo kinachofuata ni kunyakua kombe la kulitua juu ya mlima Kilimanjaro-Visit Tanzania. Kuna baadhi huleta dhihaka kwamba Simba imechukua kombe gani Afrika?!! Ni kweli hajachukua lakini ni nani anayeweza kutoka 1 ghafla akafika 10 bila kupita 2 na 3? Kwa hiyo Yanga wanayo ya kujifunza zaidi ya mengi ambayo mpaka sasa wamejifunza.

Kwanza kabisa wameingia kwenye kuendesha timu kiuwekezaji kama ilivyofanya Simba Sc na Mo Dewji. Hatimaye GSM amewekeza Yanga na matunda yameanza kuonekana. Pili wamekuwa na msukumo wa kuhakikisha wanatumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata matokeo. Hii ndiyo ile Simba wanaita Kwa Mkapa hatoki mtu.

Leo hii katika point 46.5 za Tanzania CAF Simba ina point 39 na Yanga ina 10 pekee. Nasema izidishe bidii kujifunza ili kuvuna point nyingi zaidi na kufika viwango vya Simba Sc. Ikazane kwa sababu wote walikuwa ligi ya mabigwa Afrika lakini Simba anakuwa mkiwa bila mdogo wake Yanga ambaye hatimaye amedondokea Kombe la Shirikisho.

My Take
Wivu wa maendeleo ni jambo jema, ila wivu wa chuki ni dhambi itakufa kifo kibaya
Kweli Yanga inahitaji kujifunza,sasa tueleze mlifanya fanya vipi mpaka mkapata access ya kuingia na kuni katikati ya uwanja mpaka mkafanikiwa kuwasha moto kule South Africa?
 
Kwani shortcut lazima iwe kinyume cha sheria? Tunaongelea njia za mkato.
Njia za mkato tumeiba? si tumetumia hela zetu,nyie Mudy katoa 1.5b msimu uliopita mnawaleta watu wa ajabu ajabu,mara Okwa,Okra siju Sawadogo.

Sisi tunatumia hela yetu na tuna sajili kwa kufuata ataratibu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom