Yanga ilikuwaje wakaitwa Kandambili na Pan Africa wakaitwa Raizoni?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,954
Mpaka leo wachora katuni hutumia picha ya Kandambili kuwakilisha timu ya Yanga. Nakumbuka ni utani kati ya Yanga na Pan African, ndiyo ulileta jina la Kandambili Yanga na Raizoni Pan African.

Raizoni ndiyo vilikuwa viatu vya maana sana zama hizo, na Kandamimbili zilikuwa zinavaliwa na watu maskini na hohe hahe. Ni kwa nini Yanga huwa inapewa majina ya kuonesha kuwa wao ni watu wa Makasiriko??
 
Me sijui ila subiri waje wakina kaka Mshana Jr watupe history kdg
 
1667310350708.png

RAIZONI

1667310398257.png

KANDAMBILI
 
Kuna dhana mbili. Moja ni kuwa mashbiki wa Yanga huvua kandambili zao na kuzishika mkononi wakisukuma basi lao kutoka Karume au taifa mpaka Jangwani. Wakawa wanaitwa kandambili.

Dhana ya pili, ni wakati wa mgawanyiko, Kina Shiraz na Mangara wakawa wanawaambia wachezaji waliobaki na Tambwe Leya kuwa achaneni na hao kandambili., jina walilokuwa Malo kabla ya mgawanyiko mje huku Raizoni.

Mashbiki wa Simba pia walikuwa wakijiita Raizoni.

Halafu Yanga hatuchukii tukiitwa kandambili. Tulipokea jina hilo with pride kutoka kwa wazee wetu. Nakumbuka tawi la Yanga mtaa wa Mkumba Temeke lilikuws linaitwa "Msichoke" na lilikuws na picha ya Kandambili kubwa tu ya kuchora kwenye ubao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom