Yanga Hatari!

Yeyote atakayepata matokeo ya wekundu wa msimbazi (Simba) na Prisons, atuwekee tafadhali.
 
Wekundu wa Msimbazi wameishinda Prisons 3-1. Wanakumbuka shuka asubuhi...

Hii ni kwa mujibu wa dullonet.com
 
Mimi ni Yanga tangu nina miaka kumi.
Lakini sasa kitendo cha pesa yetu kutumika kufadhili mpira hata kama ni kwa timu ninayoipenda kimeniudhi sana.
Yanga tutafute njia nyingine ya ku finance timu yetu.
Haya mambo ya kutegemea Maji kila siku atufadhili kwa kweli kinatudhalilisha.
Najua mwisho watatuita EPA haooooooooooo. Aibu hii tutaificha wapi?
 
Madega: Kipa mzungu sasa safi
Jessca Nangawe

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Imani Madega amesema kipa wa timu hiyo, Mserbia Obren Curkovich kwa sasa anaweza kushiriki Kombe la Shirikisho baada ya leseni yake kukamilika.


Obren ambaye anaichezea Yanga baada ya kusajiliwa akitokea nchini Serbia alikuwa katika hatihati ya kutoshiriki mashindano hayo baada ya leseni yake kuzuiwa na shirikisho la mpira la Afrika (CAF) baada ya kutaka maelekezo kama mchezaji huyo anaichezea Yanga kihalali na ITC inatambulika.


Akizungumza na Mwananchi jana, Madega alisema tayari wamekamilisha maelekezo yote kwa shirikisho hilo na kwa sasa mchezaji huyo yuko huru kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.


"Kikubwa ambacho tulikua hatujakamilisha kwa golikipa huyu ni vivuli vya hati yake ya uhamisho ambapo CAF walikua wakihitaji lakini tayari tumefanya mazungumza na chama cha soka nchini Serbia na tumeshamalizana na tatizo hilo," alisema Madega.


Yanga itapambana na Wacomoro hao ikiwa ni mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Naye kocha wa Yanga Dusan Kondic amejipa matumaini ya kuibuka na ushindi mnono kutokana na maandalizi ya timu yake ingawa amedai mchezo utakuwa mgumu kutokana na timu zote kutokuwa na historia na timu pinzani.

My Take: Ina Maana Jamaa ameshiriki mechi za ligi kuu bila yakuwa amekamilisha uhamisho wake wa Kimataifa!
 
Ina Maana Jamaa ameshiriki mechi za ligi kuu bila yakuwa amekamilisha uhamisho wake wa Kimataifa!
Mkubwa hizo ndio siasa za simba na yanga
 
Wenye matokeo ya Yanga(KAGODA FC) na Moro watupe update
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom