Yanayojiri mkutano wa taifa vijana, Dodoma...!

kwa hiyo wao walikubaliana kama chama kuwa rushwa itolewe na wanaume tu, hakujua kuwa ccm hakuna ubaguzi wa kijinsia na wanachama wote ni sawa!?? Acha kila mtu atoe sasa muone hata wamama ambao wamekuwa wakiwapeleka madarakani!
Pia niliona itv jana akielezea kwa undani kuwa viongozi wanaopatikana kwa rushwa ni 'DHAIFU'. Ngoja niitafute maana niliipenda sana
JK said:
"Nimeyasema haya ni lazima tufike mahali tutambue kuwa haya si mazuri na yanapohusisha mpaka wanawake, maana zamani nilidhani haya mambo ni ya wanaume tu, lakini sasa hadi wanawake ndio tena tumekwisha. Tunakoelekea sio kuzuri sana na kama hatutafanya jitihada ya makusudi kubadiliks, tupo hapa mtakuja kunieleza jinsi mtakavyoelekea kwenye shimo." Source: Nipashe
 
Zoezi la ugawaji wa vitabu vya maelezo binafsi ya wagombea ngazi ya Taifa limekamilika.,ambapo jumla ya wagombea 133 wa ngazi ya Taifa wamechukuliwa maelezo yao na kuelezwa ndani ya kitabu hicho.
 
Zoezi la UUchaguzi linatarajia kuanza hivi punde ambapo Msimamizi wa Uchaguzi Mhe. Lukuvi na msaidizi wake Mhe. Jennister Mhagama wanaendesha zoezi la kuwasimamia Kamati ya Utekelezaji kujiuzulu ili kupisha zoezi hilo liendelee kulingana na kanuni za umoja wa vijana na kanuni za uchaguzi ndani ya Chama.

Amekaribishwa Mwenyekiti wa Vijana Ndugu Malisa avunje kamati ya utekelezaji, nae amekaribisha wajumbe wa kamati yake ya utekelezaji waweze kushukuru na kusalimia ambapo ndugu suleyman kutoka zanzibar na Ndugu Zainab Kawawa waliwakilisha wajumbe wengine wa kamati hiyo...!
 
huo mkutano pekee una wajumbe wapatao 1300.achilia mbali wale waliopo ngazi za chini ambao wanaishia kwenye matawi kata na mashina.wewe peke ako ndio uko huko lakini vijana wenye akili timamu wapo ccm
hao vijana majority wakipimwa akili, wataonekana wana matatizo makubwa! TUFIAKWA!!!! kuliko niwe ccm, ni bora kuwa sina chama!! GOD FORBIDS!!
 
Mgombea wa kwanza nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa chama cha mapinduzi ndugu ABDALLA Lulu Mshamu. Ameanza kutoa maelezo yake ambapo mwisho wa maelezo amesema kuwa amejitoa kugombea nafasi hiyo na hivyo kuwaacha wagombea wawili tu katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti...!
 
Zoezi la upigaji kura linaendelea baada ya wagombea wote kujieleza kwa kina na wajumbe kuuliza maswali kwa wale waliodhani wanahitaji kuwauliza.,wajumbe wa arusha,dodoma, kigoma, kilimanjaro na wajumbe wa mikoa mingine wanaendelea kuunga foleni.
 
Huu msemo huwa una maana gani "kula CCM kura kwa CHADEMA"" hii kauli ya JK ni mwendelezo wa kauli za wanasiasa wetu zinazoonyesha kwamba wote wanafanana. Kama mtu anashindwa kuwaambia watu wake kwamba msichukue rushwa badala yake anasema chukueni rushwa lakini sisi tupeni kura, ni yale yale!!
 
Back
Top Bottom