Yanayojiri mkutano wa taifa vijana, Dodoma...!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mheshimiwa Rais atoa hotuba kali kwa vijana ambayo inalenga kuwajenga na kuwataka wafanye tathmini ya kutosha kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa ngazi ya Taifa ya Jumuiya hiyo ya Vijana.

Alianza kwa kuwakumbusha Ibara ya 5 ya katiba ya chama cha mapinduzi ambayo inaeleza MALENGO NA MADHUMUNI ya CCM.,ambapo imeelezwa kwenye ibara hiyo kuwa madhumuni ya CCM ni "kushinda katika uchaguzi wa serikali kuu na Mitaa"

Lakini pia akaeleza kuwa CCM kinategemea Jumuiya yake hii kufanya kazi ya siasa miongoni mwa vijana wa TANZANIA na kuwashawishi wakubali kuwa wanachama na wapenzi wa CCM. Akasisitiza kuwa matumaini makubwa ya msingi kuliko yote ya Chama Cha Mapinduzi ni kuona jumuiya yake hii inakuwa MKOMBOZI wa vijana.

Akawataka wahakikishe kuwa wanapata Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na viongozi wengine ambao wataongoza vyema,watakaoongoza juhudi za kuendeleza, kutetea na kulinda maslahi ya CCM. Viongozi wanaoijua na kuipenda jumuiya ya Vijana.

Na pia akawataka baada ya uchaguzi wajipange kutimiza wajibu wao kwa jumuiya yao na Chama kwa Ujumla..,

HOTUBA INAENDELEA....
Ndugu zangu mimi kama mwanaCCM nipo ndani ya huu mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya jumuiya hii ya chama lakini yanayotendeka humu ndani kwa kweli sikubaliani nayo na ndio mana hata CHADEMA wanapotusema nje ni vema tukawa waungwana na kukubali kuwa ni vema tukajaribu kubadilika lakini ni vigumu mana tunaendelea kuwahadaa watanzania kuwa tupo kuwatetea wao.

Mimi nipo ndani ya CCM hapa katika kikao hiki lakini siungi mkono vitendo vya rushwa vinavyoendelea kuitafuna CCM mpaka sasa ndio matokeo yanatangazwa ya washindi wa uchaguzi lakini ukweli ni kwamba wanatangazwa waliofanikiwa kutoa fedha na kuweza kuchaguliwa sasa hiki ni chama gani kama mpaka utoe fedha ndio uchaguliwe.

HUU NDIO UCHWARA UNAOENDELEA KUWAPA UMAARUFU WAPINZANI WETU PALE TUNAPOKUWA WAGUMU KUJIREKEBISHA.
HAPA NDIO MATOKEO YANAANZA KUTANGAZWA PUNDE NITAYAJUMUISHA HUMU ILA TUNASIKITISHWA MAANA BILA KUWA NA PESA HUWEZI ONGOZA UVCCM NA KWELI VIJANA TUMEONESHA MFANO MBOVU MANA TUMESHINDWA KUSHIKAMANA NA KUTETEA SWALA LA RUSHWA.

MATOKEO YA MWENYEKITI NI WIZI MTUPU MTU KWA SABABU ANAO UWEZO WA KUTOA PESA KATOA NA KAPITA DUUUUUUUUUUU NAUMIA HAPA KAMA NIMLUKIE LUKUVI MANA NDIO ANATANGAZA MATOKEO MANA NAPATA HASIRA SANA.
MWENYEKITI SADIFA MAKAMU MBONI MHITA HAYA NDIO MATOKEO YALIYOPANGWA NA WANAOJIITA VIGOGO WA CHAMA MIMI KWELI NASEMA KAMA TUNAHITAJI KWENDA MBELE NA CCM YETU VEMA TUBADILIKE .
 
Alianza kwa kuwakumbusha Ibara ya 5 ya katiba ya chama cha mapinduzi ambayo inaeleza MALENGO NA MADHUMUNI ya CCM.,ambapo imeelezwa kwenye ibara hiyo kuwa madhumuni ya CCM ni "kushinda katika uchaguzi wa serikali kuu na Mitaa"
Kushinda tu?.....Kushinda kivipi?......Na vipi kuwahudumia wananchi? Ndio maana alitoaahadi 100 za uwongo
 
hivi kuna vijana bado wapo ccm??? ni majanga TAIFANI mwetu!!

huo mkutano pekee una wajumbe wapatao 1300.achilia mbali wale waliopo ngazi za chini ambao wanaishia kwenye matawi kata na mashina.wewe peke ako ndio uko huko lakini vijana wenye akili timamu wapo ccm
 
Hizi ni moja ya kauli za Jakaya akiwahutubia UVCCM kule Dodoma.

Kuna watu wananipa updates ntakuwa nawapa.

Ila hii imenistua kidogo.

Hivi sheria inasemaje kuhusu anayetoa na kupokea Rushwa?

Tusemezane!
 
Mheshimiwa Rais pia ameeleza kuwa anafahamu kuwa uchaguzi huacha ufa na mpasuko miongoni mwa wanachama na hivyo kuwakumbusha viongozi na wanachama kuwa imara hata baada ya uchaguzi kwa kuziba nyufa na migawanyiko iliyotokana na uchaguzi. Na akawataka kuipa kipaumbele cha juu kazi hii ya kuziba nyufa ili wapate utulivu utakaowapa fursa ya kupanga mipango ya kujenga na kuimarisha jumuiya....
 
Hapo ni sawa na kumruhusu binti yako afanye ufuska ila asipewe mimba.Rushwa ni adui wa haki hairuhusiwi kutoa wala kupokea rushwa
 
huyo ni dhaifuuuu tutajuta sana mpaka kufika 2015 hakuna rangi tutaacha kuona,huyo jamaa ni sawa na boxi hana kitu kabisa tangu anasoma ni wa hovyohovyo tu, njaa zetu ndio zimetufikisha hapo........
 
Kama ni kweli kasema hivyo basi kazi ni kubwa kuliko tunavyofikiri! Rais anasahau kuwa yeye ndie anayemteua Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa. Anasahau hiyo taasisi inatakiwa kumsaidia kufanya nini kuhusu rushwa. Haoni ubaya wa rushwa. Haoni madhara ya kauli yake hiyo yaani watu wachukue tu rushwa ili mradi wasiwapigie kura waliotoa rushwa. Hajui kuwa kutoa na kupokea rushwa yote ni makosa. ..................Kazi ipo.
 
Pia mheshimiwa Rais amewaomba wawe na moyo wa ustahamilivu na ukomavu wa kisiasa. Amewataka wawe na moyo mpana wa kukubali matokeo.

Na pia amewaomba vijana na kuwataka watambue kuwa kugombea ni haki ya kila mwanachama wa jumuiya,kwa maana kila baada ya miaka mitano uchaguzi hufanyika, hivyo hakuna sababu ya kumchukia mwanachama aliyejitokeza kugombea.

Na pia akawaambia kuwa ikiwa watazingatia hayo watatoka kwenye uchaguzi huu wakiwa na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya ya kutimiza wajibu wa jumuiya na CCM.
 
huo mkutano pekee una wajumbe wapatao 1300.achilia mbali wale waliopo ngazi za chini ambao wanaishia kwenye matawi kata na mashina.wewe peke ako ndio uko huko lakini vijana wenye akili timamu wapo ccm

kumbe tanzania bado vijana vichaa wanafika hata1300
 
Mheshimiwa Rais wa Serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi..,Chama tawala na Chama Imara Tanzania amaliza hotuba yake kwa kuwaambia kuwa anaamini kuwa "RAIS WA TANZANIA MWAKA 2025 YUPO KWENYE UKUMBI HUU LEO HII"

Na hivi sasa anaelekea nje ya Ukumbi ambapo atapiga picha ya pamoja na wageni waalikwa kwa ajili ya ukumbusho na kisha ataendelea na majukumu yake mengine ya kuijenga na kiimarisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
sidhani kama ni suplaiz kwa watawala wetu kutoa kauli kama hizi, ila kwa nafasi ya huyu mkuu na kwa kuzingatia madhara ya hii vita ni kama kuendelea kuudhihirishia uma udhaifu wake (yale ya mnyika ndo yanatimia)
 
Nashauri Bunge lifutilie mbali sheria inayohusiana na TAKUKURU. Tuoke kila shilingi na TAKUKURU ni kielelezo cha matumizi mabaya ya fedha ya umma.
 
sidhani kama ni suplaiz kwa watawala wetu kutoa kauli kama hizi, ila kwa nafasi ya huyu mkuu na kwa kuzingatia madhara ya hii vita ni kama kuendelea kuudhihirishia uma udhaifu wake (yale ya mnyika ndo yanatimia)

kuna watu wengine wanatoa rushwa ya kunaniliuliwa. unafikiri ukimnaniliu vizuri atashindwa kukupigia kura!?
 
Back
Top Bottom