Yanayojiri Mikutano ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Magufuli mkoa wa Kigoma

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM upande wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Magufuli ameonja joto ya jiwe leo akiwa jimbo la Kigoma mjini, imethibitika.

Baada ya wasanii mbalimbali kutumbuiza kwenye jukwaa, wananchi walisikika wakisema kuwa wameshatosheka na tamasha na sasa wanaondoka zao. Walipoulizwa wanasema nini ndipo walipopaza sauti kuwa ni Zitto na Lowassa tosha huku wakipunga mikono kuhashiria kuaga.

Baada ya muda mfupi uwanja ulibaki na mashabiki walioambatana na Magufuli wakiwa wameketi jukwaa la mbele.

Hii ni mara ya nne kwa Magufuli kukataliwa hadharani baada ya kufanyiwa hivyo Njombe, Mbeya na Songea mjini.
Wewe sio ndiyo yule ilieleta propaganda kuwa Magufuli alimnadi Chenge wakati ni uongo.

Hizo propaganda za kipuuzi mkapigie huko mitaani humu wengi wanauelewa.
 
attachment.php

Hiyo ngazi ni ya matofali yamepangwa sidhani kama alisaidiwa kupanda huyo kijana alikuwa anaweka balance mheshimiwa asianguke...
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM upande wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Magufuli ameonja joto ya jiwe leo akiwa jimbo la Kigoma mjini, imethibitika.

Baada ya wasanii mbalimbali kutumbuiza kwenye jukwaa, wananchi walisikika wakisema kuwa wameshatosheka na tamasha na sasa wanaondoka zao. Walipoulizwa wanasema nini ndipo walipopaza sauti kuwa ni Zitto na Lowassa tosha huku wakipunga mikono kuhashiria kuaga.

Baada ya muda mfupi uwanja ulibaki na mashabiki walioambatana na Magufuli wakiwa wameketi jukwaa la mbele.

Hii ni mara ya nne kwa Magufuli kukataliwa hadharani baada ya kufanyiwa hivyo Njombe, Mbeya na Songea mjini.

Unajitekenya na kucheka mwenyewe! Ukiwa muongo weka akiba ya uongo wako kama ilivyo kwa viongozi wa chadema, wanaongopea hadi wanasahau jana walisema nini. Mimi nilikuwepo hayo unayoyasema yalitokea eneo gani la uwanja? Uwe angalau ukitoka chooni usinywe viroba haraka kwanza uvute hewa safi.
 
Wewe sio ndiyo yule ilieleta propaganda kuwa Magufuli alimnadi Chenge wakati ni uongo.

Hizo propaganda za kipuuzi mkapigie huko mitaani humu wengi wanauelewa.

Hilo jamaa lenye id ya G.Sam ,ni lijinga fulani hivi! Linaishi kwa kuichafua jf na kuandika pumba na sijui kwa nn wanamuacha tu, inafaa aonywe kwa uzushi au apigwe ban.
 
Last edited by a moderator:
Unajua kwenye ukweli uongo hujitenga hata ukiupamba vp,mkutano Wa magufuli katika viwanja vya kawawa ujiii ulikua na watu ambao hawajawahi kutokea ktk mkutano wowote ule ktk historia ya kigoma.

Ila kusema ukweli mgombea wa ubungo kigoma mjini ndie alozomelewa tena saaana ila kwa magufuli kashangiliwa saaana tena kwa mapenzi yoote,kwa hyo dada yng acha umbea nilikuepo tena mlangoni kama unataka kwenda posta,.

Mkuu Mkoa wa Kigoma hua na matamasha machache sana ya Wasanii wa Muziki na kwa hulka ya wenyeji wa huko ambao CCM Di lolote kwao usistaajabu hao watu uliowaona wameenda kwa dhumuni la kuangalia show ya bure toka kwa Wasanii.
 
Kwa hyo unakubaliana na Mimi kua nyomi ilikua ya kutosha tu japo ilifata hao wasanii ila mwenzako alikua anapotosha umma sio
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM upande wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Magufuli ameonja joto ya jiwe leo akiwa jimbo la Kigoma mjini, imethibitika.

Baada ya wasanii mbalimbali kutumbuiza kwenye jukwaa, wananchi walisikika wakisema kuwa wameshatosheka na tamasha na sasa wanaondoka zao. Walipoulizwa wanasema nini ndipo walipopaza sauti kuwa ni Zitto na Lowassa tosha huku wakipunga mikono kuhashiria kuaga.

Baada ya muda mfupi uwanja ulibaki na mashabiki walioambatana na Magufuli wakiwa wameketi jukwaa la mbele.

Hii ni mara ya nne kwa Magufuli kukataliwa hadharani baada ya kufanyiwa hivyo Njombe, Mbeya na Songea mjini.

acha unaafiki wewe hiyo njombe sehemu gani alifanyiwa hivyo??
 
Mahaba kitu kibaya sana...

Mbona taarifa ya ITV haijaonesha haya unayoyaeleza?

Na idadi ya watu waliojitokeza ni maradufu ya wale waliojitokeza siku Lowassa akiwa Ujiji...

itv wameficha, wameonesha watu walipokuwa wakipunga mkono ni kipindi wasanii wanatumbuiza tu, si umeona hata hawajaonesha maongezi marefu ya magufuli kama ilivyo kawaida yao?
 
huyo JPM ni jambazi tu kama majambazi wengine wa sisiem. asituhadae. maana hata Jk nae aliwahadaa watz kama huyo jamaa, lkn hakuna alichocmamia. so ukawa kwanzaaa!!!!!!!
 
Kwa hyo unakubaliana na Mimi kua nyomi ilikua ya kutosha tu japo ilifata hao wasanii ila mwenzako alikua anapotosha umma sio

Nimeuangalia Mkutano kupitia StarTv, kwakua CCM hufanya Mikutano yao kwa kusomba watu sehemu mbalimbali na wengi wao wanaenda kwa ajili ya Wasanii hivyo Mtu muelewa hawezi tishika na huo Umati wa watu.
Kuna jamaa yangu anafanyia biashara zake hapo Mjini ngoja nimuulize hali halisi ilivyokua hizi siku mbili kabla ya huo Mkutano.
 
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM upande wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu John Magufuli ameonja joto ya jiwe leo akiwa jimbo la Kigoma mjini, imethibitika.

Baada ya wasanii mbalimbali kutumbuiza kwenye jukwaa, wananchi walisikika wakisema kuwa wameshatosheka na tamasha na sasa wanaondoka zao. Walipoulizwa wanasema nini ndipo walipopaza sauti kuwa ni Zitto na Lowassa tosha huku wakipunga mikono kuhashiria kuaga.

Baada ya muda mfupi uwanja ulibaki na mashabiki walioambatana na Magufuli wakiwa wameketi jukwaa la mbele.

Hii ni mara ya nne kwa Magufuli kukataliwa hadharani baada ya kufanyiwa hivyo Njombe, Mbeya na Songea mjini.
hata aibu huna wee nyumbu. nani wanaweza kuepa kumuona na kumsikiliza mtu kama magufuli. labda kama ni mpumbavu na lofa.
 
MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."

Na Mwandishi wetu,
Kigoma
 
Back
Top Bottom