Yanayojiri bungeni Dodoma leo tarehe 27 Mei, 2015

nsuka
Mkuu Kigoma si Dubai huko?

Magufuli ana mbwebwe sana halafu wabunge wa CCM wanaunga mkuno hoja 100%, baadae anaanza kulalamika hadi kengele inalia.

Marire.
Inawezekana hatukumuelewa vizuri Jakaya aliposema Kigoma itakuwa Dubai kwakuwa Dubai ni sehemu nzuri na safi lakini Kigoma hata hailezeki kwa hari ngumu hata kimaisha.Ila namshukuru Mungu kwamba wale wote tuliokuwa tunawambia ukweli juu ya usanii huo wa Kigoma kuwa Dubai huku wao wakituona sisi niwachonganishi sasa wanatukubari kwajinsi tunavyosota pamoja!
 
Kuna viashiria kutoka kwa baadhi ya wabunge walishaonwa kuhakikisha bajeti inapita. Hayo makelele siyo bure! Hii bajeti siyo ya kupitishwa aisee! Wakorofi wamekwenda wapi leo?
 
Waziri wa Ujenzi ndugu John Pombe Magufuli leo amewasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake ya ujenzi mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi kwa muda wa Afrika ya Mashariki.

Katika hotuba yake ambayo ni ya mwisho kwake katika uhai wa serikali ya awamu ya nne, ameainisha mipango na mafanikio katika wizara hiyo kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, madaraja, nyumba za watumishi wa serikali pamoja na vivuko.

Ameainisha miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja ambapo hadi kukamilika kwake, zinahitajika zaidi ya trilion nne za kitanzania. Aidha ametumia michoro mbalimbali na ramani kuonyesha miradi iliyopo kwenye mpango huo wa ujenzi katika wizara yake.

Kwa sasa anaomba zaidi ya bilioni 932 ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa sasa.

===updates===
Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni imewasilishwa na mh. Mkosamali ambapo hotuba yake imejikita katika madeni yanayodaiwa na makandarasi katika wizara hiyo ambapo madeni hayo yanakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 800, kiasi ambacho ni karibia kiasi kinachoombwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Mambo mengine lazma tuseme ukweli...tuache ushabiki usio na maana....sote tunaamini kambi ya upinzani kazi yao ni hiyo aliyoifanya mkosamali ila kiukweli hii wizara imefanya kazi kubwa sana asilimia zaid ya 80 ya barabara ipo katika kiwango kizuri na cha kupitika...zile barabara zote korofi nchini zimejengwa tena kwa kiwango kizuri..... Mkosamali anataka barabara zilizo kwenye mipango ya utekelezaji, nani asiyejua uwezo wa nchi zinazoendelea tena kubwa kama tanzania uwezo wake katika kutekeleza miradi mikubwa kama hii....tuache ushabiki na unafiki usio na maana penye jambo zuri tujaribu kusema....halafu watanzania tunaofaidika na barabara hizo tulizozipigia kelele wenyewe leo tunakuja kwenye mitandao ya kijamii kuponda....THIS IS TOTALY UKWARD......HONGERA MAGUFULI KWA KAZI KUBWA MLIYOIFANYA KIKUBWA ENDELENI KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU KWA SPIDI ZAIDI
 
nimesikiliza jinsi kigwangala alivyoshindwa kutafsiri mfano alioutoa peter msigwa nikachoka. uzuri msigwa amemchana na kumtoa kwenye watu wenye udaktari usio magumashi
 
harudi asirudi msg delivered!!!

Mungu alie sirini awajalie hawa vijana wa ukawa na ambao ni wabunge wetu mkoani Kigoma ikiwa ni pamoja na huyu wa ccm Serukamba waweze kurudi bungeni tena. Kusema ukweli na wala sio ushabiki wa vyama hawa wabunge ni majembe haswa na ndio wakombozi wa mkoa huo.Mimi sio mwenyeji na wala mkazi wa mkoa huo ila ni mfuatiliaji mzuri wa bunge na mwanachama na mfuatiliaji michango Jf. Onyo langu kwao wasijidanganye kuhama vyama vyao kipindi hiki kwani hawatachaguliwa. Sasa ombi kwa wapiga kura na haswa vijana wa mikoa yote nchini wachagueni hawa vijana wenzenu wa ukawa watawaletea ukombozi mnaotegemea. Wapo wabunge waadilifu huko ccm kama kina Filikunjombe Esther Bulaya na vijana wengine watakaojitokeza huko ccm mkawaona wana vission na misimamo yao wenyewe na sio ndio mzee.
 
...Mr Magufuli porojo na hekaya zako,zimefikia ukingoni,hata wabunge wenzio wa CCM,wanakuona muongo,refer jana Idi Azzan,Mbunge Kinondoni alivyosema haliridhishwi na majibu yako..
 
Nilikuwa namtazama na kumsikiliza Mh. Rose Kirigini mbunge wa viti maalumu wa CCM na mkuu wa wilaya ya Maswa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya ujenzi katika television akisema uongo wa waziwazi kabisa dhidi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayotoka Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi, kwamba mkandarasi yuko site tayari kuanza ujenzi. Nasikitika sana kwamba amejidanya yeye mwenyewe, kakidanganya chama chake cha CCM na zaidi sana kawadanganya wananchi wa Maswa mchana kweupe.

Ukweli ni kwamba hakuna ujenzi wowote unaoendelea na wala hata dalili tu kuwa labda mkandarasi anafanya maandalizi ya kuanza ujenzi hakuna kinyume na yeye alivyosema kuwa kampuni ya kichina ya CHICO iko site. Mimi nashangaa sana viongozi kama hawa wanatuonaje sisi wananchi iwapo wanasimama tena kwenye forum muhimu na ya kipekee kama bunge kusema uongo wa wazi kama huu badala ya kuiambia ukweli serikali ili iwatekeleze wajibu wake.

Ni kweli kuwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na hususani wilaya za Bariadi na Maswa tangu mwaka 2005 na kisha 2010 waliahidiwa na serikali hii ya CCM chini J.M. Kikwete kujengewa barabara hii kwa kiwango cha lami.Inawezekana kabisa kazi za awali kama upembuzi yakinifu (feasebility study) zilishafanyika, lakini ni ukweli ulio wazi pia kwamba na hasa kwa wananchi wa wilaya kongwe ya Maswa iliyozaa wilaya za Kishapu, Meatu, Bariadi na sasa ni mkoa mpya wa SIMIYU , hakuna ujenzi wowote wa kiwango cha lami ambao umekwisha kuanza achilia mbali kuona tu maandalizi ya vifaa vya mkandarasi vikiwa ktk site kama ambavyo mheshimiwa huyu amesema kwa udanganyifu!!.

Nifahamuvyo mimi ni kuwa, mwananchi wa kawaida (wapiga kura) wala hata haelewi nini maana ya upembuzi yakinifu na kwake yeye hiyo hata si sehemu ya ujenzi wa barabara. Kwa mwananchi wa kawaida kwake yeye ujenzi wa barabara ni kuona ma - greda na malori yakiwa site lami ikimwagwa na si kama ambavyo huyu mbunge wa CCM tena akiwa ni mkuu wa wilaya ya wananchi haohao anaowadanganya!.

Kwa wasiofahamu, ni kuwa, wilaya ya Maswa ina majimbo ya uchaguzi mawili; Maswa Magharibi mbunge wake ni JOHN MAGALLE SHIBUDA (CHADEMA) na Maswa mashariki ni SYLEVESTER KASULUMBAYI (CHADEMA). Sina hakika kama hawa jamaa walikuwepo au hawakuwepo bungeni leo, na kama walikuwepo sijui ni kwa nini walimwacha tu huyu mama akiwadanganya wananchi wao mchana kweupe!...Na nasikia huyu mama anataka kugombea ubunge katika moja ya majimbo haya na kwa uongo huu sidhani kama CCM watayarudisha tena haya majimbo, wamekosa kura tayari!!

Mimi nadhani mh. Rose Kirigini na mkuu wa wilaya ya Maswa hebu tu awaombe radhi wananchi wa wilaya yake kwa kuwaona wajinga, hawaoni na hawana ufahamu kwamba serikali haijaanza ujenzi wa barabara hii ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi kwa kiwango cha lami!!
 
Mungu alie sirini awajalie hawa vijana wa ukawa na ambao ni wabunge wetu mkoani Kigoma ikiwa ni pamoja na huyu wa ccm Serukamba waweze kurudi bungeni tena. Kusema ukweli na wala sio ushabiki wa vyama hawa wabunge ni majembe haswa na ndio wakombozi wa mkoa huo.Mimi sio mwenyeji na wala mkazi wa mkoa huo ila ni mfuatiliaji mzuri wa bunge na mwanachama na mfuatiliaji michango Jf. Onyo langu kwao wasijidanganye kuhama vyama vyao kipindi hiki kwani hawatachaguliwa. Sasa ombi kwa wapiga kura na haswa vijana wa mikoa yote nchini wachagueni hawa vijana wenzenu wa ukawa watawaletea ukombozi mnaotegemea. Wapo wabunge waadilifu huko ccm kama kina Filikunjombe Esther Bulaya na vijana wengine watakaojitokeza huko ccm mkawaona wana vission na misimamo yao wenyewe na sio ndio mzee.

ukawa wanashabikia madeni as if madeni ni kitu haramu
 
Nilikuwa namtazama na kumsikiliza Mh. Rose Kirigini mbunge wa viti maalumu wa CCM na mkuu wa wilaya ya Maswa wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya ujenzi katika television akisema uongo wa waziwazi kabisa dhidi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayotoka Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi, kwamba mkandarasi yuko site tayari kuanza ujenzi. Nasikitika sana kwamba amejidanya yeye mwenyewe, kakidanganya chama chake cha CCM na zaidi sana kawadanganya wananchi wa Maswa mchana kweupe.

Ukweli ni kwamba hakuna ujenzi wowote unaoendelea na wala hata dalili tu kuwa labda mkandarasi anafanya maandalizi ya kuanza ujenzi hakuna kinyume na yeye alivyosema kuwa kampuni ya kichina ya CHICO iko site. Mimi nashangaa sana viongozi kama hawa wanatuonaje sisi wananchi iwapo wanasimama tena kwenye forum muhimu na ya kipekee kama bunge kusema uongo wa wazi kama huu badala ya kuiambia ukweli serikali ili iwatekeleze wajibu wake.

Ni kweli kuwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na hususani wilaya za Bariadi na Maswa tangu mwaka 2005 na kisha 2010 waliahidiwa na serikali hii ya CCM chini J.M. Kikwete kujengewa barabara hii kwa kiwango cha lami.Inawezekana kabisa kazi za awali kama upembuzi yakinifu (feasebility study) zilishafanyika, lakini ni ukweli ulio wazi pia kwamba na hasa kwa wananchi wa wilaya kongwe ya Maswa iliyozaa wilaya za Kishapu, Meatu, Bariadi na sasa ni mkoa mpya wa SIMIYU , hakuna ujenzi wowote wa kiwango cha lami ambao umekwisha kuanza achilia mbali kuona tu maandalizi ya vifaa vya mkandarasi vikiwa ktk site kama ambavyo mheshimiwa huyu amesema kwa udanganyifu!!.

Nifahamuvyo mimi ni kuwa, mwananchi wa kawaida (wapiga kura) wala hata haelewi nini maana ya upembuzi yakinifu na kwake yeye hiyo hata si sehemu ya ujenzi wa barabara. Kwa mwananchi wa kawaida kwake yeye ujenzi wa barabara ni kuona ma - greda na malori yakiwa site lami ikimwagwa na si kama ambavyo huyu mbunge wa CCM tena akiwa ni mkuu wa wilaya ya wananchi haohao anaowadanganya!.

Kwa wasiofahamu, ni kuwa, wilaya ya Maswa ina majimbo ya uchaguzi mawili; Maswa Magharibi mbunge wake ni JOHN MAGALLE SHIBUDA (CHADEMA) na Maswa mashariki ni SYLEVESTER KASULUMBAYI (CHADEMA). Sina hakika kama hawa jamaa walikuwepo au hawakuwepo bungeni leo, na kama walikuwepo sijui ni kwa nini walimwacha tu huyu mama akiwadanganya wananchi wao mchana kweupe!...Na nasikia huyu mama anataka kugombea ubunge katika moja ya majimbo haya na kwa uongo huu sidhani kama CCM watayarudisha tena haya majimbo, wamekosa kura tayari!!

Mimi nadhani mh. Rose Kirigini na mkuu wa wilaya ya Maswa hebu tu awaombe radhi wananchi wa wilaya yake kwa kuwaona wajinga, hawaoni na hawana ufahamu kwamba serikali haijaanza ujenzi wa barabara hii ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi kwa kiwango cha lami!!

kuna magreda mkuu yanafanya usafi wa barabara wiki yote
 
wanaharakat wenzangu kwa yeyote mwenye hotuba ya magufuli jioni ya leo atuwekee hapa na sisi tulio nje ya nchi yetu tujue kinachoendelea huko nyumbani
 
nimesikiliza jinsi kigwangala alivyoshindwa kutafsiri mfano alioutoa peter msigwa nikachoka. uzuri msigwa amemchana na kumtoa kwenye watu wenye udaktari usio magumashi

bunge safari hii limepwaya wabunge wameenda majimboni akiwepo KUB
 
Madeni ya makandarasi karibu ni sawa na bajeti nzima ya wizara yako----800+ Billions vs 900+ billions respectively. Kuwa mkweli utazilipaje katika hali ya kifedha ya taifa hili? Unadanganya mchana kweupeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom