Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Tarehe 12 Machi 2014 - Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Habari wadau wote wa Mtandao Pendwa Tanzania, mtandao wa kila mtu bila kujali itikadi zake za kisiasa, kidini, umri na jinsia, Mtandao wa JamiiForums.

Ni matumaini yangu kuwa Mwenyezi Mungu amewaamsha salama na wengi wenu mpo kwenye majukumu ya kujipatia riziki na kujenga taifa.

Wale ambao hawajaamka vema kwa siku ya leo kwa maana ni wagonjwa, Mwenyezi Mungu awajaalie wapone kwa haraka ili waungane nasi hapo jioni wakati tutakapowaletea moja kwa moja yatakayojiri Bungeni Dodoma wakati wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Kwa wale ambao wametangulia mbele za haki, tuwaombee dua kwa Mwenyezi Mungu ili wafike kwa amani kwenye nyumba ya milele na awaondolee adhabu za kaburi

Wadau, ikiwa ni saa moja kabla ya muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu, ni wagombea wanne wamejitokeza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum.

Wagombea hao ni SAMMUEL SITTA, THERESIA HUVISA, HASHIM RUNGWE na JOHN CHIPAKA. Bado sijapata taarifa za wagombea hao kurejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni Prof Costa Mahalu kupitia Ofisi za Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi.

Pindi tutakapopata taarifa za uhakika, tutazirusha kama kawaida. Kwa sasa tuendelee kupata maoni ya wadau mbalimbali juu ya uchaguzi huu huku tukiendelea kutafakari uchaguzi huo kwa ujumla wake.

Kama kawaida natarajia kuungwa mkono kutoka kwa wadau mbalimbali hususan Skype, Simiyu Yetu, MaishaPesa, MKUU WA KAYA, Deo Corleone, Pasco na wengi ambao sijawataja lakini wamekuwa pamoja nasi tangu tuanze utaratibu huu.

Stay Connected

=====================

UPDATE 1:
- Wabumge wameanza kuingia Ukumbini. Ndani ya Ukumbi wa Bunge, idadi ya Wabunge ni ndogo dakika 10 kabla ya Kikao Kuanza.

- Wagombea waliotimiza vigezo vya kugombea ni wawili tu na wengineo hawapo tena katika kinyang'anyiro hicho. Waliokidhi vigezo kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba; Samwel J. Sitta na Hashim Rungwe!

- Kila mgombea anapewa nafasi ya Dakika tatu kujieleza kisha yatafuata maswali. Anaanza kujieleza Hashim Rungwe.

* Rungwe kamaliza kujieleza; zaidi amedai yeye ni Mtanzania wa kwanza kuwa na Yard ya Magari mwishoni mwa miaka ya 80 na yeye ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania

* Sitta kajieleza wasifu wake kwa ufupi na kuwahakikishia wajumbe kuwa hatapendelea upande wowote. Anataka kuwahakikishia watanzania kuwa wataona sababu ya wajumbe kupewa hata kiinua mgongo watakapomaliza zoezi hili. Kasema yeye kupewa kiti ni sawa na kumrudisha chura kwenye maji, ni wazi ataogelea tu!
*Zoezi la upigaji kura linaendelea



================================================================

UPDATES 2

MATOKEO
Jumla ya wabunge wote 629
waliopiga kura ni. 563
Kura zilizoharibika ni. 7
Hashim Rungwe. 69 (12.3%)
Sammuel Sitta. 487. (86.5%)

======================



 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    737.5 KB · Views: 1,914
Pamoja Mkuu! Leo nimenunua "bundle" ya kutosha kuniwezesha kuwepo kwa muda mrefu ndani ya JF!
 
MR Chabruma nimekupata vilivyo, kuna habari zinazagaa mtaani kuwa Mh Sitta ameugua ghafla na yupo hospitali ni za kweli au ndio ya Ibilisi kuwatisha watu. nakama ni uzushi au ukweli katika jina la Yesu habari au ugonjwa ushindwe "Watapigana nawe laki hawatakushinda"
 
Wakuuu msijeshangaa hapo Mwanamama Pekee Dr Tereza Hovisa akachaguliwa kwa wingi wa kura na hao jamaa wa CCM, si mnajua SITA alivyowashughulikia huko nyuma????
 
Mbona wagombea wengine wana kwashakoo mvuto hawana wanatuaribia mechi ya leo
 
[QUOTE
quote_icon.png
By mpombo
kuna habari zimezaga mtaani kuwa Mh sitta ameugua ghafla na sasa yupo hospital je ni kweli
[/QUOTE]

Hizi habari ni za kweli au ni uvumi? Source uk wa kwanza humu kwenye kichwa;
[h=2]re: Uchaguzi: Hii ndio Dira ya Mh. Samuel J. Sitta Kama mwenyekiti Bunge la Katiba[/h]
 
Sita mnafiki sana na CCJ yake
Wenye chama wameshamweka sawa hana lolote tena lazima awasikilize kwani toka mwanzo walishasema hawataki katiba mpya iliyopo inatosha sana hicho ni kiherehere cha JK
Changa la macho
Mwenyekiti ilipaswa awe Mtanganyika, Mch. Mh. Christopher Mtikila basi tu.
Chama Cha Makalio ndivyo kilivyo
 
Hujanitaja mimi,zaidi umewarusha wana lumumba
Samahani mkuu. Nilikutaja kwa ujumla wake. Ila kuna wengine nimewataja si wana Lumumba. Katika mjadala huu wa Katiba Mpya tumewekeana makubaliano kuwa tofauti zetu za kisiasa tuziweke pembeni
 
mpombo MR Chabruma nimekupata vilivyo, kuna habari zinazagaa mtaani kuwa Mh Sitta ameugua ghafla na yupo hospitali ni za kweli au ndio ya Ibilisi kuwatisha watu. nakama ni uzushi au ukweli katika jina la Yesu habari au ugonjwa ushindwe "Watapigana nawe laki hawatakushinda"[/QUOTE]
Mkuu, kumbuka ule msemo kuwa Tanzania kuna mitambo ya kupika majungu. Kuwa mwangalifu na unachosikia
 
Last edited by a moderator:
Sita mnafiki sana na CCJ yake
Wenye chama wameshamweka sawa hana lolote tena lazima awasikilize kwani toka mwanzo walishasema hawataki katiba mpya iliyopo inatosha sana hicho ni kiherehere cha JK
Changa la macho
Mwenyekiti ilipaswa awe Mtanganyika, Mch. Mh. Christopher Mtikila basi tu.
Chama Cha Makalio ndivyo kilivyo
Mkuu, mchakato ulikuwa wazi na hakuna mtu aliyekatazwa kuchukua fomu
 
Tuko pamoja! Saa nne ndo hii muda wa mwisho wa kurudisha fomu tupe majina ya waliorudisha fomu!
 
Back
Top Bottom