Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumamosi, Tarehe 12 Aprili 2014 - Uwasilishaji wa Taarifa za Kamati

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, naamini kuwa hamjambo na mmeamka salama. Nami pia Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniamsha salama. Wale wagonjwa tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapone haraka. Wale waliofikwa na mauti, tumuombe Mwenyezi Mungu awape mwisho mwema.

Wadau, uwasilishaji wa Taarifa za Kamati 12 za Bunge Maalum umeanza juzi Alhamis tarehe 10 April 2014. Katika siku hiyo, jumla ya kamati 4 ziliwasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 2,5,9 na 11. Aidha, Jana Ijumaa kamati nne ziliwasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 1,8,10 na 12. Hivyo, hadi leo Kamati nne hazijawasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 3,4,6 na 7. Kwa vile Bunge kwa siku ya leo linaishia saa saba mchana, ni wazi kuwa kamati mbili tu zitawasilishwa. Kamati mbili zitakazobaki zitawasilisha siku ya Jumatatu ijayo.

Mpaka sasa, kuna mfanano usio wa kawaida kwa taarifa zote. Taarifa za walio wengi kwa kamati zote zinafanana ikiwa ni pamoja na ibara zinazofanyiwa marekebisho, aina ya marekebisho na sababu za marekebisho. Mathalan, katika Ibara ya Kwanza, walio wengi wanapendekeza marekebisho badala ya neno shirikisho, wanapendekeza litumike neno Jamhuri. Pia badala ya neno Tanganyika, wanataka itumike Tanzania Bara. Halikadhalika katika Ibara ya 60 juu ya muundo wa muungano, walio wengi kwa kamati zote wanapendekeza muundo wa serikali mbili badala ya serikali tatu zilizopo kwenye rasimu ya katiba. Sababu kuu inayotolewa ni Hati ya Muungano

kwa upande wa maoni ya walio wachache, wao ni copy and paste kama ilivyo kwa walio wengi. Wao wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye Rasimu ya Katiba yaendelee. Sababu kubwa wanayotoa ni kwamba Maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni Maoni ya Wananchi. Pia maoni ya walio wachache wanatumia rejea zile zile kuimarisha hoja zao. Mathalan, wamekuwa wakitumia na kutetea takwimu zile zile za Warioba, wamekuwa wakirejea tume zile zile za akina Kisanga na Nyalali.

Na wamekuwa wakinukuu kazi zile zile za wasomi mbalimbali kama akina Prof Shivji, Paramagamba Kabudi nk. Hali hii imefanya baadhi ya wadau kuhoji uwepo wa utitiri wa kamati ilhali maoni yao yanafanana. Wanasema kuwa mfumo uliotumika wakati wa kujadili Rasimu ya Katiba ungetumika ambapo watu waliotoka makundi mbalimbali waliounda kamati moja chini ya Prof Costa Mahalu na walitoa mapendekezo ya rasimu ya kanuni inayokubalika. Wanasema kuwa hali hiyo ingeokoa muda zaidi na wabunge wangepata muda zaidi wa kujadili. Hayo ni maoni tu ya wadau.

Karibu kwamjadala

----------------------------

- Mwenyekiti ameingia na dua imesomwa. Kamati inayoanza kuwasilisha taarifa yake ni kamati namba tatu ambayo inasomwa na mwenyekiti wake Dr Fransis Michael

- MAONINYA WALIO WENGI
* Ibara ya kwanza wanapendekeza iwe Jamhuri badala ya shirikisho. Sababu wanayotoa ni Sheria ya mabadiliko ya katiba, Ibara ya kwanza inataka uwepo wa Jamhuri ya Muungano. Wanasema kuwa hata Kamati ya Warioba ililitambua hili na ndani ya randama ya tume, ukrasa wa 3 imetaja uwepo wa Jamhuri. Pia wanasema kuwa makubaliano na sheria ya mwaka 1964 yanatambua uwepo wa Jamhuri na hivyo wanapendekeza makubaliano hayo yawe nyongeza ya Rasimu ya Katiba. Walio wengi wanashangaa wachache kutamka hati ya Muungano ilhali Tume ya Jaji Warioba inaitambua.

- Dr Fransis anasema kuwa Hati ya Muungano ni sahihi na Wazanzibari walihusika kuiridhia. Amenukuu maneno ya Marehemu Thabit Kombo wakati akichangia hoja ya kuridhia hati hiyo kwenye Bunge la Tanganyika.

- Dr Fransis anasema kuwa kuna watu hawana utashi wa muungano huu kudmu na hivyo wanataka uwepo wa serikali tatu ili wavunje muungano

- Mwenyekiti anatoa ufafanuzi kuwa wanaowasilisha wanaruhusiwa kutoa ufafanuzi wa hoja ili mradi hawako nje ya mada na wahakikishe kuwa wanaacha dakika zisizopungua 15 kwa ajili ya kusoma maoni ya wachache

- Dr Fransis anamnukuu Juma Duni Haji wakati aki wind up election campaign kwa chama cha CUF huko Zanzibar mwaka 2005 aliposema kuwa "Wakati wa kutawala watu weusi Zanzibar umeisha"

- Anasema kuwa muungano wa shirikisho unaweza kusababisha matatizo mengi ambayo yatahatarisha muungano wetu. Pia kukiwa na shirikisho, kila nchi itakuwa na mila na desturi zake ambazo zinaweza kusababisha mgongano na hivyo kuweza kuhatarisha umoja na mshikamano wetu

- Dr Fransis anasema kuwa muungano wetu ni wa udugu hasa kwa vile wameoleana katika pande zote

- Dr Fransis anapendekeza kuwa mipaka ya nchi isitenganishwe baina ya Zanzibar na bara

- Dr Fransis anapendekeza ziwepo Ibara ambazo zitahakikisha hifadhi na matumizi sawa ya ardhi na vitu vilivyomo kwa manufaa ya watu wake.

- Dr Fransis ametumia muda mwingi kufafanua hoja ya wali wengi. Hakika katika hili napenda kulilaumu bunge hili kwa kutoliangalia hili toka mwanzo

- Walio wachache wamekataa taarifa yao kusomwa na Dr Fransis na hivyo mchungaji Msigwa anawasilisha taarifa hiyo

- Kuhusu Ibara ya kwanza, walio wachache wanapendekeza jina liitwe shirikisho kwa vile wakati zinaungana nchi mbili hizi, zilikuwa huru. Hivyo nchi huru zinapoungana, kinachozaliwa ni shirikisho na si Jamhuri. Hapa anamnukuu Prof Issa Shivji

- Msigwa anasema kuwa shirikisho litaondoa utata unaojitokeza ndani ya muungano uliopo ambao umesababisha kuvunjwa kwa katiba ya jamhuri na serikali zote mbili

- Kuhusu mipaka, wanapendekeza ibaki kama ilivyo kwenye rasimu ispokuwa kila nchi iweke mipaka yake kama ilivyokuwa kabla ya muungano

- Mchungaji Msigwa naona alikuja na desa jingine. Alikuwa anasoma taarifa tofauti na iliyowasilishwa kwa Katibu wa Bunge.

- Msigwa amemaliza kutoa ufafanuzi na Mwenyekiti anasema kuwa wabunge wamenufaika na nukuu mbalimbali ila si ufafanuzi wa sura ya kwanza na ya sita

- KAMATI NAMBA NNE
DR HAMISI KIGWANGALLAH anawasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti Christopher Ole Sendeka ambaye ameenda kwenye kumbukumbu ya kifo cha Edward Moringe Sokoine huko Monduli

- Hamisi Kigwangallah ameanza kwa kutaja majina ya wajumbe walio wengi

- Dr. Kigwangallah anasema kuwa mjadala unaoendelea umetawaliwa na muundo wa muungano anaeleza jinsi changamoto zilizobainishwa na tume ya katiba mpya

- Kama kuna Member wa UKAWA ajitokeze humu kutueleza ni kwa nini mpaka sasa kamati tisa zimewasilisha, hakuna hata msemaji mmoja mwanamke wa maoni ya wachache. Hii ni aibu kubwa kwa UKAWA kukumbatia mfumo dume. Binafsi kuna wanawake jasiri wengi tu ndani ya UKAWA kama akina Esther Matiko, Lucy Owenya, Halima Mdee, Chiku Abwao nk. Kwa nini wanaendekeza mfumo Dume?

- Lissu ameanza mbwembwe zake. Anamnukuu yuleyule Prof Shivji. Prof Shivji anasema kuwa muungano huu haujawahi kuridhiwa na baraza la wawakilishi

- Lissu pia anamnukuu yuleyule Mwakyembe kama walivyonukuu kamati zilizopita. Mwakyembe amenukuliwa akisema kuwa mfumo wa Serikali tatu ni suluhisho pekee la matatizo ya muungqno uliopo

- Tundu Lissu ananukuu pia maoni ya wahadhili 15 wa chuo kikuu cha DSM ambao walipendekeza muundo wa serikali tatu. Anasema kuwa baadhi ya wahadhiri hao wapo ndani ya bunge na wamepiga kura kukataa shirikisho

- Lissu anauliza kama Hati ya Muungano ipo, halali na je Muungano huu ni halali?

--------------------

attachment.php


Wananchi+wakifuatilia+Bunge.JPG


Wananchi katika moja ya mskani ya Kikwajuni Weles (Zanzibar) wakifuatilia mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba Tanzania kupitia Kituo cha Television ya Taifa TBC, kikiripoti moja kwa moja kutoka Dodoma wakati Mhe Tundu Lissu alipokuwa akizungumza. (picha: ZanziNews.com)

Kupitia blogu yake, Mjumbe wa Bunge la Katiba, Salma Said ametoa ufafanuzi wa kilichotokea leo Bungeni na mustakabali wake kama ifuatavyo:

Ni kweli hali ya hewa leo katika Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea Dodoma ilichafuka ghafla na kusababisha kelele na manunguniko kutoka kwa wajumbe wakilalamikia kukatika kwa matangazo ambapo matangazo yanayorushwa moja kwa moja (Live) na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutoka Bungeni Dodoma yalikatika kulikotokana na sababu za kiufundi.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta amelazimika kuakhirisha kikao hadi Jumatatu ambapo kabla ya kusikilizwa taarifa za kamati nyengine mbili zilizobaki itabidi Mjumbe wa Bunge hilo Tundu Lissu aendelee kutoa ufafanuzi wake ambao aliuanza leo kabla ya kukatika kwa matangazo hayo.

Mwenyekiti wa Bunge hilo alilazimika kusitisha shughuli hizo baada ya Mjumbe Freeman Mbowe kutoa taarifa za kupokea kwa kukatika kwa matangazo huku baadhi ya wajumbe wengi wakiwa wametumiwa sms katika simu zao wakitaarifiwa kwamba matangazo hayo yanayorushwa moja kwa moja kupitia TBC hayapo hewani. Mwenyekiti alimtuma Katibu wake Yahya Khamis kwenda kusikiliza kinachoendelea na hatimaye kuja na taarifa kwamba ni khitilafu iliyotokana na hali mbaya ya hewa huko Dar es Salaam ambapo kuna mvua tokea juzi.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe walipingana na uamuzi huo wakihoji ni kanuni gani inayosema kuwa kwa kuwa matangazo yamekatika ndiyo bunge liakhirishwe lakini Mwenyekiti alijibu kwamba kanuni inamruhusu Mwenyekiti kuchukua maamuzi ambayo anaona yanafaa na kutumia busara, hivyo yeye ametumia busara kutokana na kuwa mjadala wa katiba muhimu kusikika na Watanzania wote.

Kwa umuhimu huo, ili watu wengine wasije kuona kwamba matangazo hayo yanakatwa kwa hujuma au kuwanyima haki wengine na kuwapa fursa wengine, ameamua kuchukua uamuzi huo ili kila upande uweze kusikika huko nje na umma wa Watanzania na hasa kwa kuzingatia tayari kuna mkataba kati ya Serikali, Bunge na Shirika la Utangazaji (TBC) kwamba wataonesha live shughuli za majadiliano katika Bunge Maalumu la Katiba. Hivyo basi wananchi walikataa kuendelea na mjadala huo hadi hapo matangazo hayo yatakaporudi na ndiyo Mwenyekiti akatumia busara kuliakhirisha Bunge hadi Jumatatu.

Juzi wakati akitoa ufafanuzi ya maoni ya wajumbe wachache Professa Ibrahim Lipumba pia matangazo hayo yalikuwa yakikatika katika jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wananchi wengi ambao wanaofuatilia mjadala huo wa katiba na hivyo kiasi cha baadhi ya wananchi kujenga dhana kwamba hali hiyo husababishwa kwa makusudi ili kuwakosesha wananchi wasisikie maoni kutoka kwa wapinzani ambao wana haki sawa kama wanachama wengine ambao wanahitaji kusikiliza hoja za pande mbili.

…tutaendelea tena inshallah Jumatatu ambapo watakaotoa ufafanuzi ni kamati mbili zilizobaki ambazo ni Freeman Mbowe na Ismail Jussa, baada ya Wenyeviti kuwasilisha maoni ya Wajumbe wengi na wachache.

Lissu+LIpumba.jpg


Wajumbe wa Bunge Maalum la KatibaTundu Lissu( kushoto) akisalimiana na Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) mara baada ya kikao cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. Kulia ni Mchungaji Peter Msigwa.

Chanzo: wavuti: Lissu kuendelea Jumatatu alikokomea leo baada ya TBC kukata ghafla - wavuti.com

=========================

MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA​

Soma - https://www.jamiiforums.com/katiba-...a-nne-iliyowasilishwa-na-mhe-tundu-lissu.html
 
Kama badala ya neno Tanganyika itumike Tanzania Bara basi na badala ya Zanzibar itumike Tanzania Visiwani, hata raisi wao aitwe wa Tanzania Visiwani
 
Hayo maoni yawezekana yanaandikwa na watu/mtu fulani.Ni marudio tu ya Hotuba ya Rais Kikwete.Sijui lengo hasa ni nini?
 
- Mwenyekiti ameingia na dua imesomwa. Kamati inayoanza kuwasilisha taarifa yake ni kamati namba tatu ambayo inasomwa na mwenyekiti wake Dr Fransis Michael

- MAONINYA WALIO WENGI
* Ibara ya kwanza wanapendekeza iwe Jamhuri badala ya shirikisho. Sababu wanayotoa ni Sheria ya mabadiliko ya katiba, Ibara ya kwanza inataka uwepo wa Jamhuri ya Muungano. Wanasema kuwa hata Kamati ya Warioba ililitambua hili na ndani ya randama ya tume, ukrasa wa 3 imetaja uwepo wa Jamhuri. Pia wanasema kuwa makubaliano na sheria ya mwaka 1964 yanatambua uwepo wa Jamhuri na hivyo wanapendekeza makubaliano hayo yawe nyongeza ya Rasimu ya Katiba. Walio wengi wanashangaa wachache kutamka hati ya Muungano ilhali Tume ya Jaji Warioba inaitambua.

- Dr Fransis anasema kuwa Hati ya Muungano ni sahihi na Wazanzibari walihusika kuiridhia. Amenukuu maneno ya Marehemu Thabit Kombo wakati akichangia hoja ya kuridhia hati hiyo kwenye Bunge la Tanganyika.

- Dr Fransis anasema kuwa kuna watu hawana utashi wa muungano huu kudmu na hivyo wanataka uwepo wa serikali tatu ili wavunje muungano

- Mwenyekiti anatoa ufafanuzi kuwa wanaowasilisha wanaruhusiwa kutoa ufafanuzi wa hoja ili mradi hawako nje ya mada na wahakikishe kuwa wanaacha dakika zisizopungua 15 kwa ajili ya kusoma maoni ya wachache

- Dr Fransis anamnukuu Juma Duni Haji wakati aki wind up election campaign kwa chama cha CUF huko Zanzibar mwaka 2005 aliposema kuwa "Wakati wa kutawala watu weusi Zanzibar umeisha"

- Anasema kuwa muungano wa shirikisho unaweza kusababisha matatizo mengi ambayo yatahatarisha muungano wetu. Pia kukiwa na shirikisho, kila nchi itakuwa na mila na desturi zake ambazo zinaweza kusababisha mgongano na hivyo kuweza kuhatarisha umoja na mshikamano wetu

- Dr Fransis anasema kuwa muungano wetu ni wa udugu hasa kwa vile wameoleana katika pande zote

- Dr Fransis anapendekeza kuwa mipaka ya nchi isitenganishwe baina ya Zanzibar na bara

- Dr Fransis anapendekeza ziwepo Ibara ambazo zitahakikisha hifadhi na matumizi sawa ya ardhi na vitu vilivyomo kwa manufaa ya watu wake
 
CCM bara hawathubutu kusema hilo wazi wazi mbele ya wenzao wa zanzibar.Sijui ccm bara imelogwa vile yaani haijitambui kabisa na kukosa uzalendo wa tanganyika
'Mayu' CCM walishakata mishipa ya aibu,ni kama wapo kwenye nchi ya watu wasio na akili kabisa isipokuwa wao.sasa tutatumia vizuri uchache wetu ndani ya BMK kuwanyosha wote pamoja na mabwana zao
 
kulikuwa na udhibiti mkubwa wa ccm kwenye kamati...sasa huyu msomi alipenya penyaje? na mbona anaongea vitu illogicaly!
 
Dk fracis ni kama ummy mwalimu anaweka mambo sawa kwenye ukumbi anafuta upotoshaji wote wa ukawa.
 
WAJUMBE wengi wa Kamati Namba Moja ya Bunge hilo, wameona kuwa hatua ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kupendekeza uwepo wa serikali tatu, imekiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Hayo yalisemwa bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ummy Mwalimu alipokuwa akiwasilisha maoni ya wajumbe wengi na walio wachache baada ya kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.

Mwalimu alisema kwa maoni ya wajumbe walio wengi, Tume hiyo kupendekeza kuwepo kwa serikali tatu, si tu kumekiuka kifungu cha 9 (2) (a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, bali kumekiuka Mkataba wa Muungano wa mwaka 1964, sheria zilizoridhia Mkataba huo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Alisema pamoja na sababu za kisheria zilizoelezwa na wajumbe wengi, maoni ya wajumbe wengi dhidi ya pendekezo la muundo wa serikali tatu ni kuwa serikali ya shirikisho ya Jamhuri ya Muungano, inayopendekezwa na Tume ni dhaifu kimfumo na kimuundo. Tume hiyo iliongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Alisema kiutawala na kwa mamlaka iliyopewa na rasimu, serikali hii imeundiwa mfumo, ambao unaitenganisha na wananchi kwa sababu haina mamlaka ya kushughulikia masuala yanayowagusa wananchi moja kwa moja na hivyo mfumo huo hauwezi kuchukuliwa kwamba unaimarisha Muungano.

“Kwa maoni ya wajumbe walio wengi, Muungano wa Serikali Mbili ndio muafaka kulingana na mazingira yetu, muundo huo pia umekuwa ndio nguzo kubwa na imara katika kuimarisha amani na usalama wa pande zote mbili, utaifa, udugu, umoja na mshikamano, ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii kati ya Watanzania wa pande zote mbili.

“Hadi leo miaka 50 baada ya kuasisiwa kwa Muungano wa Serikali Mbili wananchi wa Tanzania bado wanajisikia kuwa ni wamoja, wanashirikiana katika mambo mbalimbali bila ya kujali wanatoka upande gani wa Muungano,” alisema Mwalimu.

Kuhusu Sura ya Kwanza inayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu alisema maoni ya wajumbe wengi, yanapendekeza kuwa neno Shirikisho liondolewe katika Ibara 1, Ibara ndogo ya Kwanza na Ibara ndogo ya (2).

Alisema kutokana na kuondolewa kwa maneno hayo, sasa Ibara hiyo itasomeka kuwa; Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili, ambayo imetokana na Muungano wa nchi hizi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, ambazo kabla ya Hati ya Makuibaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.

Ibara ya Kwanza (2) itasomeka; “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujitegemea, utawala wa sheria. Inayoheshimu misingi ya haki za binadamu na isiyofungamana na dini yoyote.”

Alisema kwa mujibu wa maoni ya walio wengi, sababu ya kutaka neno Shirikisho liondoke ni kutokana na kuwa neno hilo, ambalo mantiki yake inajiakisi kwenye Ibara ya 60 (1) ya Rasimu ya Katiba, inayoonesha Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu.

Alisema pendekezo hilo la Rasimu ni kinyume na Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964.

“Msingi mkuu wa makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 ni muundo wa serikali mbili. Kwa maana hiyo Hati ya Makubaliano ya Muungano wa Serikali mbili haiwezi kutumika kujenga msingi na kuwa mwendelezo wa shirikisho la Serikali Tatu,” alisema Mwalimu.

Alisema kama ilivyo wazi, Mkataba wa Muungano wa mwaka 1964 na sheria mbili zilizouridhia, Katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, msingi wake mkuu ni muundo wa serikali mbili na kwamba hadi leo muundo huo haujawahi kurekebishwa pamoja na marekebisho kadhaa yaliyowahi kufanywa.

“Pamoja na sababu zilizotajwa hapo juu, maoni ya walio wengi pia yamezingatia kifungu cha 9 (2) (a) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83 ya Sheria za Tanzania.

“Kifungu hiki kinalenga kuhakikisha kwamba katika kuandika Katiba mpya, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalindwa na kuendelezwa. Mantiki yake ni kuwa Jamhuri ya Muungano inayotamkwa kwenye sheria na inayopaswa kulindwa ni ile iliyoasisiwa na Mkataba wa Makubaliano wa Muungano wa mwaka 1964 ambao msingi wake mkuu ni muundo wa serikali mbili. “

Aidha katika hadidu za rejea, Tume ya Mabadiliko ya Katiba (Tume) haikupewa maelekezo ya kwenda kukarabati muundo huu na kuleta na kuleta muundo tofauti,” alisema Mwalimu.

Kuhusu maoni ya wajumbe walio wachache, Mwalimu alisema wajumbe wengi waliomba kuona nakala halisi au nakala iliyothibitishwa kisheria ya Hati ya Muungano, iliyosainiwa na waasisi wawili Mwalimu Julius Nyerere na Rais Abeid Karume Aprili 22, 1964.

Hata hivyo, alisema kilicholetwa kilikuwa ni nakala ya Sheria ya Uthibitisho wa Hati ya Muungano ya 1964, ambayo ina jedwali la maudhui ya Hati ya Muungano iliyosainiwa Aprili 25, 1964 na hadi Kamati ilipomaliza mjadala, nakala ya Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyothibitishwa haikupatikana.

“Wajumbe walio wachache walieleza kuwa Hati ya Makubaliano ya Muungano imetambua uwepo wa Serikali Tatu ambapo Serikali ya Muungano ndiyo ilikuwa mamlaka ya juu ya kidola, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ina mamlaka ya mambo yasiyokuwa ya Muungano na kwa upande wa Tanganyika yapo ambayo hayako katika Muungano,” alisema.

CHANZO: Habarileo
 
Hakuna haja ya kuwepo na rais zanzibar, iwe serikali moja tu. Tanzania tu kwisha hakuna haja ya visiwani au bara
 
Shikamoo Mzee wetu, Mwalimu Nyerere,

Mwalimu, imebaki miezi michache tu ili Muungano huu utimize miaka 50, lakini nina mashaka kama hautakufa kabla ya miaka hiyo kutimia. Umoja, amani, upendo na mshikamano uliojengwa na muungano huo umetoweka kabisa.

Ndiyo, si unaelewa kwamba hivi sasa Watanzania wako kwenye mchakato wa Katiba Mpya? Ile ambayo wewe uliikataa kipindi kile na kushauri kasoro ndogo ndogo ziwe zinarekebishwa (yaani itiwe viraka), sasa inaelekea kupatikana, maana mabilioni ya fedha za walipa kodi yamekwishatumika.

Halafu nikwambie kitu kimoja, ile serikali iliyowaponza John Malecela na Horace Kolimba mpaka ukawatungia kitabu – serikali ya Tanganyika – sasa inazaliwa rasmi. Ndiyo, na Wanzibari uliokuwa ukiwatetea kwa kuulinda Muungano, safari hii ndio vinara wa kuupinga Muungano. Tena basi kuna vikundi tayari huko Visiwani vinavyohamasisha kuupinga na kutaka Serikali ya Tanganyika iwemo ndani ya Katiba.

Mwalimu, nafahamu kwamba unatambua jinsi Muungano ulivyopitia katika vipindi vigumu mno na kuna nyakati ambapo umetiwa msukosuko kiasi cha kutishia hatma yake. Hilo, kwa kiasi kikubwa, limetokana na baadhi ya watu kutoa mapendekezo anuai yanayoashiria muungano huo ama unaweza kuendelea kudumu au kuvunjika kabisa.

Wananchi wa Tanzania wanazijua faida na hasara za muungano huo kwa kipindi chote hicho na ni wazi kwamba ndiyo maana wengi wao wamejitokeza kuchangia mawazo yao katika Rasimu ya Katiba wakitaka Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.

Wazanzibari wanasema wanataka kuona nchi ambayo waliungana nayo ikitajwa kwenye Katiba, lakini Wabara nao wanasema wanataka Tanganyika ili wawe na sauti. Ni changamoto kweli Mwalimu. Wakati Wazanzibari wanasema Muungano umeumeza utaifa wao, baadhi ya Watanganyika nao wamekuwa wakisema rasilimali nyingi za Tanzania Bara zimekuwa zikitoweka kuwanufaisha Wazanzibari katika kile kinachoonekana kama kujipendekeza kwa serikali ya CCM kulinda kwa nguvu zote ili usivunjike.

Wazanzibari, kwa upande wao wanaendelea kusema kwamba kwa kipindi chote hicho wameshindwa kufanya jambo lolote kwa maendeleo yao kutokana na kivuli cha muungano na kwamba kila wanalotaka kulifanya lazima serikali ya Muungano ihoji.

Nukuu la Daniel Mbega.
 
Wadau, naamini kuwa hamjambo na mmeamka salama. Nami pia Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniamsha salama. Wale wagonjwa tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapone haraka. Wale waliofikwa na mauti, tumuombe Mwenyezi Mungu awape mwisho mwema.

Mathalan, katika Ibara ya Kwanza, walio wengi wanapendekeza marekebisho badala ya neno shirikisho, wanapendekeza litumike neno Jamhuri. Pia badala ya neno Tanganyika, wanataka itumike Tanzania Bara. Halikadhalika katika Ibara ya 60 juu ya muundo wa muungano, walio wengi kwa kamati zote wanapendekeza muundo wa serikali mbili badala ya serikali tatu zilizopo kwenye rasimu ya katiba. Sababu kuu inayotolewa ni Hati ya Muungano

kwa upande wa maoni ya walio wachache, wao ni copy and paste kama ilivyo kwa walio wengi. Wao wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye Rasimu ya Katiba yaendelee. Sababu kubwa wanayotoa ni kwamba Maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni Maoni ya Wananchi. Pia maoni ya walio wachache wanatumia rejea zile zile kuimarisha hoja zao. Mathalan, wamekuwa wakitumia na kutetea takwimu zile zile za Warioba, wamekuwa wakirejea tume zile zile za akina Kisanga na Nyalali.
Kama kawaida, nitakuwa na wadau mbalimbali katika mjadala huu. Kwa upekee naomba kutambua ushiriki wa akina kibo10, Skype na wengineo. Karibu kwamjadala


Hapo kwenye nyekundu mwenye asili haachi asili yake! Kwa hiyo unataka kuwa shawishi wasomaji na wana JF kuwa hayakuwa maoni ya wananchi kama mzee wa Kaya na wanaGreen wenzake wanavyowaaminisha wa Tanganyika na Wazanzibar
 
Back
Top Bottom