yaliyonikuta leo

mtengwa

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
1,600
847
habari zenu wana JF. Ngoja niwaelezee changamoto niliyoipa leo kama msaka ajira. Kama mnavyojua ajira ni ngumu, basi kuna siku nimeingia zoom tanzania nikaona kazi ya kukusanya taarifa kampuni ya Neema Herbalist kwa malipo ya Tshs 5,000/= kwa kila taarifa ya mtu mmoja mwenye matatizo ya kitambi, unene uliozidi na matatizo ya lishe, na mkusanya taarifa anatakiwa akusanye taarifa za watu 100 kwa siku 20 hivyo ukifanikiwa unalipwa laki 5, nikaona ni kazi nzuri so nika apply baada ya siku nikatumiwa email na attachment nijaze then niende ofisini kwao changanyikeni tar 8/10, basi leo nikaenda na mzuka wangu wa kazi. Bahati mbaya nikachelewa kama nusu saa, so nikakuta ofisi imefungwa, nikapiga namba zao zote hazipatikani, nikafika jirani kuulizia ndo wakaniambia kua jamaa alikuwepo hapo kuna watu walikuja wakaongea nae then waasepa nae. Nikaanza kuwadadisi kuhusu huyo jamaa, nikagundua jamaa ni mtu wa mambo mengi nasikia alifungu darasa la ujasiria mali akazinguana na wanafunzi wake, mara ofisi yake anabadilisha jina kila mara. Nakaona kweli watu wanajua kutumia fursa za tatizo la ajira kutaka kujinufaisha wao
 
Mimi nimepata ujumbe mmoja tu. Ulichelewa kwenye appointment.
 
Hivi kama jambo ni la muhimu sana inakuwaje unachelewa tena kwa nusu saa?
Kuna watu hawapo serious!
 
mayb walimuambia afike saa 12 asubuhi. hafu anakaa mbali. teh teh

ila mm kwa nlivo na dhiki ya kazi. ningeamka saa 8 usiku nianze mdg mdg.
 
"a lazy person has tones of baseless excuses" umechelewa alafu unalaumu? aliyetangaza kazi ndo ulipenda aje kwako kukuamsha ? kwa mtindo huu wakenya na waganga watalaumiwa sana....acha uvivu...chukua hatua.
 
habari zenu wana JF. Ngoja niwaelezee changamoto niliyoipa leo kama msaka ajira. Kama mnavyojua ajira ni ngumu, basi kuna siku nimeingia zoom tanzania nikaona kazi ya kukusanya taarifa kampuni ya Neema Herbalist kwa malipo ya Tshs 5,000/= kwa kila taarifa ya mtu mmoja mwenye matatizo ya kitambi, unene uliozidi na matatizo ya lishe, na mkusanya taarifa anatakiwa akusanye taarifa za watu 100 kwa siku 20 hivyo ukifanikiwa unalipwa laki 5, nikaona ni kazi nzuri so nika apply baada ya siku nikatumiwa email na attachment nijaze then niende ofisini kwao changanyikeni tar 8/10, basi leo nikaenda na mzuka wangu wa kazi. Bahati mbaya nikachelewa kama nusu saa, so nikakuta ofisi imefungwa, nikapiga namba zao zote hazipatikani, nikafika jirani kuulizia ndo wakaniambia kua jamaa alikuwepo hapo kuna watu walikuja wakaongea nae then waasepa nae. Nikaanza kuwadadisi kuhusu huyo jamaa, nikagundua jamaa ni mtu wa mambo mengi nasikia alifungu darasa la ujasiria mali akazinguana na wanafunzi wake, mara ofisi yake anabadilisha jina kila mara. Nakaona kweli watu wanajua kutumia fursa za tatizo la ajira kutaka kujinufaisha wao

Daah hao jamaa na mimi walinitumia hizo document but nilivoona sharti lao moja tu nikagaili.
Nanukuu,"HUTALIPWA KAMISHENI YA SHILING 5000 KAMA UTALETA TAARIFA ZA MTU AMBAYE HAWEZI KULIPIA SHILLING 25000 KAMA ADA YA KUJIUNGA" nikawaona longolongo
 
Jamani ndugu zangu, hawa jamaa ni matapeli, wanatumia majina tofauti tofauti. Kwenye hiyo ofisi yao, wanatumia majina km vilw RAFIKI ELIMU FOUNDATION, NEEMA RECRUITMENT AGENCY, NEEMA HERBALIST. Owanaishi kwenye nyumba ya kupanga ambayo iko changanyikeni, nyumba hiyo haina wanaitumia km ofisi bibi ya kutapelia wowatu. Na matangazo yao hupenda kuyaweka zoomtanzania. Hivyo jihadharini ni hao watu ni matapeli, wanatumia tatizo la Ajira kuwadhulumu watanzania maskini. Hivyo tujihadhari nao ndugu zangu.
 
Mdogo wangu katumiwa hii muda huu:

Habari , tunasikitika kukutaarifu kuwa , kumekuwepo na ubabaishaji wa hali ya juu sana miongoni mwa watu wanao kusanya taarifa katika program hii. Wengi wao wamekuwa wakileta taarifa ambazo sio sahihi , ambazo hazitusaidii chochote sisi kama kituo. Tunakutahadharisha kuwa endapo utaleta taarifa ambazo si sahihi hautapata malipo yoyote, hivyo kama hauna uhakika na usahihi wa taarifa zako, ni bora ukaachana na mchakato wa kukusanya taarifa mara moja kuliko kuendelea kupoteza muda wako kwa kukusanya taarifa ambazo si sahihi. Kama unaona kuna ugumu wa kukusanya taarifa, usilazimishe wala usi rush, ni bora utufahamishe kuwa umeshindwa ili sisi kama kituo tuangalie utaratibu mwingine utakao kuwa na manufaa kwetu. Vilevile, kama unaona jukumu hili ni gumu sana, ni vyema, utuandikiea barua pepe ya kujitoa kwenye program hii mara moja ili tujue tunabaki na watu wangapi wanao weza kufanya kazi hii kwa terms na conditions zetu.
ASANTE NA SIKU NJEMA.
Neema Boniface,
Mkurugenzi Mtendaji,
Neema Recruitment Agency.
 
Jamani ndugu zangu, hawa jamaa ni matapeli, wanatumia majina tofauti tofauti. Kwenye hiyo ofisi yao, wanatumia majina km vilw RAFIKI ELIMU FOUNDATION, NEEMA RECRUITMENT AGENCY, NEEMA HERBALIST. Owanaishi kwenye nyumba ya kupanga ambayo iko changanyikeni, nyumba hiyo haina wanaitumia km ofisi bibi ya kutapelia wowatu. Na matangazo yao hupenda kuyaweka zoomtanzania. Hivyo jihadharini ni hao watu ni matapeli, wanatumia tatizo la Ajira kuwadhulumu watanzania maskini. Hivyo tujihadhari nao ndugu zangu.

me nilivyoona ofisi ni fremu tu alafu inamajina tofauti tofauti. Kuuliza majirani wakaniambia anafanya kazi mtu mmoja ndo anaifunguaga, nikaona hapo ni utapeli tu
 
Back
Top Bottom