Yaliyomo ndani ya Hukumu Kesi ya CHADEMA dhidi ya Meya Matata na diwani Chagulani iliyotolewa jana.

one activist

Senior Member
Oct 13, 2012
114
14
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali ombi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyofungua kupinga maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, ya kuendelea kuwatambua Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata pamoja na Diwani wa Igoma kuwa madiwani halali, licha ya kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho.
Katika kesi hiyo ambayo ilikuwa ikifuatiliwa kwa ukaribu na mamia ya wafuasi wa Chadema, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Aisheri Sumari, alisema baada ya kusikiliza pande zote imekubaliana na maamuzi ya Hakimu Mkazi kuendelea kuwatambua madiwani hao hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa.

Katika maamuzi yake, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanza alisitisha maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata pamoja na Diwani wa Kata ya Igoma, Adamu Chagulani, hadi pale kesi ya msingi waliyofungua itakapokamilika, ambapo kwa wakati huo aliamuru Matata aruhusiwe kuwania kiti cha Meya wa Manispaa ya Ilemela.

Hata hivyo, baadhi ya madiwani wa Chadema, Josephat Manyerere pamoja na Dan Kahungu pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho, Benson Kigaila, walidaiwa kukiuka maamuzi ya Mahakama kwa kumzuia Matata kuwania Umeya ambapo Matata alifungua kesi kuitaka Mahakama hiyo iwafunge jela wahusika hao, hata hivyo Mahakama ilitoa hukumu ya kwenda gerezani au kulipa faini kutokana na kukaidi maamuzi ya Mahakama.

Pia Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilisema kuwa katika ombi la pili la Chadema la kutaka Meya huyo wa Ilemela kuadhibiwa na Mahakama kwa kitendo chake cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama katika mahakama ya Hakimu Mkazi na kisha mahakama kuu, maamuzi yake yatatolewa Agosti 12 mwaka huu.

Hata hivyo, alisema shauri la pili lililofunguliwa na Chadema kuitaka mahakama hiyo kumuadhibu Matata kwa kutumia vibaya chombo hicho cha kisheria litatolewa uamuzi Agosti 12, mwaka huu.

Katika shauri hilo la pili, Chadema kinaitaka mahakama kuu kumuadhibu Matata kwa kitendo chake cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kisha kufungua kesi hiyo hiyo katika Mahakama Kuu.

Katika shauri hilo, wakili wa Chadema, Method Kimomogoro alidai kuwa kitendo ni matumizi mabaya ya taratibu za mahakama hivyo anapaswa kuadhibiwa.

Wakili Kimomogoro alidai kwamba mara baada ya kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu, Matata na Chagulani walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kupinga uamuzi huo, kwa kutaka kuendelea kutambuliwa kama madiwani na kupewa haki zao zote.

Jaji Sumari alisema kuwa madai ya Matata kutumia vibaya chombo hicho cha kisheria yatatolewa uamuzi Agosti 12, mwaka huu, lakini kuhusu mahakama hiyo kuingilia uamuzi wa Chadema utabaki kama ulivyo.

Jaji Sumari alisema kwamba Chadema ni taasisi ya umma ambayo lengo lake kuu ni kuunda Serikali za Mitaa au Serikali Kuu, hivyo mahakama inayo mamlaka ya kuingilia kati maamuzi yake yoyote ili kuona kama hayajakiuka haki za wananchi au wanachama wake.

[h=4][/h]
 
Mahakama za sisiemu, majaji wa sisiemu.. unategemea nini??.....
 
Kwa hali tz ilipofikia, siyo mahakama wala bunge linaweza kuaminiwa tena kusimamia haki bila kuegemea itikadi. Kilichobaki ni ama kubadilisha dola kwa kutumia sanduku la kura au kufanyike kile alichofanya Jenerali Muhammed Buhari Desemba 31, 1983 kule Nigeria.
 
Mi naona kama kama kuna maungufu ya maamuzi, CHADEMA wa appeal tu.
 
Namkubali sana Adam Chagulani mwanasiasa makini,aliejaribu kuonyesha upande wa pili wa shilling wa vyama vyetu vya siasa vya upinzani
 
Wao hao kina Matata wanaogopa nini kuondoka kwenye Chama ambacho hawakitumikii ili waende kwenye chama wanachopenda ,uchaguz uitishwe ili warudi tena kama madiwani?
 
Yaani kwa akili zenu kila chadema kinachofanya ni haki? kila mwanachama anayefukuzwa na chadema amenunuliwa na ccm? kila mwanachama anayepingana na maamuzi au makubaliano yasiyo na tija ametumwa na ccm? Tuache umbulula Meya bado anajihesabu kama mwanachama wa chadema na ndiyo maana anakata rufaa ya kupinga kunyang'anywa uanachama. Hapa mnasema chezea ccm, mara mahakama haiaminiki wala vyombo vya dola!!!!! haaaa mbona inaposhinda chadema hayo hatuyasikii jamani? au chadema ndiyo wenye haki kwenye vyombo vya dola wengine wote wahalifu?

Ushauri wangu, badala ya kukurupuka na kutoa kauli zisizo na msingi yujiulize au tutafute chanzo cha yote hayo. Ukweli chanzo ni Mbunge ambaye ni mbabe na anayetaka anachosema yeye kiwe ndich hicho hata kama hakina tija, meya akikubaliana na hoja ya chama kingine tayari ni msaliti. Tuifunze uongozi bora si uongozi chama.
 
...kaka..kupitia jamiiforums nimesikia kuwa kuna baadhi ya wachangiaji wenye mwelekeo, wa kuunga mkono ccm, na wenye kupinga au kukosoa chadema kuwa "ati" hupewa "shing" alfu 7 na kijana wa marehem mzee, brigedia moses..kama malipo...!nahisi huo ni mchezo ambao labda hata "kile chenye hedikota yake mtaa wa togo" kinaucheza..!wanasiasa wengi wanataka watumia vijana kwa maslahi binafsi ya kisiasa, na vijana wengi wamekubali hilo...!
 
Kupitia Jamii Forum fahamu kuwa kwa upande CHADEMA ni tofauti kabisa. Ndani ya CHADEMA hakuna mwanasiasa anayewaza kuwatumia Vijana kwani hao vijana ndio wanasiasa wa CHADEMA na wanaitumia CHADEMA kufikia malengo ya ukombozi wa pili wa taifa.
 
.........kwa CHADEMA ni tofauti kabisa. Ndani ya CHADEMA hakuna mwanasiasa anayewaza kuwatumia Vijana kwani hao vijana ndio wanasiasa wa CHADEMA na wanaitumia CHADEMA kufikia malengo ya ukombozi wa pili wa taifa.
..mkuu! tutakubaliana jambo moja tu nadhani..kwamba ccm ni mafisadi..! lkn wengi wa wanasiasa wa tanzania ya leo wanaeleweka..!.."hapa vijana wanashangilia kubadilishana soksi chafu".... ni kwakukipigania kupata katiba mpya na bora nje ya ushabiki wetu wa vyama vyetu vya kisiasa, (na wa wanasiasa wetu) ndio tu, tutapata kile ambacho tunaamini ni bora na heri kwetu..! si C.CM., wala si CHADEMA, wala si CUF, wala si NCCR, na wala si chama chochote cha siasa kitakachoweza kutupa kile ambacho watanzania tunakitaka..!
 
Kwa kweli mifumo ya utawala na ile ya kutetea Haki za wananchi hapa Tz kwa sasa zime collapse kabisa. Hivi Matata anaweza kusema atamsadia mwana Ilemela wa kawaida kwa nafasi hiyo aliyonayo na kwa mazingira haya kweli hii inadhihirisha kwamba watu wamekwisha jichokea hata kumuogopa Mungu. Kesi imejaa siasa tupu utashangaa mpaka ikamilike itakuwa tumefika uchaguzi mwingine 2015, wanataka kuwaaminisha watu kwamba haya yanatokea kwa vile walichagua CDM. Hivi wananchi tutachezewa hivi na wanasiasa wenye uchu na madaraka hadi lini? hata hivyo kila jambo lina mwanzo na mwisho wake!
 
Kuna haja ya chadema kuunda kitengo maalumu cha kushughulikia migogoro ya namna hii inapojitokeza kwa njia za kidipromasia. Si wakati wote mitazamo tofauti ndani ya chama ni usaliti, wakati mwingine ni namna ya kukijenga chama.

Lakini pia lazima tuanze kufukiri ni kwa namna gani maamuzi yetu (kufukuza) yanaathiri shughuli za maendeleo katika maeneo husika, tufikirie gharama za kurudia uchaguzi, lakini kikubwa zaidi tufikirie thamani ya muda (time)

Ni imani yangu kwenye katiba mpya wadau watakuwa wameliangalia hili ili diwani au mbunge akishachaguliwa awajibike kwa wananchi waliomchagua na sio kwa chama alichokiwakilisha, na kwa mtazamo wangu cdm wangeweza kuwa wa kwanza ku practice hili mapema.

Si lazima cdm ifanye kama ccm, vinginevyo wananchi hatuwezi kuona tofauti ya vyama hivi
 
Ndugu hapa inaonekana kuwa wengi wa wachangiaji/wakosoaji wa chadema hawajui ni kwa sababu gani Matata na Chagulani walivuliwa uanachama wa chadema.kwa ufupi hakukuwa na adhabu nyingine kwani wawili hao walikwisha onywa mara kadhaa na hawakutaka kujirekebisha;kibaya zaidi Chagulani alikuwa chini ya uangalizi kwa miezi sita na akafanya kosa la makusudi.
 
..mkuu! tutakubaliana jambo moja tu nadhani..kwamba ccm ni mafisadi..! lkn wengi wa wanasiasa wa tanzania ya leo wanaeleweka..!.."hapa vijana wanashangilia kubadilishana soksi chafu".... ni kwakukipigania kupata katiba mpya na bora nje ya ushabiki wetu wa vyama vyetu vya kisiasa, (na wa wanasiasa wetu) ndio tu, tutapata kile ambacho tunaamini ni bora na heri kwetu..! si C.CM., wala si CHADEMA, wala si CUF, wala si NCCR, na wala si chama chochote cha siasa kitakachoweza kutupa kile ambacho watanzania tunakitaka..!

Katiba mpya ni jibu, lakini ni chama gani chenye utashi wa kuitumia hiyo katiba ikishapatikana? Bila shaka chama hicho sio c.c.m ila ni chadema. Angalau chadema kinawalazimisha vijana kufua soksi chafu kabla ya kuzivaa{tumia mfano wa kuwafikuza Matata na Chagulani}na kiawatafutia vijana soksi mpya;KATIBA MPYA
 
Jamani mimi nadhani tatizo lipo kwenye sheria zetu, maana hata nikitazama records za nyuma tunaona kwamba Hamad Rashid Mohammed mbunge wa Wawi ameendelea kuwa mbunge baada ya kufungua kesi dhidi ya kuvuliwa kwake uanachama na kesi ya msingi haijaisha, na ni kwa utaratibu huohuo Kafulila aliendelea kuwa mbunge baada ya kukimbilia mahakamani, na kwa Matata nilitarajia hili pia.
 
Back
Top Bottom