bissmark marktosh
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 233
- 47
:what::what:Sisi UKAWA kama wale nyumbu wa Serengeti, tumeumia sana na campaign ya jana ya CCM. Hatukudhani kama CCM bado inamashabiki wengi kiasi hicho. Tulikuwa tunawatisha watu na mafuriko yetu na kuwaaminisha WATANZANIA sasa wameichoka CCM. Sasa yaliyotokea jana yanadhidi kutupa kazi kubwa ya kufanya. Kwa yaliyotokea jana, tunawadanganya vipi tena hawa WATANZANIA. Je tuitupe karata yetu ya mwisho ya KINGUNGE? Kwani tulipanga KINGUNGE ahame CCM mwishoni ilikuchangamsha mambo? Vipi sasa tuitupe hiii karata mapema?
Pamoja na hayo mgombea wa CCM ana nguvu na ari ya kuibadilisha nchi. Anaongea sera tu. Maneno yake yanaingia mpaka kwenye cell za damu. Sasa nikianglia mgombea wetu hata kutaja jina la mke wake ni kazi kubwa. Anaishia kusema tu 'narudia' maneno yale yale. Sasa najiuliza huyu mgombea wetu wa UKAWA ataweza kweli kuhutubia na kujenga hoja kwa angalau dakika 15? Sijui... lakini nimehakikishiwa kuwa yule dakatari wake wa Ujerumani amekuja na sindano nyingi tu za kumchoma ili awe fit. Kwa hiyo ni matumaini yangu atahutubia kwa mda kidogo.
Sisi UKAWA bado tunakajiimani hii miezi miwili tutaandikwa sana kwenye magazeti. Iliyobaki heri tuoshe nyota kwa kuuza sura. Ila uhakika wa kushinda Oktoba umeyeyuka kama icecream Za AZAM.