Yaliyojiri: Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari - Nov 26, 2013

Mnyika kaamua kuwasaliti watanzania na kujiunga na wahafidhina.

Kawaida yake hata post za nyuma tumesoma mambo mengi juu ya unafiki wake, UBUNGO asahau tena,
Ahamie Arusha jimbo ligawanywe naye babu yake atampa.
 
Mheshimuwa John Mnyika, Tundu Lissu na Benson Kigailla ndio wazungumzaji wakuu.

Mnyika - amewaleeza waandishi kuwa sekritarieti ya chama ilikaa kikao chake jana kujadili mambo kadhaa ndani ya chama.

Ameeleza kuwa wahusika wamesha andikiwa barua zenye tuhuma zao 11 wanazotakiwa kuzijibu ndanj ya siku 14.

Ameeleza kuwa press conference waliyofanya wamejitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao.

Benson Kigailla anaeleza mikakati inayoendelea kwenye kanda ambayo kimsingi ripoti zililetwa kwenye kamati kuu.

Anasema mpango na programu ya chadema ni msingi pamoja na M4C kanda unaendelea kwa mafanikio makubwa kwani misingi inaendelea kuundwa na mpaka sasa zaidi ya wakunzi elfu tisa kutoka katika kanda mbalimbali wameshafundishwa.

Anaeleza kuwa kuna timu nne zimeundwa kwenda kwenye kanda mbalimbali kukagua misingi iliyokwisha simikwa.

Ziwa Mashariki misingi 3069 kati 7098

Ziwa Magharibi 3840 kati 9757

Kaskazini 3278 kati ya 8417

Juu kusini 2113 kati ya 10,857

Magharibi Kata 235 kati ya kata 315

kanda ya Kati Kata 363 kati ya 495

Kanda Kusini 219 kati ya 387

Kanda ya Pwani misingi 846

Tundu Lissu.

walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba na maadili ya uongozi, kuvuliwa kwao nafasi zao hakuhusiani na mambo ya PAC wala kuuza nafasi zetu za wagombea kwa maccm, wala kutokushiriki kwenye ziara za chama.

anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu"

anasema chadema haijaanza kufanya maamuzi magumu leo, ilishafanya hivyo kwa Dr Walid Kaburu na kwa Chacha Wangwe na mara zote vyombo vya habari vimekuwa vinaandika kuwa CHADEMA yapasuka, mara CHADEMA inakufa lakini kipindi chote haijawahi kufa wala kupasuka, na hata kwenye hili haitakufa kama ikitokea kamati ikiwafukuza.
Watu wanakulalamikia hapa una matatizo gani????????????????
 
tundu lissu.

Walichokifanya kina zitto na kitilla ni "diversion" mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba na maadili ya uongozi, kuvuliwa kwao nafasi zao hakuhusiani na mambo ya pac wala kuuza nafasi zetu za wagombea kwa maccm, wala kutokushiriki kwenye ziara za chama.

Anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu"

anasema chadema haijaanza kufanya maamuzi magumu leo, ilishafanya hivyokwa dr walid kaburu na kwa chacha wangwe na mara zote vyombo vya habari vimekuwa vinaandika kuwa chadema yapasuka, mara chadema inakufa lakini kipindi chote haijawahi kufa wala kupasuka, na hata kwenye hili haitakufa kama ikitokea kamati ikiwafukuza.

penye red..
wote tunajua kifo cha chacha wangwe kilitokea baada ya kuutaka uenyekiti kumbe kilichomuua chacha wangwe ni kuutaka uenyekiti wa CHADEMA ambao mbowe hataki kuuachia adi leo.

Mungu mlinde shujaa wa demokrasia ZITTO ZUBERY KABWE wasije wakamfanyia walichomfanyia CHACHA WANGWE KWA KUTAKA UENYEKITI..... lakini mwsho wa mtei na mbowe kufanya chadema saccos yao umefika
 
Duh naona chadema nia yao, wanapima upepo..

CDM ni chama cha wananchi,mamluki yeyote ajue hana nafasi.cdm inauwezo wa kuchukulia hatua za kinidhamu kwa wanachama wake wanaokiuka taratibu zake tofauti na maccm yaliyoshindwa kuvuana magamba wala kuwavua madiwani wa bukoba kwa kuhofia kushindwa katika chaguzi.CDM 4VER
 
huwa nakukubali sana Mtoi na hili bandiko lako linazidi kuwafunua macho wale wanachama wasio tazama vitu kwa jicho la tatu, wasijue ni jinsi gani Zitto anavyozidi kufirisika kila siku kisiasa, asijue wapi anapotoka na anapoenda, kwa sisi wanachama tulio hai tushajua anatafuta huruma yetu lakini asipo tumia njia sahihi tutamwacha hazidi kutumbukia shimoni, kila la heri Zitto.
 
Dr Slaa ni mwanasiasa mnafiki. Hili sakata yeye kama katibu mkuu ndiye anayestahili kulisimamia, lakini kwa sababu ya unafiki wake anajifanya kamuachia Tundu Lissu, ili lawama zote ziwe kwa Lissu. Leo wamemuingiza na Mnyika.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misigni ya kilaghai...

Bila kumtaja Slaa tundu lako huko nyuma haliendi chooni?
 
penye red..
wote tunajua kifo cha chacha wangwe kilitokea baada ya kuutaka uenyekiti kumbe kilichomuua chacha wangwe ni kutaka uenyekiti.

mungu mlindo shujaa wa demokrasia zitto zuberi kabwe lakini mwsho wa mtei na mbowe kufanya chadema saccos yao umefika

SIASA NYEPESI kachukue buk 7 zako kwa nepi.
 
THE BIG SHOW mbona hajatolea ufafanuzi wa zile fedha za TISS , zilizopelekwa Ujeremani na kuzigawa kwa M-Pesa kwa watu wake???
CDM hatutavumilia wasaliti na mamluki wa CCM, WATUHARIBIE. CHAMA!!!
Tuko macho M/Kiti Mbowe ana Baraka zoote za wanachama!!!
 
Last edited by a moderator:
Tundu kweli akili yake imejaa matundu,
Sasa ndo kachambua nini?
Milembe kweli panamuhitaji kwa haraka zaidi
 
Kweli ndio maana pale kikurunge jimboni kwetu Kibakwe umeme hakuna na ukienda Tanesco wanakwambia Simbachawene kasema msiwekewe umeme maana bei itapanda
 
Live live huwaga tamu, unapata kitu bila chenga. Sometimes hata facial expression tu huwa zinasema mengi zaidi kuliko hata maneno.

Asante kwa kutujuza.
 
Kwa sababu wewe ndiye unayegawa ubunge? hujitambui!
mwazo wa kukufaham nilifikili ktk wenye uwelewa mkubwa Cdm humo kumbe na wewe ni mbulula aiseee, unaunga mkono kukimaliza chama kwa huruka za wapenda madaraka? au na wewe umetoka Mombasa kutafuta maitaji? Zitto bila Chadema hakuna kitu, waliobaki wote Viazi tu.
 
Hupigi kura peke yako wewe mbulura wa lumumba.acha kupiga yako hiyo 1,makamanda tutampigia za kutosha.

Mimi ni mwanachama wa CHADEMA huenda kama wewe, lakini tunapishana kimtazamo kama ulivyojibu hapa..Yote katika yote tukiendelea na malumbano yasiyo na msingi wa hoja...hakika 2015 hatutafikisha malengo.
 
Mnyika angekuwa mbunge tangia 2005 kama si hujuma zenu ccm ila 2010 watu walisema inatosha kuhusu UBUNGO JJ ataendelea kuwa mbunge labda aamue yeye kuacha kwani jimbo la Ubungo Mnyika anakubalika ndo chimbuko la CDM sasa sijui unataka watu wabara waje mpigie kura? MNYIKA SPECIAL FOR UBUNGO CONSTITUENCY.

Kawaida yake hata post za nyuma tumesoma mambo mengi juu ya unafiki wake, UBUNGO asahau tena,
Ahamie Arusha jimbo ligawanywe naye babu yake atampa.
 
Last edited by a moderator:
Hizo tuhuma 11 ambazo Mnyika anasema ni zipi? yaani hiki chama ni usanii mtupu
 
Back
Top Bottom