Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

nimeangalia taarifa ya habari mlimanitv wameyalipua magamba kwa kuonesha magari yaliyokodiwa kupeleka watu jangwani
hakika ccm kwisha habari yake
 
Leo ndani ya jangwani mambo yalikuwa mabaya kwa ccm baada ya waziri magufuli kutangaza kuwa wanaotaka kurudisha kadi na kujiunga upya wajitokeze, watu wachache sana na hawafiki hata 100 na hakuna hata mmoja aliye enda kujiunga upya, baada ya kuona hali ni tete ndipo nape akalopoka kuwa hawapokei wanachama upya mpaka baada ya uchaguzi ndani ya CCM.

Kwaiyo wale waloenda pale walipigwa fimbo kufika pale hawakwenda kwa hiyari Yao?!
 
Huo ni mkutano wa kisiasa mambo yakiwa mahakamani hutakiwi kuyaongelea hadhalani. Acheni mambo ya ushabiki ambao hauna tija. Kama kitu kizuri lazima usifie. Kuna sometime Mungu anatupa laana kutokana na kuongea mambo yasiyo na maana. Kwanini tusikae na tuwaombee viongozi wetu?
Utakuwa unatania, nani awaombee! kwanini wasitubu na kuomba wao wenyewe?
 
We ni noumaa like like like
Hizi ndizo kauli za wasichana wanaobishana sokoni kuhusu mvulana yupi ni mzuri. Na ccm imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Ccm inawahadaa watu kama wewe mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na ccm. Wanapewa mimba, wanazaa ufukara na kisha wanatelekezwa kwa maisha duni!

Nionavyo mimi:
Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!
 
Leo utalala hoi mkuu.
Ni kweli mkuu ndio nafika nyumbani nasubiri tamko la UAMSHO kwani Waislamu wametukanwa bila sababu yeyote makanisa wachome magamba lawama ziende UAMSHO sisi CDM tunawaheshimu na kura zao ni muhimu kwetu lakini nyinyi mnawaita majambazi mtakoma mwaka huu
 
nilihudhulia mkutano wa chadema jangwani,nilicho gundua ni kwamba chadema ni wazuri wa kulalamika matatizo yaliyopo ila hawawezi kusema wakichukua nchi watatatua vipi matatizo hayo! one major weakness of chadema wazuri wa kulaumu but they are poor to walk the talk hata majimbo waliyo chukua kama iringa mjini,mwanza,ubungo,msoma,mbeya bado wabunge wao wamekaa mkao wa kulalamika utadhani sio wabunge! leo jangwani mkutano wa ccm nitahudhulia nijue udhaifu wa ccm na uzuri wao!


Tena huu ni udhaifu mkubwa sana na si kama hawaujui wanajua sana ila hawana la kuwaambia watz. Wao sera yao ni ufisadi tu hawana jipya na lingine ni kulalamika lalamika ili waonyeshe wana uchungu na nchi.mi CDM namuona Zitto tu wengine wo
 
kwa unafiki aliouonyesha kwenye swala la richmond hakika huyu si mtetea haki za walala hoi ikumbukwe leo watanzania tunalipa mabilioni kwasababu ya unafiki wake...sema anauafadhali ukimlinganisha na walioko ndani ya ccm

Kwahiyo ushauri wako sasa aache tu mambo ya haribike sababu ya richmond? wewe ni Agent wa mafisadi!
 
Kwa ufupi Kinana alisema CDM hawafai, hawawezi ili hali juzi ilitaka kuvunja serikali kutokana na hoja ya Zitto kabwe ya saini 70 hadi JK kubadilisha baraza la mawaziri. Kama CDM hawafai , hawana ubafu inakuwaje CCM wanaandaa mkutano ambao lengo lake kuu ni kujibu mapigo? wanaogopaje Chama kisicho faa si wangejikalia wakaendelea na shughuli zao? Unafiki huu wa akina Kinana na wenzake wa kuganga njaa kwa kuwadanganya waTZ ndo umeifikisha nchi njia panda
 
Kupanda kwenye malori hao ni desturi yao toka miaka ya sabini mwanzoni nilipoanza pata akili, mwlimu alikuwa raisi tulikuwa wanapandishwa kwenye malory kwenda Airport kumpokea pia kwenda uwanja wa Mkwakwani.
 
Pinda amesema leo kibaha kuwa VIWANDA VINAZIDI KUFA kuna watu wanakula kama mchwa!haya jangwani wassira anasema tunapata maendeleo!tumwamini nani?
 
Kupanda kwenye malori hao ni desturi yao toka miaka ya sabini mwanzoni nilipoanza pata akili, mwlimu alikuwa raisi tulikuwa wanapandishwa kwenye malory kwenda Airport kumpokea pia kwenda uwanja wa Mkwakwani.
 
Je mawaziri waliofika pale walikuwa wanantumia magari yao ya uwaziri au waliletwa na FUSO kama wengine? Iwapo walikuwa wanatumia magari yao ya uwaziri, je sheria inasemaje kuhusu matumizi ya mali za serikali?
 
yaani pale
  • 25% wako kikazi, kwamba ni viongozi chama katika nafasi mbalimbali au watu wa usalama (kasoro polisi, hawa wamenawiri sana, kweli wanakula mema ya nchi)
  • 70% wameletwa na mabasi tena hawa walikua wanashuka unajiuliza mara mbilimbili kama wanaelewa hata nchi inavoendeshwa wengi wana afya mbovu kuonesha hali yao ilivvyo ngumu, wamekonda na wako dhoofu sana, sijajua kitu gani kiliwafanya waje, labda ni watu walikusanywa wakapewa pesa, wengi walikua na tshirt za ccm mpya ila ni za wakati wa uchaguzi wa 2010, inaelekea kuna stock ilibaki ndio wametumia
  • 5% ndio kama sie tulioenda kuangalia hawa wenzetu wanakipi kipya

Mkuu wengi walienda kwa ajiri ya mgao na pilau,
watu wana maisha magumu sana,
hiyo ndio sababu ya kwenda mkutanoni.
 
Nilichoona, wengi ni "wanachama wao" maana hawakuvuta watu wengi wasiokuwa na rangi zao, na hii ni hatari maana kama ikitokea hao "wanachama wao"wakabadilika basi watakuwa hawana mtu wa kuwasikiliza. Pia wao inaelekea kadi za maana zinazorudishwa ni za wapinzani wao wakubwa, hawajui kuwa wapiga kura 2015 hawatopiga kwa kadi za chama bali chama kitakachoonekana kuwakomboa na haya yote watu wanajifunza katika kipindi hiki cha mpito kuelekea ukombozi wa kweli 2015. Hizo kadi zitaasaidia kuchagua viongozi wa chama lakini siyo wa nchi, daftari la wapiga kura na kitambulisho cha kupigia kura ndivyo vitu vya maana, labda ingekuwa vizuri wafanye kampeni ya kukusanya vitambulisho hivyo
 
Lowassa mwamba wa kaskazini hakuwepo ccm kwisha!!!!!!

Hakutaka kujiabisha maana anajua hawa jamaa wanajibu kujitetea vitu ambavyo viko wazi, badala ya kuvifanyia kazi kujinasua wao wanafikiri wapinzani wao wanatunga atu, waache yawakute.
 
Back
Top Bottom