Yaliyojiri ktk Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, uwanja wa Taifa - Dar es Salaam

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,957
1,327
Leo ni leo, Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA inaadhimsha miaka 50 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1964 ambapo jamhuri ya Tanganyika iliungana na jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Kwa wale wasiopata kwa sasa matangazo live kwa njia ya Tv wanaweza kuangalia matukio ya sherehe za Muungano LIVE ONLINE kupitia LINK hii ya IKULU Yetu.

http://www.ikulu.go.tz/

Maadhimisho hayo yataongozwa na rais wa Tanzania, Mh. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Stay tuned, fuatilia uzi huu, tutawarushia updates zote pamoja na picha. Tbc1 watarusha live pamoja na tbc fm.

=====
Viongozi mbalimbali wa kitaifa wanazidi kuingia hapa, mawaziri, mabalozi, viongozi wakuu wastaafu, diplomats, watu mashuhuri, wabunge na wanasiasa maarufu.

- Vikosi mbalimbali vya ulinzi vinazidi kujiimarisha hapa, vinatumbuiza kwa mbwembwe kweli kweli, ni kivutio tosha hakika...watoto wa halaiki wapo upande wa mashariki mwa uwanja wakiwa very smart na mavazi yao ya bendera ya taifa...very interesting

- farasi haooooooo.

- Mawaziri wakuu wastaafu wameingia hapa kwa bus maalum wameshuka wanapanda jukwaa kuu.

- Kuna vijana wanaendesha baiskeli ya mguu mmoja apa, very interesting...ni ustadi wa hali ya juu sana.

- Marais wa nchi jirani kama Yoweri Museveni (Uganda), Uhuru Kenyatta (Kenya), Joyce Banda (Malawi), Joseph Kabila (DRC) na marais wa Burundi, Msumbiji n.k wamehudhuria!

-
Uhuru Kenyatta naye amehudhuria. Kati ya marais wote wa nchi za Afrika ya Mashariki, ni Paul Kagame pekee hajahudhuria kutokana na sababu zinazojulikana

- Naam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio ameingia uwanjani hivi sasa na Unaimbwa Wimbo wa Taifa na Mizinga 21 kupigwa!

- Kamanda wa Gwaride ametambulisha guards mbalimbali zilizoshiriki kwenye maadhimisho haya na sasa Mheshimiwa Rais anapita kwenye guards hizo tayari kwa kukagua gwaride.

Amri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete anakagua Gwaride.

- Rais Kikwete amemaliza kukagua gwaride na sasa ameelekea sehemu yake ya kuketi,anasalimiana na viongozi mbali mbali wa kitaifa pamoja na viongozi wengine wa kimataifa, Naam amemaliza kusalimiana.

Gwaride limeanza na viongozi pamoja na raia wengine wanasimama tayari kwa kuimba wimbo wa taifa.
kukosa kuona sherehe hizi ni kukosa uhondo kweli kweli
......
gwaride linapita kwa mwendo wa haraka hivi sasa
....
mwendo wa kukimbia huo.......full raha, guard ya komando na wanamaji
.. Guard maalum ya marine na komandoo wametoa heshima hapo, mwendo wao ni wa kuvutia kweli kweli
..kikundi cha makomandoo kinakuja kuonyesha ukakamavu wa jinsi ya kupambana na adui kwa mikono
..hii ni dojo hakika, gusa unate....mtindo wa karate, an armed combat na kuvunja vitu vigumu kwa mikono na miguu

Hawa ndio makamanda wa kweli,anapigwa, ananyanyaswa na kuwa tortured hata km anekamatwa mateka hatoi siri za nchi
......hivi sasa zana vita zinapita, zinaanza kamandi za nchi kavu
Sherehe za Muungano Live online pitia LINK hii hapa chini uungane nasi Watanzania.

Jamii forums ni sehemu ya kuhabarishana na pia ni kisiwa cha kuchota uelewa.

- Sasa ni magari ya deraya , zinayotumika kwa mapambano ya mjini
- Zinapita infantry fighting vehcle
- Vinapita vifaru vya kisasa vinavyotumiwa na mataifa makubwa duniani, vyenye uwezo wa kupiga masafa marefu na kuweza kuelea baharini,
- Zinafuata zana za uhandisi wa medani...
- Yamepita madaraja ya kivita, vikwazo , boat na madaraja ya haraka yanayotumika kuvushia majeshi
- Zana za madaraja ya kuvushia majeshi rafiki
- Haya magari ni sehemu ya daraja

- Sasa yanapita mamitambo ya kutegua mabomu ya kutegwa ardhini pamoja na vikwazo mbali2

- Mitambo ya kuchimbia visima vya maji
- M itambo ya kusafisha maji
- Sasa ni mitambo ya ujenzi wa barabara
- Sasa ni mizinga apa hatareeeeeeeeee
vifaaa vya kuongozea mitambo.....balaaaaaa
- Mizinga mikubwa mikubwa na ya kisasa kabisa inayotumika duniani hiyoooooooo, inatumia mfumo wa kidigitali

- Sasa inakuja mitambo na zana za jeshi la anga, kudungulia ndege za angani
- Silaha ng'ang 'anizi
gari zilizobeba boat, za kisasa, zenye kasi na mitsmbo ya kisasa.
Iheshimuni tz jamani
imepita mitambo ya radar za kiuchunguzi majini na angani.

- Sasa zinapita ndege za kivita zenye bendera ya taifa
- Zimepita ndege ndogo ndogo na kubwa na za usafirishaji na na ndege ya serikali
imepita ndege kubwa sana a kivita.
Sasa ni ndege za ulinzi wa rais zimepita.

Sasa makomandoo wanapasha kwa ajili ya kupokea parachute/ toka angani...parachute zitashuka hivi punde,
hatareeeeeee gari inatoa moshi wa kijani wa kivita
- Ndege vita zimepita apaaaa
- Ndege zitapitá kwa mtindo wa rolling

- Parachute hizooooooooooooooo askari wa kwanza tayari ameshuka na parachute daaahhhhhhh tanzania yangu weeeeeee.
Parachute ya pili sasa askari huyoooooooooooooo anashuka
....wa tatu huyoooooooooooooooooooooo si mchezoooo.
Askari wengine wawili wanashuka, mmoja bado yuko angani.
Kikundi kizima kiko ardhini hivi sasa, hatareeeeeeeeeeeeeeeee.

Rais amewaita askari/ wanajeshi walioshuka na parachute na kuwapa mkono, wamepiga salute za nguvu apa na hatimaye wamemaliza na kuaga kwa salute.

- Kinachofuata sasa ni maandamano ya watu waliozaliwa mwaka 1964,pikipiki na baiskeli kisha farasi waliofunzwa.....bendi itakayoongoza maandamano imeingia haa uwanjani.

- Farasi haoooooooooooooooo wanapita ni askari wa kikosi cha farási,
farasi amependeza hakika

- Wapanda pikipiki wametoka mikoa yote ya tz, wamezunguka nchi nzima wanahitimisha kwenye muungano wetu leo

waliozaliwa mwaka 1964 wanapita, wamependeza kweli, wamerusha njiwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa rahaaaaaaaaaaaaa haha haaaaaaa.

wazanzibar wanacheza kwa rahaaa.

- Kikundi cha vichekesho, sharo amepiga tai juu ya tisheti ha haaaaa bonge ya kiatu af ina midoli.

- Sasa wanafuata vijana wa halaiki kutoka pande zote za muungno, bara na visiwani..wataonyesha maumbo mbalimbali ikiwamo jina la tanzania, mwaka 1964 pamoja na ujumbe anuwai.
Wanatengeneza umbo la miaka 50 ya muungano.
Wanatengeneza umbo la ramani ya tanzania rahaaaaaaaaa

- Vijana wanaruka sarakasi hapa
- Picha za viongozi wetu walioasisi muungano wa tz pamoja na bendera ya tz
- Wametengeneza umbo la kuashiria miaka 50 ya muungano
- Vijana wametengeneza umbo la meli kuashiria kuimarika miundombinu ya usafiri na usafirishaji hapa nchini.
- Wanatengeneza maumbo ya kiuchumi, kilimo na kitabu cha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali
.
-Wamecheza ngoma ya asili toka mkoa wa pwani iitwayo ngodo na sasa wanacheza ngoma ya asili toka mkoa wa Kusini Unguja inayoonesha mama akisuka ukili.

- Sasa ni mazoezi a viungo huku wakitengeneza maumbo mbalimbali,sasa ni baiskeli zenye ringi moja zinapita huku vijana wakiendelea na utengenezaji wa maumbo mbalimbali.

- Style ya kurusha kofia nyingi kwa mara moja minogeshoooooooo
- Wwanatengeneza mnara mkubwa wa ajabu na kupeperusha bendera ya Tanzania.

- Yupo rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais wa Burundi, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na rais Kabila wa DRC.

- Sasa wanaonyesha vyombo vya ulinzi na usalama, kuonyesha ukakamavu, amani na upendo, wanafanya mazoezi ya viungo ili kuonyesha sura ya zana za kivita,ndege za masafa na deraya
.

- Watoto wa maonesho ya halaiki wamemaliza sasa yanafuata maonesho ya mbwa wenye mafunzo maalum.

- Hawa mbwa inabidi atembee upande wa kushoto wa askari tayari kwa kupambana na uharifu.Mbwa hawa wana uwezo wa kukakamata waharifu kwa ukamataji salama na ukamataji harifu.

- Mbwa wameambiwa wakae chini na wametii amri,wameambiwa kulala chini pia wakalala.Mbwa hawa wanaonesha kuwa na afya njema na wenye nguvu.

- Kuna mbwa kwa ajili ya kugundua madawa ya kulevya,doria,mabomu yaliyotegwa na kukamata waharifu.
...kuna mbwa wa kugundua madawa ya kulevya, kulinda mipaka nk
...sasa ni onyesho la jeshi la magereza,wanaonesha shughuli mbalimbali na harakati za kukabiliana na wafungwa na mahabusu, mpambano mkali sana hapa
.......askari wanapambana na wafungwa na mahabusu, vibaka wasiosika,wakorofi na wahalifu sugu...lengo ni kuwakamata na kuwpeleka katika sehemu zao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa...harakati za kuzuia uhalifu magerezani

.......mchanganyiko wa wasanii mashuhuri wote nchini, wa mziki wa injili,nyimbo za asili bongo fleva,taarabu,mashairi,music wa dansi nk wametumbuiza kwa kuimba wimbo wa tanzania......mrisho mpoto anashairisha hapa kwa tungo zake tata......wasaniii wote wamejitambulisha apa kwa mbwembwe kweli kweli..

.........bado wanatumbuiza akina christina shusho,ommy dimpo,flora mbasha,dully sykes,diamond,keisha,hadija kopa,msechu,shar,queen darlin,chege ,mwana FA ,mwasiti ,luisa mbutu,kalala junior,rais wa manzese,dogo asley,nk

;;;;;:::::;;;///////))))))))((((((((( mh Rais anatoa shukran sasa anawashukuru watz wote kwa kudumuisha muungano,kujitokeza kw wingi uwanjani,jeshi la polisi,jwtz,magereza,ffu wanajeshi kwa maonyesho,vijana wa hlaiki kwa maonyesho mazuri..wataalam wa halaiki,waliobuni sura ,balimbali za maonyesho...asanteni saaaana

.......tunawashukuru sana wasaniii kwa kuungana na kuimba wimbo wa pamoja
.......anawashukuru viongozi mblimbali kutoka nje ya nchi ...
.....anawashukuru wakuu wa nchi mbalimbali waliohudhuria... Anaelezea kwa ufupi historia ya maadhimisho haya ya muungano kwamba ilikuwa ni siku kma ya leo miaka 50 iliyopita ambapo viongozi waasisi wa tanganyika na znz waliunganisha nchi zao n kupata tnzania.....

...........leo tunasherehekea vitu vikubwa viwili....tunamsherehekea pamoja na mawao yake mwk nyerere na abeid karume
......kwa mfano wa muungano huu muungano wa Afrika unawezekana
anawatambulisha
1,mfalme wa lesotho
2.mfalme mswati wa 3 wa swaziland.....anaelezea kdg historia ya swaziland na lesotho..
3.rais yoweri museveni waugsnda aliyejifunzia kila kitu hapa tanzania,amesomea udsm
4.rais pieree nkutunzinza wa burundi
5.rais pekee mwnamke mama joyce banda w malawi,mwenyekiti wa sadc wa sasa
6.rais kijana kuliko wote ukanda wa afrika mash. Uhuru kenyatta wa kenya
7.makam wa rais wa nigeria mohamed sambo...nigeria ilikuwa karibu sana na tz wakati wa kupigania uhuru wa nchi zetu
8.makam wa rais nchi jiran na sisi dk gaiskoti wa zambia
9.ibrahim mahlap, waziri mkuu wa misri
10. Waziri mkuu wa msumbiji dr clementio vaquina
11.piere hapukubamba wa rwanda...hatuna ugomviiiii
12.makam mwenyekiti wa bunge la china chen jang chi
13.spika wa bunge obin minaff
14.zimbabwe ni waziri wa mambo ya nje simbanashe mumbegeshe
15.waziri wa mambo ya nje wa komoro hassan
16. Shelisheli vicent mariton pm huyu
17. Waziri w maendeleo shevdent gilman
18.oman ni dr rawia bin said waziri wa elimu y a juu
19. Ethiopia waziri wa mambo ya nje dr tedrose abanin gebroyesus
20.sudan kusiniwaziri wa mambo ya ndani na hifadhi ya wanyama. Alley aiyemi aleiwo
21.angola brnito bartazar iyoko....
22.A.u imewakilishwa na erastos yanche
23....
24.mauritius balzi wao
25.botswana jina gumu kdg hon.twelonyana olefant mwanamke huyu
26.balozi abdulkarim kingsley
27.jamaica
28. Madhirika ya kimataifa ADB makam wa rais yupo
29.EAC .dr richard
30.france, balozi wao
31. Korea kusini balozi
32.brazil
33.uholanxi
34.uingereza
35.qatar
................
36. Rais mstaafu wa namibia sam nuyoma aka sam mwakangale
37.
 
Watu ni wengi sana hapa uwanjani, na wanazidi kumiminika, uwanja utafungwa endapo watu watajaa sana
 
Burudani mbalimbali zinaendelea hapa, huku jwtz wakiwa tayari kuonyesha vifaa mbalimbali,zana za kivita na deraya
 
Maadhimisho yanaanza rasmi saa tatu kamili ambapo ndio rais ataingia na kukagua vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi kisha kupigwa mizinga 21
 
Ni maadhimisho ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar au Maadhimisho ya Miaka 50 ya muungano wa Majeshi ya Tanganyika na Zanzibar?

Au ni miaka 50 ya Uongo unaolindwa na Majeshi?

Mkuu wewe Kilaza usibishe bwana.
Au ndio nyinyi mumetaka waraka wa muungano ulipoletwa mukatafuta chengine.

Naamin umekuwa frustrated tayari na hapa ndio inaonesha kama hivi vyama vengine havina nia njema na muungano.
 
Ni maadhimisho ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar au Maadhimisho ya Miaka 50 ya muungano wa Majeshi ya Tanganyika na Zanzibar?

Au ni miaka 50 ya Uongo unaolindwa na Majeshi?
Siku hizi kuna vichaa wanavaa suti na tai. Hii comment ni ya watu wa aina hiyo
 
Mkuu wewe Kilaza usibishe bwana.
Au ndio nyinyi mumetaka waraka wa muungano ulipoletwa mukatafuta chengine.

Naamin umekuwa frustrated tayari na hapa ndio inaonesha kama hivi vyama vengine havina nia njema na muungano.

""Jifunze kuandika kwanza ndiyo uanze tena kujifunza namna ya kujenga hoja na si kutokwa na mapovu bila kipigo""
 
Sipo kaka tunawakilisha huku vijijini kufuta ujinga unaoenezwa Na Umoja wa Katiba ya Wahuni UKAWA

""Sikushangai sababu utafiti umeshaonesha Tanzania is among the Top 10 Countries in Africa with the Lowest Populalion IQ.Hivyo endelea na huo ujinga wako sababu si kosa lako!""
 
Ni muungano uliodumu kwa miaka 50 sawa tunakubali.
Ila ni upuuzi,unafwiki,ukatili na udhalimu mkubwa kutoka kwa watawala hawa wenye nia ovu ya kukataa maoni yetu ya sasa juu ya kuhitaji serikali 3.
Sina nia wala ari ya kuufurahia huu muungano kwa ni naona unatuingizi madeni kwa taifa na kufilisi kodi zetu.
"willafrica"
 
Ni maadhimisho ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar au Maadhimisho ya Miaka 50 ya muungano wa Majeshi ya Tanganyika na Zanzibar?

Au ni miaka 50 ya Uongo unaolindwa na Majeshi?

Katibu muenezi mitandaoni wa UKAWA nje ya bunge, ndugu Ben Saanane
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom