Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022

Jamhuri baada ya kutathmini mwenendo wa mashahidi waliokuwa wanawaleta imeonekana:

1. Karibu madhahidi wote waliofuata baada ya Kingai kutoa ushahidi wake wamekuwa wanaharibu msingi wa ushahidi wa Kingai, hivyo wanaharibu kesi pasipo kudhamiria.

2. Kuna tetesi zilizagaa kuwa kuna mashahidi wasiopungua nane (wawili tayari walishatoa ushahidi wao) wamegeuka na kuwa kinyume na lengo la Jamhuri (Hostile witness)

3. Tathmini ya ushahidi na mashahidi waliofika mpaka sasa mahakama wamejikuta wakitoa siri za ndani za utendaji wa vyombo vya usalama ikiwemo JWTZ, TISS, Polisi, Magereza ma ofisi ya mwendesha mashtaka (kwa nchi hichi sio kitu kizuri sana, hakina afya).

4. Upo uwezekano mkubwa kwa muda unaotakiwa wa kuendesha kesi hii ukaisha kabla ya ushahidi wa jamhuri kukamilika kutolewa. (Hili ni suala la kitaalamu kidogo)

5. Lipo shinikizo kubwa sana kutoka mahali mahali linalotaka kesi hii ifutwe, sasa kuendelea kutoa ushahidi huku hilo shinikizo likiendelea kuwepo kunaipa jamhuri na ofisi ya mwendesha mashtaka wakati mgumu (progress dilemma), hivyo kufunga ushahidi mapema kunaweza kuharakisha hukumu kutolewa ili kuondokana na hilo shinikizo.
 
Naomba kama mheshimiwa Kibatala na wenzake wakiridhia sisi sote tuliofuatilia kesi mwanzo mpaka hapa ilipofika basi tupate hata certificate za Misingi ya Sheria mahakamani,
Tumejufunza vingi
Aisee siyo siri home ss hv hadi wananiita Kibatala mtu akizingua tu naanza kumpa yale maswali kama ya Kiba....utasikia sitaki maswali yako ya kina Kibatala.... kwa kifupi nina basic Cert ya Law kwa kupitia hii Case!!!
 
John mimi nakataa aisee. Wametukosesha uhondo. Nilikuwa nataka nisikie ushahidi wa Boaz maana ndiye kila kitu kwenye hii kesi. Ila nimejifunza mengi kuhusu sheria na ushahidi.
Aisee ingawa imewatesa akina Mbowe na wenzake lakini kesi hii imekuja na faida nyingi sana.

Nimejua namna mitandao ya simu inaweza kutumika kutoa ushahidi namna tunavyorekodiwa maongezi na miamala ktk saver za mitandao.

Nimefahamu kwa kifupi idara mbali mbali za jeshi la polisi za uchunguzi na baadhi kidogo jwtz.

Pia PGO

Hii ni module nzima pale Udsm Law schoo
 
Jamhuri baada ya kutathmini mwenendo wa mashahidi waliokuwa wanawaleta imeonekana:

1. Karibu madhahidi wote waliofuata baada ya Kingai kutoa ushahidi wake wamekuwa wanaharibu msingi wa ushahidi wa Kingai, hivyo wanaharibu kesi pasipo kudhamiria.

2. Kuna tetesi zilizagaa kuwa kuna mashahidi wasiopungua nane (wawili tayari walishatoa ushahidi wao) wamegeuka na kuwa kinyume na lengo la Jamhuri (Hostile witness)

3. Tathmini ya ushahidi na mashahidi waliofika mpaka sasa mahakama wamejikuta wakitoa siri za ndani za utendaji wa vyombo vya usalama ikiwemo JWTZ, TISS, Polisi, Magereza ma ofisi ya mwendesha mashtaka (kwa nchi hichi sio kitu kizuri sana, hakina afya).

4. Upo uwezekano mkubwa kwa muda unaotakiwa wa kuendesha kesi hii ukaisha kabla ya ushahidi wa jamhuri kukamilika kutolewa. (Hili ni suala la kitaalamu kidogo)

5. Lipo shinikizo kubwa sana kutoka mahali mahali linalotaka kesi hii ifutwe, sasa kuendelea kutoa ushahidi huku hilo shinikizo likiendelea kuwepo kunaipa jamhuri na ofisi ya mwendesha mashtaka wakati mgumu (progress dilemma), hivyo kufunga ushahidi mapema kunaweza kuharakisha hukumu kutolewa ili kuondokana na hilo shinikizo.
Nahisi simu imepigwa leo kutoka Brussels
 
Aisee siyo siri home ss hv hadi wananiita Kibatala mtu akizingua tu naanza kumpa yale maswali kama ya Kiba....utasikia sitaki maswali yako ya kina Kibatala.... kwa kifupi nina basic Cert ya Law kwa kupitia hii Case!!!
Basi ngoja ibaki hivyo
Mheshimiwa Kibatala ataona
 
Kesho tarehe 16 February 2022 Vichwa vya Habari Kurasa Za Mbele za Mitandao na Magazeti Yote:

JAMHURI YABWAGA MANYANGA (KUENDELEA) KUTOA USHAHIDI ...endelea kusoma kwa kina kurasa za ndani juu ya yaliyojiri ktk kesi namba 16/2021 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzie watatu ......
 
Wengi hawakujuwa kwamba Freeman Mbowe alikwenda Dubai kwa kibali.
Kuna wakereketwa wa lumumba fc humu walikuwa wanasema eti alitoroka mkono wa Chuma.

Mbowe is very smart in his actions.

Ndio Bilionea pekee mwanasiasa wa upinzani ambaye ni mdanya biashara hana doa lolote la kukwepa kodi hata jpm alimshindwa. Hakuwa na namna ya kumkamata zaidu ya kutumia ukatili
 
Wamefunga kesi mapema,mashahidi hawana ama hawana jipya.Ushahidi aliotuambia igp upo wapi sasa?
Upande wa Serikali haujatutendea haki! Binafsi, nilipenda KINGAI na BOAZ nao waje wakabiliane na maswali ya akina Kibatala, Nashon, Mtobesya nk. Huyo Swila, kuna maswali mengi ameshindwa kuyajibu, na kudai Boaz na Kingai ndiyo wanaojua! NIMEHUZUNIKA!
 
Nahisi simu imepigwa leo kutoka Brussels

Wadau wa maendeleo kutoka nje mbinyo wao kuhusu utawala bora / good governance umekuwa mkubwa, usiokoma na endelevu kiasi ya kuwa vyombo vya serikali ya CCM vimeshindwa kuhimili na kukubali kutafuta pa kutokea ...
 
Wamefunga kesi mapema,mashahidi hawana ama hawana jipya.Ushahidi aliotuambia igp upo wapi sasa?
Yaani wamefunga ushahidi bila hata ya kumwita yule ambaye tukio la ugaidi lirilipotiwa kwake, yaani DCI, mtiririko muhimu wa kuthibitisha mashtaka haya utakosekana, au wameogopa ndio watazidi kujichanganya, au wamemuonea huruma DCI kuburuzwa na Kibatala siku 3?
 
Lakini tulitakiwa pia tumsikie aliyemtuma Swila. Maana Home boy Urio na Swila wameongelea sana maelezo na kutumwa kwao na Boaz. Angekuwepo ili aongeze nguvu ya kumfunga Gaidi. Pia Homeboy alipeleka ushahidi moja kwa moja kwa Boaz. Tungemsikia pia
Tuta anza kuleta mshahidi soon. Shahidi wetu wa kwanza ni yule alie mdanganya Mh. Rais kwamba dunia itashangaa kwani ushahidi uko wa kutosha. Na Chadema wasione Mbowe kama Mungu.
Sasa Siro jiandae kama shahidi namba moja upande wa utetezi. Nawe sijui utaenda chooni mara ngapi?
 
Wamefunga kesi mapema,mashahidi hawana ama hawana jipya.Ushahidi aliotuambia igp upo wapi sasa?
Hawa mashahidi Urio na Swilla wameharibu sana sasa kama angeletwa shahidi mwingine baada ya huyu basi angeharibu zaidi ndo mana mawakili wa serikali wameona waishie hapo
 
Back
Top Bottom