Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,777
Wadau, amani iwe nanyi.

Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.

kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected

======================================================================================
UPDATES 1

Wadau, semina imechelewa kuanza kwa vile Kamati ya Mashauriano ilikuwa inaendelea na kikao chake. Kwa sasa kikao kimemalizika na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo James Mbatia, Steven Wasira, Askofu Donald Mtetemela na Sheikh Jongo wameingia Ukumbini. Ni wazi kuwa muda si mrefu Semina itaanza. Tuwe na subira

UPDATES 2
Bunge limeahirishwa hadi saa 10 jioni ambapo wwbunge wataridhia Rasimu ya Kanuni hizo baada ya zoezi la kuzipitisha kukamilika

UPDQTES 3
Wabunge wameanza kuingia abungeni tayari kwa kuanza kikao cha Kupitisha Rasimu ya Kanuni.
attachment.php
attachment.php

UPDATES 4
Mwenyekiti ameingia ukumbini huku idadi kubwa ya wabunge hawapo ukumbini kama picha hiyo hapo chini inavyoonekana
attachment.php

UPDATES 5
Bunge limesimama kwa muda ili kusubiri wabunge wengi waingie ukumbini. Wakati huo huo Rasimu ya Kanuni zinagawiwa kwa wabunge.

UPDATES 6
Bunge limeahirishwa mpaka saa 12 jioni kutokana na zoezi la kudurufu Kanuni za Bunge kutokamilika
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    697.7 KB · Views: 11,434
  • image.jpg
    image.jpg
    621.2 KB · Views: 11,067
  • image.jpg
    image.jpg
    648 KB · Views: 10,821
Barabara kabisa raia mwenzangu (nimekwepa kusema Mtanganyika au Mzanzibari kwa nia njema ya kushirikiana ktk hili), hamjambo ndugu wana jf, karibuni na tuko pamoja, tunasubiri tu muda muafaka utimu ili tushuhudie yaliyoridhiwa na kamati ya mashauriano.
 
fafanua ni raia mwenzako wa Tanganyika au zenjibar????
 
Posho watachukua saa ngapi???siku ya 21 leo,hawana jipya wehu hao

Kulingana na mtiririko wa matukio ya uchukuaji posho toka bunge limeanza, nimekua nikiona wanapewa posho jioni, kwa hivyo nadhani posho itakua jioni.
 
Barabara kabisa raia mwenzangu (nimekwepa kusema Mtanganyika au Mzanzibari kwa nia njema ya kushirikiana ktk hili), hamjambo ndugu wana jf, karibuni na tuko pamoja, tunasubiri tu muda muafaka utimu ili tushuhudie yaliyoridhiwa na kamati ya mashauriano.
Pamoja sana Mkuu, kwa sasa niite tu Mtanzania kwani ndo kiungo chetu sote. Tuwe pamoja na tushirikiane katika hili ili jahazi lifike salama
 
Wadau, amani iwe nanyi.

Kama kawaida yetu tutaendelea kuwaletea mtiririko wa mijadala Bungeni Dodoma. Kwa sasa Bunge lipo kwenye mchakato wa kukamilisha kupitisha vifungu vya Kanuni za Bunge. Mtakumbuka kuwa vifungu vyote 87 vimepitishwa isipokuwa kifungu cha 37 na 38 ambavyo kwa ujumla wake vinahusu ufanywaji wa maamuzi ndani ya Bunge Maalum. Mjadala hapa ni ama matumizi ya Kura ya Wazi au ya Siri. Mtakumbuka kuwa siku ya Ijumaa ya tarehe 7 Machi, Mwenyekiti Kificho aliunda Kamati ya Mashauriano kuhusu vipengele hivyo. Kamati bado haijamaliza kazi yake na leo wanaendelea na mashauriano. Semina kwa siku ya leo itaendelea kuanzia saa 5 Asubuhi mara baada ya Kamati ya Mashauriano kumaliza kazi yake.

kama kawaida, nitakuwa sambamba na wadau wengine kuwaletea updates zote. Natarajia kupata ushirikiano kutoka kwa mdau wetu ambaye ni Mbunge wa Bunge hili Maalum, Simiyu Yetu. Pia kwenye Mjadala, natarajia kuwaona akina Skype na MaishaPesa. ​Stay Connected

tunataka full update mkuu
 
Naomba kupewa dondoo kuhusu maridhiano yaliyofikiwa ktk vifungu vya 37 na 38 kabla semina haijaanza.

cc. Chabruma
cc. MaishaPesa
cc. Simiyu Yetu
cc. Mjumbe mwingine yeyote mwenye kujua hili
 
Last edited by a moderator:
niko ofisini na kwa bahati nzuri ofisi yetu ina tv. kwa muda huo wa saa tano itanipasa niombe ruhusa kwa kazi maalumu ya kuona nini wawakilishi wetu wanachotaka kuamua kwa maslahi ya Taifa ukizingatia kutishana kushakuwa kwingi
 
Hapo kwenye kutishana ndipo panapotaka kuharibu mchakato kabisa, hivi wanaotishia lengo lao nini hasa?
 
vp bunge wanarusha live au ndo magumashi sielewi ccm washenzi na wahuni wakubwa kuna uwezekano kikao cha leo wasionyeshe live.
 
Hapo kwenye kutishana ndipo panapotaka kuharibu mchakato kabisa, hivi wanaotishia lengo lao nini hasa?

Mkuu Skype mi toka siku wanaanza mchakato wa masuala ya kanuni bungeni nimeona masuala ya vitisho yakipamba moto siku hadi siku na wala sijui ni nini kitatokea leo. LENGO LA VITISHO NI KULINDA Maslahi ya wachache mkuu. Namuomba Mola atuepushe na balaa ambalo kimsingi naona kama lanukianukia hivi
 
Amina.
 
Back
Top Bottom